Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ububu wa serikali washtua mataifa makubwa
Ububu wa serikali washtua mataifa makubwa
By Habari Tanzania | Published  11/25/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu

HATUA ya Serikali ya Awamu ya Nne kukaa kimya pasipo kuweka bayana hatua zozote za wazi dhidi ya tuhuma kadhaa zinazoelekezwa kwa taasisi kadhaa za umma na watendaji wake, sasa zinaonekana kuanza kuishtua jumuiya ya kimataifa.

Kinachoonekana kuishtua jumuiya hiyo ya kimataifa, ni kile kinachoonekana kuanza kutoweka taratibu za matumaini makubwa ambayo yalijengwa na Serikali ya Awamu ya Nne kabla na baada ya kuingia madarakani.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka kwa nchi mbili wanachama wa Umoja wa Ulaya zinaonyesha kwamba, mataifa hayo yameshaanza kutafakari hatua za kuchukua dhidi ya serikali kutokana na hatua yake ya kutokuwa tayari kuweka bayana masuala kadhaa ambayo yanaonyesha kuwapo kwa walakini katika misingi ya utawala bora.

Miongoni mwa mambo ambayo yamesababisha mataifa hayo kufikia hatua hiyo ni pamoja na serikali kukaa kimya pasipo kusema lolote au hata kuchukua hatua zozote dhidi ya watendaji wake wanaohusishwa na kashfa kadhaa za ubadhirifu wa mali za umma.

“Tangu serikali hii iingie madarakani, vyombo vya habari vimekuwa vikiandika mambo mengi mazito yanayohusu matumizi mabaya ya fedha za umma, habari ambazo zinaonekana kufa kifo cha kawaida,” kilisema chanzo kimoja cha habari kutoka katika ubalozi mmoja wa nchi za Scandinavia.

Habari zaidi ambazo Tanzania Daima inazo, zinaeleza kwamba, hivi sasa serikali moja ya nchi za Scandinavia ambayo imekuwa rafiki mkubwa wa kihistoria na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeshaanza kufikiria kuhusu kuweka vikwazo vya kiuchumi, kushinikiza hatua kuchukuliwa.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima inazo zinaeleza kwamba, ofisa mmoja wa juu wa ubalozi kutoka nchi hiyo, alisafiri hadi Dodoma ambako kikao cha Bunge kilikuwa kikikutana hivi karibuni na akazungumza na wabunge kadhaa kuhusu uwezekano wa serikali yake kuanza kuitenga Tanzania.

Mmoja wa wabunge aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini, alikiri kukutana na ofisa wa nchi hiyo ambaye alimweleza bayana kuhusu hatua ambazo nchi yake inafikiria kuzichukua.

Hata hivyo, chanzo chetu kingine kililieleza gazeti hili kwamba, uamuzi wa nchi hiyo kufikia hatua hiyo, ulikuwa utangazwe na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa nchi hiyo, ambaye alikuwa akitarajia kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa.

Wakati nchi hiyo ya Scandinavia ikieleza kusikitishwa na mwenendo wa mambo serikalini na hususan usiri katika kufikiwa kwa maamuzi, jana ofisa wa juu wa ubalozi mwingine wa Ulaya alifika katika chumba cha gazeti hili na kueleza kuwapo kwa dhamira kama hiyo kutoka katika serikali yake.

Ofisa huyo wa ubalozi aliieleza Tanzania Daima kuhusu hofu yao ya kukwama kwa ahadi ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa, bungeni ya kuwaomba wabunge wamwachie kilio walichompa ambacho kilihusu ufisadi ndani ya Maliasili na Utalii.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, uamuzi wake wa kuja katika chumba cha gazeti hili, ulikuja baada ya viongozi wake kusoma habari nyingine zilizokuwa zikihusu ubadhirifu mkubwa ndani ya Idara ya Wanyamapori zilizokuwa zimeandikwa na Tanzania Daima jana na juzi.

“Yameandikwa mambo mengi, tumeyafuatilia kwenye vyombo vya habari, hasa gazeti lenu. Tunashangaa kuona hakuna majibu ya serikali,” alisema ofisa wa ubalozi huyo na kuongeza:

“Kwa sababu za kidiplomasia, tunaomba usitunukuu sasa, lakini tunajiandaa kutoa taarifa.

“Hii ni kati yangu na wewe. Serikali inapaswa kuwa inatoa maelezo kuhusu tuhuma zinazotolewa na vyombo vya habari.

“Mambo kama haya katika nchi yetu, yakitolewa asubuhi, jioni serikali inajibu, ama kwa kukanusha, au kwa kueleza ukweli wa mambo, hapa si hivyo, lakini sisi tukiwa miongoni mwa wafadhili wakuu, tunajitahidi kulifuatilia suala hili,” alisema.

Mbali ya hilo, ofisa mwingine kutoka ubalozi mkongwe hapa nchini jana hiyo hiyo (jina tunalihifadhi kwa sasa), alifika katika ofisi za Tanzania Daima, Mtaa wa Mkwepu, akitaka asaidiwe vielelezo na rejea za ripoti mbalimbali za uchunguzi.

Miongoni mwa mambo ambayo ubalozi huo ulitaka kupata nakala zake ni pamoja na ripoti ya Tume ya Wabunge iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo, ambayo imekaliwa hadi sasa.

Habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaeleza kwamba, ndani ya ripoti hiyo kumeainishwa ufisadi wa kila aina unaofanywa ndani ya Idara ya Wanyamapori ambao gazeti hili umekuwa ukiandika habari zake kwa siku kadhaa sasa.

Mara zote ripoti za kitaifa na kimataifa zimekuwa zikionyesha kwamba, Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi, ambazo iwapo zitasimamiwa vizuri na kwa uzalendo, hakuna sababu za kuifanya iendelee kuwa masikini.

Wakati nchi hizo zikianza kufuatilia mambo hayo, tayari Benki ya Dunia, imetoa ripoti ikiainisha jinsi nchi inavyopoteza mabilioni ya shilingi kila mwaka kutokana na njama zinazowahusisha viongozi ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii, na wageni waliohodhi vitalu vya uwindaji wa kitalii hapa nchini.

Ripoti mbalimbali za uchunguzi zimebaini kuwa Tanzania ndiyo nchi isiyofaidika na uwindaji wa kitalii kutokana na sababu mbalimbali zilizo wazi kabisa.

Miongoni mwa sababu hizo, ni bei ndogo ya uwindaji wa wanyama. Wakati hapa nchini tembo anauawa kwa malipo ya dola 4,000 za Marekani; nchini Botswana mnyama huyo hauawi hadi mtalii alipe dola 19,000.

Simba hapa nchini anauawa kwa dola 2,000; ilhali Botswana anauawa kwa dola za Marekani zaidi ya 5,000.

Kundi la Wadau wa Maendeleo Tanzania (DPG), limetoa ripoti likisema kuna mtandao mkubwa wa usiri kati ya viongozi wa Idara ya Wanyamapori ambao wanashirikiana na wageni wanaomiliki vitalu.

Limesema kuna mapendekezo mazuri yalitolewa miaka 11 iliyopita, lakini Idara hiyo, chini ya Emmanuel Severe, imekataa kuyatekeleza.

Mapendekezo hayo yalihusu mabadiliko ya sera na menejimenti; na kwamba yalihusu kuufumua muundo mzima wa Idara ili uweze kuwatendea haki wadau, hasa Watanzania wazalendo, lakini hakuna kilichotekelezwa.

Kwa hali ya sasa, idara hiyo inaongozwa kwa nguvu kubwa za mamlaka alizonazo Mkurugenzi, jambo ambalo linapingwa hata na wafadhili.

Vitalu vimeendelea kutolewa kwa utashi wa viongozi, badala ya kuruhusu ushindani wa haki kwa wote wenye sifa ya kuendesha uwindaji wa kitalii.

Benki ya Dunia nayo imeyaona hayo, na imependekeza mabadiliko makubwa yafanywe.

Kwa sasa mchango wa Idara ya Wanyamapori ni wastani wa sh bilioni 10 kwa mwaka, kiasi ambacho wachunguzi wa mambo wanasema ni kidogo mno. Kama ukiwapo udhibiti mzuri, kiasi hicho kinastahili kiwe mara tatu


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Eng. Magafu, F.F)
    Rating
    Tatizo kubwa la Watanzania ni ujinga. Tuko wajinga mno kiasi ambacho hatujui tofauti ya A na B.
    Mimi ni mwanachama wa CCM lakini kwa mwendo huu wa serikali ya Kikwete. Hatuwezi kufika. Hakuna maisha bora wala nini ila ni maisha duni tu. CHADEMA walitupa TAFSIRI halisi ya neno kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya. Wakati wa kupiga kura watu wakaangalia uzuri wa sura. Well, hii miaka mitano tumepoteza bure... Je, ifikapo mwaka 2010 tutafanya tena makosa haya? Mbuzi na kodoo ni lazima watengwe lakini ... Kama Nyerere alivyosema bado tuna tatizo la adui ujinga. Tunaweza kukosea ila kurudia makosa ni kosa kubwa!!! 2010 Tutarudia makosa??????
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.