Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kikwete ataka Jeshi la Wananchi imara
Kikwete ataka Jeshi la Wananchi imara
By Habari Tanzania | Published  11/24/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imedhamiria kujenga na kuimarisha uwezo wa jeshi lake ili kuweza kulinda mipaka na watu wake kwa ukamilifu.

Rais Jakaya Kikwete aliwaambia wapiganaji na askari wa vikosi mbalimbali vya jeshi la Wananchi la Tanzania baada ya kushuhudia mazoezi ya jeshi hilo yaliyofanyika juzi Msata mkoani Pwani, zoezi lililotambuliwa kama “Operesheni Pima Uwezo”

“Mafunzo na mazoezi ndiyo uhai wa jeshi lolote duniani, hatuna uwezo mkubwa, lakini lazima tujenge uwezo wa jeshi letu kwa zana, vifaa na huduma ili kuweza kuwa tayari kivita, ninayatambua matatizo hayo na tunajipanga kuyatatua.”

Lengo la zoezi hilo la kijeshi lilikuwa ni kutoa mafunzo na mazoezi kwa wapiganaji ili kuwaweka tayari kivita na katika shughuli zozote katika jamii zinazohitaji uwezo na utaalamu wa jeshi.

Zoezi hili limehusisha wapiganaji 1,750 kutoka vikosi mbalimbali vikiwemo vya anga, miguu, mizinga, mgambo na Jeshi la Kujenga Taifa .

Rais aliongozana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya, Mkuu wa Majeshi, Jenerali George Waitara, na Mnadhimu Mkuu, Luteni Jenerali Davis Mwamunyange. Wengine ni Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita, Meja Jenerali Hamis Semfuko na Kamanda wa zoezi, Brigedia Jenerali Servatus Hinda.

Rais alilipongeza jeshi na kusisitiza kuwa lazima liwe tayari wakati wote na wala sio kusubiri vita ndiyo lianze kujijengea uwezo.
Aliwataka wawe makini wakati wote katika mafunzo na mazoezi kwani ndiyo njia pekee inayoliweka jeshi katika hali ya utayari kivita.

Akimkariri mkuu wa majeshi, Kikwete alisema, "Mkuu wa majeshi amesema 'mafunzo ni ghali lakini hakuna mbadala, tunafanya mafunzo wenyewe kwa wenyewe na wenzetu pia kwa nia ya kujipima kiuwezo tayari kuilinda nchi yetu, yote haya yanatuongezea uwezo na maarifa na pia kupimana."

Rais alieleza azma yake kuwa kunapokuwa na brigedi basi iwe imekamilika kama sheria na kanuni za jeshi zinavyoelekeza.

Mapema akimkaribisha Rais Kikwete, Jenerali Waitara alisema mazoezi katika JWTZ huanza Januari hadi Desemba kila mwaka kwa nia ya kuwapa mbinu mbalimbali askari na jinsi ya kuzitumia mbinu hizo ili kuimarisha jeshi.

Wakati huo huo, Rais Kikwete kesho, anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini Uganda kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni.

Lengo la ziara hii ni kufanya mazungumzo kuhusu nchi hizi mbili na nafasi ya nchi hizi katika ushirikiano wa Afrika Mashariki, hali ya kisiasa katika eneo la maziwa makuu na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.

Hii itakuwa ziara ya tatu nchini humo tangu kupewa madaraka ya urais Desemba 21, 2005. Rais alifanya ziara nchini Uganda kwa mara ya kwanza Machi mwaka huu kwa nia ya kujitambulisha nchini humo kama kiongozi mpya wa Tanzania na alipohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Museveni Mei 11 mwaka huu.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.