Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mgawo wa umeme hadi Agosti 2007
Mgawo wa umeme hadi Agosti 2007
By Habari Tanzania | Published  11/23/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Kulwa Karedia

MGAWO wa umeme nchini utaendelea hadi Agosti, 2007, mamlaka husika imethibitisha.

Ofisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Daniel Mshana, amesema ingawa mgawo halisi unakusudiwa kumalizika muda huo, makali yake hayatakuwa kama haya wanayopata wananchi sasa.

Mshana alisema hayo jana asubuhi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha ‘Power Breakfast’ kinachorushwa hewani na redio ya Clouds FM, yenye makao yake Dar es Salaam.

Alisema Bwawa la Mtera limefungwa, wakati Bwawa la Nyumba ya Mungu na Bwawa la Kihansi; kina cha maji hakiwezi kuendesha mitambo inayozalisha umeme.

“Hali ya sasa ya upatikanaji umeme nchini imezidi kuwa ngumu kwa sehemu fulani, tunategemea kuwa mgawo huu utaendelea hadi Agosti mwakani, ambako mitambo ya kukodi itakuwa imeanza kuzalisha kwa kiwango kikubwa,” alisema Mshana.

Alisema kwa siku za karibuni, TANESCO inategemea zaidi umeme unaotokana na maji ya Mto Pangani. Unazalisha megawati 68.

Alisema baada ya kina cha maji kushuka katika bwawa hilo, hali ya mgawo imezidi kuwa mbaya, sambamba na kuharibika kwa mtambo wa Kampuni ya Songas.

“Naamini kama tutafanikiwa kujiunga na gridi ya Zambia, tunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa suala hili la mgawo, lakini pia itakuwa njia nzuri kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) katika kupambana na suala hili,” alisema Mshana.

Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa, unapata huduma ya umeme kutoka Zambia.

Kuhusu Kampuni ya Richmond, iliyoingia mkataba wa kuzalisha umeme, Mshana hakuwa tayari kuizungumzia kwa undani, ingawa alikiri kuchelewa kwa kampuni kuanza uzalishaji wa umeme. Mahitaji ya umeme kwa nchi nzima ni megawati 580.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Hawa jamaa wa awamu ya nne wanatuyeyusha. Wanaendesha nchi kisanii, huyu JK si alituahidi mambo ya mgao yataisha hivi karibuni?,sasa kila siku wanatujia na jipya. Mzee Ben yeye alakuwa kimya,ila mambo yakawa yanaenda, hawa jamaa kila siku kelele nyingi, mambo hayaendi. Huo ndio usanii wenyewe.Na hii ishu ya Richmond, kuna nyepesi mtaani zinazosema Mtoto wa Lowassa anahusika,ila ni nyepesi tu, hazina uthubitisho. Ila mambo yanayosemwa semwa mtaani huwa yana ukweli wake.Kwahiyo mimi naona ingawa wananchi wanamategemeo makubwa sana na huyu JK na wenzake,na wao maneno yamekuwa mengi, ahadi nyingi ila hakuna kitu,watu watakuja kumkumbuka mzee Ben tu.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.