Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Magari yaliyorundikana Bandarini yapigwa mnada
Magari yaliyorundikana Bandarini yapigwa mnada
By Habari Tanzania | Published  06/5/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Magari zaidi ya 2,400 yaliyokuwa yamerundikana katika Bandari ya Dar es Salaam kwa muda mrefu, yameanza kupigwa mnada.

Baadhi ya magari hayo yamekuwepo bandarini hapo tangu mwaka 1999.
Upigaji mnada wa magari hayo ni hatua ya utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Maua Daftari.

Dk. Daftari alitoa agizo hilo Mei 21, mwaka huu baada ya kutembelea ghafla Bandari ya Dar es Salaam na kukuta magari mengi yakiwa yamejazana bila wahusika kuyachukua kwa muda mrefu.

Kufuatia hali hiyo, Dk. Daftari aliwaagiza viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA) na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuhakikisha kwamba magari hayo yanaondolewa katika kipindi cha wiki mbili.

Akizugumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Meneja wa Bandari, Bw. Rugaihuruza Jason, alisema katika kuhakikisha kwamba agizo la Naibu Waziri linatekelezwa, THA imeanzisha yadi mpya kwa ajili ya kuweka magari yote yanayopigwa mnada.

Alisema yadi hiyo ipo geti namba mbili na kwamba inahifadhi magari 212 tayari kwa kupigwa mnada.

Bw. Jason alisema magari yaliyopo katika yadi ni ya wamiliki wa ndani na wa nje ambao wamekwepa kuyachukua kwa muda mrefu hali inayofanya bandari kuonekana kama dampo.

Alisema TRA kupitia kitengo chake cha Ushuru na Forodha, ilianza rasmi kuyapiga mnada magari hayo Juni Mosi, mwaka huu.

’’Zoezi hilo linaendelea hadi hapo yatakapomalizika kwani itasaidia kupunguza idadi ya magari yaliyokuwa yanafanya bandari kuonekana dampo’’ alisema Bw. Rugaihuruza.

Kuhusu magari yaliyotakiwa kusafirishwa nje ya Tanzania, alisema Kamishna wa Ushuru na Forodha, Bw. George Lauwo, ameziandikia barua Balozi za nchi husika kuzitaka kuyachukua magari yao yaliyopo katika bandari hiyo.

Alisema Balozi hizo ni zile zinazopitisha magari yao katika Bandari ya Dar es Salaam.

Alizitaja nchi hizo kuwa ni Burundi, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC), Uganda, Rwanda na Zambia.

Source Nipashe


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.