Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mkulima aua mfugaji
Mkulima aua mfugaji
By Habari Tanzania | Published  11/14/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Charles Mwakipesile, Mbeya

MKULIMA wa Kijiji cha Utengule Wilaya ya Mbarali, Bw. Zakaria Mfumbulwa, ameuawa kikatili na mfugaji wa kijiji hicho katika mapigano yaliyotokea jana wakati alipokuwa akijaribu kuzuia mifugo kutoingia katika shamba lake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mmoja wa wajumbe wa Kamati maalumu ya kuwaondoa wafugaji wanaovamia mashamba wilayani humo baada ya kuondolewa katika bonde la ardhi oevu la Ihefu, Bw. Kenneth Ndingo, alisema ugomvi huo ulitokea jana.

Alisema kuwa mfugaji huyo ambaye hadi sasa hajapatikana kutokana na madai kuwa alikuwa kibarua aliyekuwa anafanya kazi ya kuchunga ng'ombe hao , aliipeleka mifugo hiyo katika shamba la Bw. Mfumbulwa.

Bw. Ndingo, alisema kuwa marehemu kuona hali hiyo alizuia kitendo hicho kisifanyike , ndipo ugomvi ulipoanza kwa kupigana kwa kutumia fimbo hali iliyomfanya mfugaji huyo kuchomoa kisu kiunoni na kumchoma mkulima huyo.

Alisema mfugaji huyo alifanya mauaji hayo 'kijanja' mkubwa kwani wakiwa wamekumbatiana alimchoma kisu na kutokana na maumivu makali, alidondoka na kupoteza maisha.

Bw. Ndingo alisema kwa kuwa hapakuwa na mtu wakati wanapigana, mfugaji huyo alitumia mwanya huo kutorokana na hadi sasa hajakamatwa na polisi wanaendelea kumsaka.

Mapigano ya aina hiyo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara tangu kuanza kwa maandalizi ya msimu wa kilimo ambapo wafugaji waliondolewa katika hifadhi hiyo, wamekuwa wakivamia mashamba kwa ajili ya kulisha mifugo yao kwa nguvu.

Mara kwa mara vinapofanyika vitendo hivyo, wakulima wamekuwa wakija juu hali inayowafanya wafugaji kutumia silaha zikiwemo fimbo na visu kuwapiga wakulima kwa madai kwamba hawana sehemu za kwenda.

Hata sasa wafugaji wengi wameondoka wilayani humo kwenda katika mikoa ya Lindi na Pwani walikopangiwa na Serikali ambapo wanaoruhusiwa kubaki ni wale wenye mifugo michache.

Serikali wilayani Mbarali inaendesha kampeni kabambe kuhakikisha wafugaji wanaondolewa wilayani humo na wanaokamatwa na mifugo yao wakiwa wameificha, wamekuwa wakitozwa faini.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.