Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mradi wa umeme Mnazi Bay kukamilika Desemba
Mradi wa umeme Mnazi Bay kukamilika Desemba
By Habari Tanzania | Published  11/20/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Oswald Rutaihwa, Mtwara

WAKAZI wa miji ya Mtwara na Lindi wataanza kutumia umeme wa uhakika utakaotokana na gesi ya Mnazi Bay, baada ya Kampuni ya Artumas Group ya Canada, kukamilisha sehemu kubwa ya mradi huo.

Rais Kikwete ambaye yuko mkoani hapa kwa ziara ya kikazi, aliweka jiwe la msingi katika kituo cha jenereta za uzalishaji wa umeme wa gesi ya Mnazi Bay na kuwaambia wakazi wa Mtwara kuwa baada ya ndoto ya kupatikana kwa nishati hiyo ya uhakika katika mikoa ya Mtwara na Lindi kutimia, kilichosalia ni kuhakikisha inachochea maendeleo ya viwanda.

Mradi huo ambao unatumia gesi inayochimbwa eneo la Msimbati, katika Wilaya ya Mtwara Vijijini unatarajiwa kuzalisha megawati 24 pindi utakapoanza Desemba 8, mwaka huu.
Wawekezaji wamewekeza zaidi ya Sh120 bilioni na hadi kukamilisha kazi ya usambazaji wa umeme zitatakiwa Sh20 bilioni nyingine.

"Umeme utakuwa wa uhakika, ndoto imetimia na ukombozi umetimia, nawashukuru Artumas Group kwa kuweza kuvumilia vikwazo walivyokumbana navyo wakati wa utekelezaji wa mradi huu," alisema Rais Kikwete bila ya kufafanua vikwazo hivyo.

Aliisifu kampuni ya hiyo kwa kuhakikisha kuwa mradi huo unatoa ajira kwa Watanzania 400 na kuwapongeza kwa kuwasimamisha hadharani aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdulrahmani Kinana na Anold Kileo ambao ni wajumbe wa Bodi ya Artumas Group kwa maelezo kuwa uwakilishi wao unazingatia maslahi ya nchi.


Aliitaka Tanesco kuhakikisha linaunganisha mtandao wa nyaya kati ya mkoa wa Mtwara na Lindi, ili miji hiyo iweze kupata umeme kwa wakati mmoja mara utakapoanza kutumika.

Alishutumu urasimu wa watendaji katika suala zima la kusambaza umeme huo na kusema,"rasilimali zipo, tatizo ni kwa watu waliopewa dhamana."


Hata hivyo, Rais Kikwete alisema serikali imelazimika kutoa ruzuku ya Sh14.5 bilioni ili kuwawezesha watumiaji wa umeme huo kulipia gharama sawa na ule unaozalishwa na Tanesco.

Bei ya umeme unaozalishwa na Tanesco ni dola senti 8 kwa uniti, wakati uzalishaji wa umeme wa gesi ya Mnazi Bay bila ya ruzuku ya serikali ni dola senti 12 kwa uniti. Hivyo serikali inalipia dola senti 4 kwa kila uniti itakayotumiwa na mteja.

Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alisema wizara yake itawasilisha serikalini mapendekezo ya jinsi ya kutumia gesi ya ziada inayotokana na visima vya Mnazi Bay.
Alisema hadi sasa kiasi cha gesi kilichopatikana katika visima viwili, kinatosha kwa kuzalisha megawati 24 za umeme na kwamba inaweza kutumika kwa miaka 20 na kwamba hivi sasa uchimbaji wa kisima cha tatu umeanza.

Alisema mradi huo unajumuisha uendelezaji wa visima vya gesi na mitambo ya kusafirisha gesi, ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kupitia baharini na nchi kavu lenye urefuwa kilometa 27 kutoka Msimbati hadi Mtwara.

Mradi huo pia unajumuisha ujenzi na ufungaji wa jenereta za kuzalisha umeme zenye uwezo wa kuzalisha megawati 24, kuongeza na kupanua mtandao wa usambazaji wa umeme katika miji ya Lindi na Mtwara na kuongeza uboreshaji wa huduma kwa wateja.

Rais wa Artumas Stephen Mason alisema umeme wa gesi ya Mnazi Bay utaongeza kwa kiasi kikubwa watumiaji wa umeme katika mikoa ya Mtwara na Lindi kutoka asiliamia 4 ya sasa.

Mason alisema licha ya umeme huo kuwa kichocheo cha maendeleo ya viwanda katika mikoa ya kusini na Tanzania nzima, pia utasaidia kuongeza ajira.

Balozi wa Uholanzi nchini, Karel van Kesteren, alitoa hundi ya Sh 22.5 bilioni zitakazotumika kusambaza umeme katika maeneo ya vijiji vya mikoa ya Mtwara na Lindi.

Gesi ya Mnazi Bay iligunduliwa mwaka 1982 na makampuni ya Agip na Amoco na tangu miaka hiyo hakukuwa na jitihada zozote za uchimbaji wa nishati hiyo hadi miaka ya karibuni.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.