Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Mzee Mwanakijiji  »  Rambirambi au Unafiki?
Rambirambi au Unafiki?
By Mzee Mwanakijiji | Published  11/16/2006 | Mzee Mwanakijiji | Rating:
Je ilikuwa ni ajali?
"Ajali haina kinga" waswahili walisema, kale kadaladala kugonga gari la RC yawezekana kuwa ajali (ingeweza kuwa gari la mtu yeyote kwani hiyo ni mashine tu), lakini kitendo cha mtu kuamua kutoka ndani ya gari lake, kujibizana na dereva, kumfuata hadi kwenye gari lake, kuweka kidole kwenye trigger, kulenga mahali pa kichwa na kufyatua huwezi kuita ajali, unless neno "ajali" limepoteza maana yake!!

Je aliua kwa kukusudia?
Jibu langu ni ndiyo. Hakuna mtu anayenyosha bastola iliyo na risasi, na kuweka kidole kwenye trigger huku ameielekeza kwa mtu/watu na baadaye kufyatua, mtu/watu wakafa halafu huyo mtu aseme hakukusudia kuua!! Kama lengo lake ilikuwa ni kumtishia huyo kijana, angefanya kama wanavyofanya mapolisi au hata watu wengine kabla ya kuamua kumlenga mtu kujitetea. Wanafyatua risasi hewani kutishia!!! Unapozidiwa nguvu hapo ndipo unapoua ukitetea maisha yako, and that is a defence.

Je ni mauaji ya kujitetea maisha?
Hilo lingekuwa na ukweli endapo tu, yule kijana angetajwa mahali popote kuwa alibeba silaha (ya aina yoyote) na kumtishia Bw. Mkuu wa Mkoa. Hadi hivi sasa hakuna ushahidi wowote kuwa Hassan alifanya hivyo. Kinachojulikana alipigwa risasi (iwe moja, mbili, au kumi) akiwa ameketi kwenye kiti cha gari huku amefunga vioo!

Je Bunduki inahitajika kuonesha nia ya kosa (mens rea)
La hasha, mazingira peke yake yanatosha kuonesha kama mtu alikusudia kutenda tendo ovu (actus reus) au la. Mtu akikutwa juu ya paa la nyumba ya mtu mwingine huku akiwa ameshikilia gudulia la petroli akimimina, na baadaye kushika kiberiti na kuwasha nyumba hiyo na baadaye akakutwa amesimama pembeni anaangalia huku nyumba inaungua, mkononi amebakia na njiti zilizoungua, na ana harufu ya mafuta na mashahidi wapo waliomuona akifanya hivyo, na ikathibitika kuwa ndani ya nyumba kulikuwa na mtoto wa miaka 4 aliyeuawa kwa moto, polisi hawahitaji guduria la mafuta lililotumika kumwaga mafuta!!!

Je kitendo cha viongozi kwenda kutoa rambirambi ni kuokoa vurugu?
Kwa nje kitendo hicho kinapongezwa, ni cha kibinadamu na ni cha kiungwana. Hata hivyo, ukichunguza kwa karibu utaona kuwa ndani ya kitendo hicho kumejaa unafiki, uzandiki, na wa hali ya juu. Lengo lake ni moja tu nalo kumuonesha mtuhumiwa kuwa anajutia tendo lake (kitu ambacho hakibadilishi uzito au ubaya wa tendo hilo) na kujaribu kwa namna fulani kumuombea msamaha kwa wafiwa. Kitendo cha viongozi kutoa ahadi za kuisaidia familia n.k kina lengo moja tu nalo ni kuwanyamazisha wanafamilia (siyo kuzuia vurugu). Je watu waliokuwa wanalia mwanzoni kuwa famiilia imempoteza mtu pekee ambaye ndiye alikuwa anawasaidia kwa kila inahitaji nini zaidi ya mtu kuwapa uhakika wa chakula na malazi ya hapo baadaye?

Je ni watu wangapi ambao wanafiwa na baba zao, jamaa zao wanaosadia familia zao lakini huo RAis, makamu, meya, mawaziri, n.k wakijipanga msururu kuahidi misaada?

Ukweli ni kuwa, viongozi hawa wote wanafanya wanayofanya si kwa sababu wana uchungu kuwa Mbonde ameuwa kinyama, siyo kwa sababu familia inahitaji msaada sana, siyo kwa sababu hakuna mtu anayeweza kuwasaidia tena.. La hasha!! Viongozi hawa wanafanya wanachofanya kwa sababu anayetuhumiwa kuua ni NANI.

UKWELI NI HUU
Kama muuaji wa Hassan angekuwa Mmachinga fulani, jambazi fulani n.k unadhani viongozi hawa wangepanga foleni kwenda huko Kawe? Je alipouwa yule mwandishi wa habari wa The East African, viongozi wangapi wangazi za juu walienda kutoa pole kule na kuahidi kuisadia familia yake? Sitashangaa kuna viongozi walioenda kutoa pole, sitashangaa kuna mawaziri walioenda kutoa rambirambi kule, ila WANGAPI KATI YA HAO WALIKWENDA WAKIFUATANA NA WAANDISHI WA HABARI NA WAPIGA PICHA?

Kama hamuyaoni mazingaombwe, basi inabidi mkalie ndimu!!!

M. M. Mwanakijiji

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Related Articles
Comments
  • Comment #1 (Posted by Ndela Nzali Hingi)
    Rating
    Mzee mwenzangu Mwanakijiji.
    Hii makala yako ni saaafi sana, yaani nimeipenda. Ninacho omba uiweke chumvi kidogoo! Halafu uigeuze hoja nzito na kuisoma katika Radio yako ili na masikio nayo yafaidi
    Siasa za Tanzania zinataka
    " Nguvu Ya Hoja na Hoja Ya Nguvu kwa pamoja"
    Wametufanya Mabwege kwa muda mrefu kamwe wasitufanye mabwege siku zote.
    Mzee mwenzangu
    " Stick With Your Gun"
     
  • Comment #2 (Posted by Eng. Rwechu.)
    Rating
    Hiki ni kiini macho, ni siasa tupu kwani viongozi wote hao wanalinda na kukinga chama. sio hilo tu bali ni maandalizi ya kufuta kesi bila kelele.
    Je, ni kweli bwana Mkubwa yupo rumande?
     
  • Comment #3 (Posted by McFallan)
    Rating
    Mwanakijiji,
    Kwa maoni yangu nafikiri ni vema viongozi wakazidi kwenda kuwafariji pamoja na kwamba hii inaweza kutafasiriwa kwa namna mbalimbali.Kutokana na mkuu wa mkoa kuhusika katika mauaji haya; kama viongozi wetu wasingeenda kuwafariji ingeweza kuonekana pia kama ishara ya kutokuwajibika na kutokuguswa na makosa yafanywayo na viongozi wa serikali. Nafikiri ni vema wakazidi kwenda kuwafariji. Ila mimi kinachonisumbua katika hilo ni kwamba kuishia kutoa rambi rambi hakutoshi. Kwa vile aliyefanya kosa hilo ni mtu aliyekuwa na dhamana kubwa tu kitaifa, basi uangaliwe utaratibu wa kuhakikisha watoto wa Marehemu wanahudumiwa na serikali. Nafahamu pesa za serikali ni kodi yetu, lakini sio mbaya sehemu hii ya kodi ikatumika kuwahudumia watoto hawa. Au upande mwingine, japo hili linaweza kuhitaji tafasiri ya kisheria, mafao ya huyu mkuu wa mkoa yangetumika pia kwa hili.
    Tuzidi kuwatia moyo familia hii. Maana hili gari la mkubwa linathamani kuliko maisha ya mlalahoi.
     
  • Comment #4 (Posted by ngorunde)
    Rating
    Bravo Mwana kijiji
     
  • Comment #5 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Power to the people!!!
     
  • Comment #6 (Posted by an unknown user)
    Rating
    SAFI SANA McFALLAN. UNAJUA KILA BINADAMU ANA HULKA YAKE. WAPO AMBAO UKIFANYA HILI WANAHOJI KWA NINI UNAFANAYA; USIPOLIFANYA WANAHOJI KWA NINI HAUJALIFANYA. KWA HIYO NI VIZURI PALE WATU WANAPOFANYA LILILO JEMA KAMA KUWAFARIJI HAO WALIOMPOTEZA NDUGU YAO, WAKAACHWA KUFANYA HIVYO. KWANI KUNA UBAYA GANI?
    KUHUSU MWANDISHI WA THE EAST AFRICAN, HILO SWALI LIPELEKWE KWA WAANDISHI WA HABARI WANAO-COVER HAYO MATUKIO; MAANA INAONYESHA KUNAMATUKIO AMBAYO WANKUWA NA INTEREST ZAIDI KUYARIPOTI HATUA KWA HATUA, NANI KAFANYA NINI WAKATI MATUKIO MENGINE WANAISHIA HATA HAYAPATI COVERAGE YA KUTOSHA. JE, NI KWELI MSIBA WA MWANDISHI WA THE EAST AFRICAN HAUKUHUDHURIWA NA VIONGOZI WA SERIKALI. NA JE, KILA VIONGOZI WA SERIKALI WATAKAPOKUWA WANAHUDHURIA MISIBA NA MATUKIO MBALIMBALI YA KIJAMII, HABARI ZAO ZIWE ZINATOLEWA KWA UZITO SAWA KATIKA MAGAZETI NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI? JE, NI VONGOZI WANAOWAOMBA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA MATUKIO HAYO? JE, WAANDISHI WA HABARI WANAANDIKA KWA AJILI YA KUIHABARISHA NA KUIELIMISHA JAMII AMA NI KWA AJILI YA KUUZA HUDUMA YAO?
     
  • Comment #7 (Posted by Amon)
    Rating
    Ukweli nimependa jinsi ulivyo zungumzia na kujadili hoja hii, na ni kweli umenifungua macho maana nilikuwa sioni kama ninavyoliona baada ya kusoma article yako. Keep up the good job Mwana kijiji.
     
  • Comment #8 (Posted by Hemedi Begge)
    Rating
    Kaka muhariri makala yako inania njema
    sana ila inahitaji mtu mwenye fikra zilizo tulia kujuwa nini hasa unachokusudia.Kwa ufupi tu familia ya marehemu kwenda kupewa pole na viongozi mbali mbali haileti maana kuwa ni unafiki au kuwapoza wafiwa au kunyamazisha kelel siyo kweli.Viongozi kwenda kutoa pole sababu kuu nikuwa aliye tenda tendo lile ni kiongozi wa kitaifa hivyo basi akiwa ni mkuu wa mkoa wa Tabora unapswa ujuwe nilazima viongozi wawe mstari wa mbele kuiwakilisha serekali kwa kutoa pole kama wafanyavyo kunapo tokea ajali kubwa yoyote kijamii huwa wanatoa pole za jumla kwanjia ya matangazo.
     
  • Comment #9 (Posted by sam)
    Rating
    keep it up
     
Submit Comment


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Is Tanzania a safe place to invest?
  4. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Linda Garner
  4. Nthelezi Nesaa
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.