Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Profesa Posi aanza kuonja mikikimikiki
Profesa Posi aanza kuonja mikikimikiki
By Habari Tanzania | Published  11/25/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Magreth Kinabo

MKURUGENZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC), Profesa Mwajabu Posi, ameanza kuonja machungu ya migomo ya wanafunzi vyuoni.

Katika mkutano kati ya uongozi na wanafunzi uliofanyika chuoni hapo jana, Profesa Posi alijitahidi kujenga hoja za kuwaridhisha wanafunzi, lakini bado akawa katika wakati mgumu.

Alijitahidi kutoa ufafanuzi wa fedha zilizotolewa chuoni hapo kwa ajili ya mafunzo ya vitendo, lakini wanafunzi wakawa hawataki kupokea kiasi wanachopewa sasa.

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanapewa sh 18,000; ilhali wa mwaka wa pili na wa tatu wakipewa sh 30,000 badala ya sh 120,000.

“Leo tumeshapata fedha zenu, ziko tayari tumefanya kama mlivyotutuma, lakini wanafunzi wa mwaka wa kwanza watapata kiwango cha sh 18,000 kwa kuwa hawakuwapo kwenye mapendekezo ya maombi ya vifaa hivyo.

“Ila wa mwaka wa tatu tutawapatia sh 30,000 kwa kuwa ndio waliokuwapo wakati huo,” alisema Profesa Posi.

Wanafunzi hawakufurahishwa na taarifa hiyo, hivyo walianza kupaza sauti.

Mwanafunzi Abdallah Selemani wa mwaka wa tatu, aliendelea kudai maelezo, akitaka kujua sababu za kupewa kiasi kidogo, na kiongozi aliyeamua hivyo.

Mkurugenzi huo aliamua kutoa maelezo zaidi kwa kusema kuwa mapendekezo waliyoyaomba yako kwenye mchakato.

Naye, Makamu Mkuu wa IJMC, Anastazia Rugaba, alisema: “Kwani hakuna binadamu ambaye si mkosaji au msahaulifu?

“Ninaomba tuelezwe kuwa nini kinafanyika, ili kupata ufumbuzi huo ili wanafunzi waendelee na masomo,” alisema.

Mkurungezi huyo baada ya kuona bado wanafunzi hawaridhiki na majibu, alimpa nafasi Mhasibu wa Chuo aliyejulikana kwa jina la Ngoma ili atoe maelezo.

“Tuliamua tuwape fedha hizo kwanza,” alisema Ngoma.

Jibu hilo nalo halikuwaridhisha, ndipo wanafunzi hao walipoomba uongozi wa Bodi ya Mikopo uende chuoni hapo kutoa ufafanuzi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.