Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Makambako wakerwa na katakata umeme
Makambako wakerwa na katakata umeme
By Habari Tanzania | Published  06/5/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Baadhi ya wafanyabiashara katika mji mdogo wa Makambako mkoani Iringa, wametishia kuliburuza kortini Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kudai fidia ya mamilioni ya shilingi,kwa madai ya kuwasababishia hasara kubwa.

Hasara hiyo inatokana na kukatiwa umeme mara kwa mara bila sababu za msingi.
Walisema atafungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, Jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na Nipashe, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao Bw. Philimon Bimbigah, alidai kwamba kwa takriban miezi mitatu sasa wamekuwa wakipeleka ankara za kulipa umeme, lakini bila kupata huduma hiyo.

Bw. Bimbigah alisema pia kwa zaidi ya miezi mitatu sasa wakazi wa mji huo mdogo wa Makambako wamekoseshwa huduma hiyo muhimu bila kupewa taarifa na wahusika wa shirika la TANESCO mkoa wa Iringa.

Maofisa wa TANESCO mkoani Iringa, walikiri adha inayowakabili wafanyabiashara hao pamoja na baadhi ya wakazi wa mji wa Makambako na vitongoji vya jirani.

Hata hivyo, maofisa hao wa TANESCO walisema hali hiyo inachangiwa na ukosefu wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya kuzalishia umeme.

Meneja wa TANESCO mkoani Iringa aliyejitambulisha kwa jina moja la Bw Mpanduji, alisema hali hiyo inasababishwa na upungufu wa mafuta ya kuendeshea mitambo iliyopo katika kijiji cha Uwemba.

Pia, alisema hali hiyo inachangiwa na mabadiliko ya kampuni ya TANWAT kuzuia usambazaji wa umeme katika kipindi cha miezi sita.

Kuhusu suala la ankara za wateja kuendelea kudaiwa licha ya kutopata huduma hiyo, alisema kimsingi zilipaswa kubadilika ili zilingane na matumizi halisi.

Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO wilayani Njombe, Bi, Ngairo alisema suala hilo limetokana na baadhi ya maeneo kuwa mbali na mtambo wa kuzalisha umeme ikiwemo Makambako.

Hata hivyo, alisema suala la usambazaji umeme katika mji wa Makambako, linashughulikiwa na uongozi wa TANESCO Makao Makuu.

Pia alisema tatizo hilo la Makambako linafahamika vema na Waziri wa Nishati na Madini,. Dk. Ibrahim Msabaha.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Bi. Halima Kihemba, alithibitisha kuwepo kwa tatizo hilo kwa wananchi wa mji wa Makambako.

Alieleza kuwa tayari amewaagiza maofisa wa TANESCO kushughulikia haraka suala hilo na kulitafutia ufumbuzi.

’’Hata mimi nimeshangazwa na taarifa kwamba TANESCO wanakata umeme wakati hakuna mgao katika kipindi hiki.

Ila nimepewa taarifa na Meneja wa Wilaya Bi. Ngairo kuwa wanakata kwa muda usiojulikana kutokana na ukosefu wa mafuta, hivyo niwataarifu wananchi wa wilaya yangu,’’ alisema.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.