Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  CCM, wanasheria wampongeza Mtikila
CCM, wanasheria wampongeza Mtikila
By Habari Tanzania | Published  11/19/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Happiness Katabazi

BAADHI ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wanasheria wa serikali wamempongeza Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila na wenzake, kwa uamuzi wao wa kufungua kesi nzito ya kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuhoji madaraka makubwa ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Sambamba na pongezi, pia wamewataka Watanzania kuweka pembeni itikadi zao za kichama na badala yake wamuunge mkono Mchungaji Mtikila katika kesi zote za kikatiba anazofungua kwa masilahi ya Watanzania. Wamemtaka kiongozi huyo kutokata tamaa katika harakati za ukombozi.

Mchungaji Mtikila na wenzake wawili ambao ni wajumbe wa bodi ya udhamini wa DP, Douglas Salu na Anna Nkumbwa, wameiomba Mahakama Kuu ifute kifungu cha 90(1) (C) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, wakidai kwamba kinapingana na Ibara ya 13 (1), 26 (2) na 27 (1&2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa mujibu wa hati ya madai, kifungu cha 90 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, kinakinzana na Katiba, kwa kuwa kinampa DPP kutoendeleza mashauri ya jinai yanayofunguliwa na mtu yeyote.

Pia, kwa kutumia kipengele hicho, wanasema, DPP anaweza kukitumia vibaya kumlinda mtu yeyote anayekabiliwa na kesi ya jinai. Wanaeleza kwamba kifungu hicho kinampa madaraka DDP ya kuondoa shitaka la jinai mahakamni wakati wowote na bila kutoa sababu.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti na kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini, baadhi ya wanasheria wa serikali walisema wanampongeza Mtikila kwa kufungua kesi hiyo, na kumtaja kuwa ni Mtanzania ambaye anaithamini na kuilinda katiba ya nchi, licha ya baadhi ya wananchi na vigogo wa nchi kumpuuza kwa mambo ambayo amekuwa akifanya au kuzungumza.

Walisema tatizo la wananchi na viongozi wa siasa hapa nchini ni waoga na ni wataalamu wa kuzungumza mambo chinichini na humpuuza raia anayejitoa kutetea masilahi ya nchi.

“Sikufichi, si sisi wanasheria wala majaji, mahakimu wala mawakili wa kujitegemea, kifungu hicho kinatukera kwa sababu kinapingana na Katiba…ila ndiyo hivyo, sisi tupo serikalini hatuwezi kufungua kesi dhidi ya kifungu hiki na tulikuwa tunaishia kunung’unika...ila Mungu amesikia kilio chetu na hatimaye Mtikila na wenzake wamejitoa mhanga na kufungua kesi.

“Nawapongeza sana kwa uamuzi wao makini, na ninaamini Mahakama itatenda haki kuhusu kifungu hiki. Ninawashauri wanasiasa wengine nao waige mfano wa Mtikila, kwa kuwa amekuwa akifungua kesi zenye masilahi kwa Watanzania wote na kushinda, ikiwamo kesi ya mgombea binafsi.

“Lakini cha kusikitisha, Watanzania wenyewe hawamuungi mkono kwa ufinyu wao wa mawazo, na badala yake wamekuwa wakiwaunga mkono viongozi wala rushwa na wanaowadanganya kwa ahadi tamu ambazo hazitekelezeki kila kukicha,” alisema wakili mmoja mwandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Nao baadhi ya viongozi wa CCM ambao nao walikataa kutajwa majina yao, walimpongeza Mtikila kwa kufungua kesi hiyo nzito ya kikatiba, wakisema kuna Watanzania wasiotaka kuthamini mchango wa Mtikila kwa taifa hili.

“Ndiyo, tunatofautiana naye kwa itikadi ya vyama, lakini ni ukweli ulio wazi Mtikila amekuwa mstari wa mbele kutanguliza masilahi ya Watanzania…kafungua kesi ya kutaka DDP apunguziwe nguvu…nabii hakubaliki kwao, ila naomba Watanzania bila kujali itikadi tumuunge mkono kwa hili,” alisema mbunge mmoja wa CCM kutoka Kanda ya Ziwa.

Walisema tatizo la nchi hii ni kwamba mambo yake mengi huenda mrama kutokana na baadhi ya viongozi wa serikali ya CCM kuwabagua na kutowashirikisha viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani, wakati ndani ya vyama vya upinzani kukiwa na viongozi na wanachama wenye mawazo mazuri ambayo endapo serikali ingeyachukua na kuyafanyia kazi, nchi ingepiga hatua kimaendeleo.

Walisema serikali na chama wamekuwa wakiwachukulia wapinzani kuwa ni wasiokuwa na msaada, lakini wapinzani hao wakirejea CCM wanaonekana wana akili timamu na wanapewa uongozi, kitu kinachoupaka matope uongozi wa nchi kwa kuwa uongozi huo huo ndio uliridhia kuwapo kwa vyama vingi.

‘Mimi ni CCM na Mtikila ni DP, lakini nampongeza kwa kuwa uamuzi wake wa kufungua kesi hiyo ni mzuri na ni wa kishujaa, hasa ukizingatia chama chake hakina ruzuku lakini ameweza kufungua kesi na kuweka wanasheria. Chama tawala kina ruzuku kubwa na wasomi lakini wameshindwa kufanya alilofanya Mtikila,” alisema Leonard Mutabuzi ambaye ni mchumi.

Mapema mwaka huu, Mtikila aliibuka mshindi katika kesi ya kikatiba ya kutaka kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi, kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi udiwani.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.