Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Waziri alaumu utegemezi kukwaza wazo maendeleo Afrika
Waziri alaumu utegemezi kukwaza wazo maendeleo Afrika
By Habari Tanzania | Published  11/18/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Alphan Mlacha

WAZIRI wa Viwanda Biashara na Masoko, Bazil Mramba, amesema utegemezi wa nchi zinazoendelea umechangia kwa kiasi kikubwa kwa nchi za Afrika kukosa maendeleo na kuwa na idadi kubwa ya watu wasio na ajira.

Waziri huyo alisema hayo jana jijini Dar es Salaam katika warsha ya siku mbili iliyowahusisha wataalamu mbalimbali wa uchumi na fedha kutoka Ulaya, Asia, Brazili na baadhi ya nchi za Afrika.

Alisema utegemezi uliopo ni wa wataalamu wa nyanja za kilimo na biashara, pamoja utegemezi wa fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli mbambali katika nchi zinazoendelea.

Alisema nchi za Afrika zinaweza kujikwamua kiuchumi kwa kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara na kutafuta masoko ndani ya Afrika kabla ya kufikiria masoko ya nje ya bara hilo.

Alisema mfano mzuri ni soko la Afrika Mashariki ambalo kwa sasa lina watu zaidi yamilioni 90 wanaoweza kuwa wateja wazuri wa bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizo.

Alifahamisha kuwa ili kukuza soko hilo, ipo haja ya kuboresha miundombinu, kwa ajili ya kuwezesha wanunuzi kufika kwenye maeneo ya uzalishaji kwa urahisi.

Alitoa mfano wa zao la korosho kuwa lina soko kubwa duniani, lakini uzalishaji wake unahitaji kuboreshwa ili kufikia viwango vya soko la kimataifa na kuweza kuhimili ushindani.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.