Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Games Stores kuwekeza Sh130bn Tanzania
Games Stores kuwekeza Sh130bn Tanzania
By Habari Tanzania | Published  11/18/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI Game Stores kutoka Afrika Kusini, inatarajia kuwekeza nchini dola za Marekani 129.6 milioni (zaidi ya Sh130bn) katika sekta ya biashara katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Uwekezaji huo pamoja na mambo mengine utahusu uhifadhi wa bidhaa za viwandani zinazozalishwa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Game Stores, Fanus Nothnagel, alisema jijini Dares Salaam jana kwamba, uwekezaji huo kwa Bohari ya Dar es Salaam utazalisha ajira 110.

Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba, kati ya ajira hizo 50 zitakuwa za kudumu, 60 za muda maalumu ambazo zitakuwa katika vitengo vya fedha, ulinzi na usafi. Nothnagel alitaja nafasi nyingine za ajira kwamba zitahusu ufundi na mambo ya ushuru.

Alisema gharama za kuhifadhi bidhaa katika bohari hizo zitakuwa za kawaida ambazo zimelenga kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Game Stores imekwishawekeza katika bohari 69 katika nchi nane za bara hili.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.