Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Anayedaiwa gwiji la mihadarari kizimbani
Anayedaiwa gwiji la mihadarari kizimbani
By Habari Tanzania | Published  11/21/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Irene Mark

HOJA za Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mpakanjia (CCM), kuhusu vita dhidi ya biashara ya mihadarati, zimeanza kufanyiwa kazi.

Mmoja wa watuhumiwa wa mtandao wa biashara hiyo, alifikishwa mahakamani jana. Ingawa haijatamkwa, lakini kuna tetesi kuwa hayo ni matokeo ya ‘kelele’ za mbunge huyo.

Aliyesimamishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu jana ni mfanyabiashara James Mkami au Chacha (29), ambaye anatuhumiwa kufadhili wauza mihadarati.

Ilidaiwa na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Charles Kenyella, kwamba katika kipindi kisichojulikana, wilayani Kinondoni, mtuhumiwa alimpa mihadarati aina ya heroin, Noel Mapunda, na kumwezesha kuiuza.

Kenyella, aliiomba mahakama izuie dhamana kwa mtuhumiwa kwa kuwa serikali ipo kwenye vita dhidi ya wasambazaji na wauzaji wa mihadarati.

Mbele ya Hakimu Mkazi Pellagia Khaday, SSP Kenyella, alidai kwamba, hati ya kiapo iliyotolewa mahakamani hapo na ofisa wa polisi, Valentino Mlowola, mtuhumiwa ni mmoja kati ya wasambazaji na wauzaji wakuu wa mihadarati wilayani Kinondoni.

Alidai kwamba, hati hiyo imeeleza pia kuwa mtuhumiwa anahifadhi kiasi kikubwa cha mihadarati, ambacho kiasi na aina yake, havijajulikana.

Hati hiyo ilieleza kwamba, upande wa Jamhuri unaamini kuwa mtuhumiwa anao mtandao mkubwa wa usafirishaji, usambazaji na uuzaji wa mihadarati nje na ndani ya nchi.

Alidai kwamba mtuhumiwa akipewa dhamana, atatibua upelelezi wa kesi inayomkabili.

Akijibu hoja za pingamizi la dhamana kwa mtuhumiwa huyo, wakili wa kujitegemea Samson Mbamba, alidai kwamba dhamana ni haki ya msingi ya mtuhumiwa kwa kuwa tuhuma zinazomkabili, kisheria hazizuii kupewa dhamana.

Wakili huyo alidai kwamba hati ya kiapo si hirizi, hivyo inaweza kukataliwa.

Alisema hati hiyo inaonyesha jinsi muapaji asivyokuwa na vielelezo; na kwamba anaamini zaidi maneno ya wasiri wake, hali inayoonyesha kuwa kuna mpango wa kumkandamiza mteja wake.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa Novemba 13, mwaka huu na tangu wakati huo alikuwa mahabusu ya polisi.

Baada ya hoja za pingamizi la dhamana na majibu ya wakili, Hakimu Khaday aliahirisha shauri hilo hadi leo atakapolitolea uamuzi wa dhamana.

Amina amesimama kidete katika mapambano dhidi ya mihadarati, na aliahidi kutoa ushirikiano kwa polisi ili waweze kutokomeza biashara hiyo inayoliangamiza taifa.
Kwa mujibu wa maelezo ya mbunge huyo, tayari ameanza kupokea vitisho kutoka kwa wahusika wa biashara hiyo


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.