Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbaroni kwa kuoa mwanafunzi
Mbaroni kwa kuoa mwanafunzi
By Habari Tanzania | Published  11/22/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Gasper Andrew, Singida
POLISI mkoani Singida wanamshikilia kijana mmoja, mkazi wa Kijiji cha Manguamitogho, kwa tuhuma ya kumuoa mwanafunzi wa darasa la tano wa Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Celina Kaluba, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Novemba 18, mwaka huu, baada ya mwanafunzi huyo kutoa taarifa Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa kuhusu mjomba wake kumlazimisha kuolewa na kijana huyo.

Kamanda alisema mtuhumiwa huyo anakabiliwa na tuhuma mbili, ambazo ni kumzuia mwanafunzi kuendelea na shule na kumbaka.

Kwa mujibu wa Kaluba, mtuhumiwa alitarajiwa kufikishwa mahakamani juzi mchana na wakati huo huo, msako umeanzishwa kwa ajili ya kumkamata mjomba wa mwanafunzi huyo.

Kamanda huyo aliwashauri viongozi wa madhehebu ya dini wenye dhamana ya kufungisha ndoa, kuwa waangalifu na kuacha kufungisha ndoa za wasichana wenye umri mdogo na hasa wanafunzi.

Kamanda Kaluba aliwaonya wazazi wenye tamaaza mali kuacha kuwaoza watoto wa shule mpaka watakapomaliza masomo.

Mwanafunzi huyo alilimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa yeye na mtoto wa mjomba wake walifika Singida mwishoni mwa Agosti mwaka huu kwa ajili ya kuhani kilio cha mama yake mzazi, ndipo mjomba wake akachukua mahari kwa siri na kumuoza.

Alisema alipofika Singida, alimkabidhi mjomba wake Sh70,000 amtunzie ili azitumie wakati wa kurudi Dar es salaam lakini baada ya siku chache, aligundua kuwa fedha zake zimekwishatumiwa, na mjomba wake akamtaarifu kuwa amekwishapokea mahari yake, hivyo asiwe na ndoto ya kurudi jijini.

Alisema pamoja na kukataa kuolewa kwa sababu bado ni mwanafunzi na pia hawezi kuolewa na mtu ambaye hamfahamu, mjomba wake alimlazimisha na kumpeleka kwa nguvu msikitini ambapo alifungishwa ndoa na Sheikh wa kijiji.

“Wakati nalazimishwa kuolewa, pia mtoto wa mjomba ambaye tuna umri sawa wa miaka 15, naye aliozwa kwa nguvu,” alisema mwanafunzi huyo na kuongeza kuwa inaelekea mwenzake hataki tena shule kwa sababu amekuwa kimya na anaishi na mume huyo wa kulazimishwa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.