Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wananchi kuanzisha mbuga za wanayama
Wananchi kuanzisha mbuga za wanayama
By Habari Tanzania | Published  11/24/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi Wetu

WANANCHI wa Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara wameshauriwa kushirikiana kuanzisha hifadhi za wanyamapori ili kuzuia uwindaji haramu na kuviongezea vijiji vyao mapato.

Wito huo umetolewa jana huko Orkesumeti na Mshauri wa Maliasili katika Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara, Mashughuli Minja, kwenye mkutano wa wadau wa kilimo, mifugo, maliasili na mazingira wilayani Simanjiro.

Mkutano huo ulilenga kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo, mifugo na utunzaji wa mazingira wilayani humo, kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira na uwindaji haramu unaoendelea hivi sasa.

Mashughuli alisema uanzishaji wa hifadhi za jamii za wanyamapori utawanufaisha wananchi kwa kupata asilimia 75 ya
mapato yote yanayotokana na uwindaji katika hifadhi hizo na kuzuia uwindaji haramu.

“Hakuna njia nyingine ya kuzuia uwindaji haramu na kunufaika kikamilifu bila kuanzisha hifadhi za jamii za wanyamapori,” alisema.

Alifahamisha kuwa pamoja na kuwaongezea kipato, kuanzishwa kwa hifadhi hizo kutasaidia kuhifadhi mazingira kwa ajili ya mifugo yao na wanyamapori.

Wilaya ya Simanjiro inaongoza mkoani Manyara kwa uwindaji haramu na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji ovyo miti kwa ajili ya kuni na uchomaji mkaa.

Hali hii inachochewa na wilaya hiyo kuwa mpakani na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro yenye upungufu wa ardhi kwa ajili ya kilimo na nishati, ambapo watu hukimbilia huko kupata ardhi, mkaa na kuni kwa matumizi mbalimbali.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.