Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kibali cha kutumia bendera chatolewa
Kibali cha kutumia bendera chatolewa
By Habari Tanzania | Published  11/15/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imetoa kibali cha kutumia nembo ya Taifa kama vile bendera ya Taifa kwenye matangazo ya shughuli pamoja na bidhaa za kibiashara, katika sherehe za kuadhimisha miaka 45 ya uhuru wa Tanganyika.

Taarifa hiyo iliyotolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Joseph Mungai, na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, inaeleza kibali hicho ni kuanzia Novemba 14 hadi Desemba 31, 2006.

“Matumizi ya nembo ya taifa yatakuwa kwa ajili ya matangazo ya shughuli mbalimbali pamoja na bidhaa za kibiashara zitakazotolewa kwa ajili ya sherehe za kuadhimisha miaka 45 ya uhuru,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kibali hicho kimetolewa kulingana na kifungu cha 6 (2) ya nembo ya taifa ya mwaka 2002, chenye kumpa mamlaka Waziri wa Mambo ya Ndani kufanya hivyo.

“Kwa mantiki hiyo, kibali hiki cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kimetolewa kwa taasisi mbalimbali na wafanyabiashara kwa dhamira ya kuwashirikisha kikamilifu katika maadhimisho hayo ya kitaifa.”

Tanganyika husherehekea uhuru wake kila Desemba 9 na mwaka huu inasherehea ikiwa ni mwaka wa 45 tangu ilipopata uhuru huo kutoka kwa Waingereza Desemba 9, 1961.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.