Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Upimaji ukimwi Tanzania wabadilishwa
Upimaji ukimwi Tanzania wabadilishwa
By Habari Tanzania | Published  11/14/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imefanya mabadiliko ya mfumo wa kitaifa wa upimaji wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kuruhusu kipimo kipya cha haraka.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hilda Gondwe, kwa vyombo vya habari inasema kuwa kipimo hicho kinajulikana kitaalamu kama "National HIV Rapid Testing Algorithm."

Kipimo hicho kimeruhusiwa baada ya wizara hiyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Kishirikishi cha Sayansi ya Afya Muhimbili, kufanya tathmini ili kuainisha vitendanishi vinavyofaa zaidi katika mazingira ya kitanzania na vigezo vilivyozingatiwa katika tathmini hiyo ni ubora wa kiufundi, bei, mahitaji ya uhifadhi, na muda wa kuweza kutumika.

Akifafanua kipimo hicho, Gondwe alisema katika utaratibu mpya, upimaji wa virusi vya ukimwi utatumia vitendanishi vinavyotoa majibu kwa muda mfupi na kuyahakiki kwa kutumia vipimo vitatu tofauti.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kipimo cha kwanza kinaitwa SD Bioline na endapo majibu ya kipimo hicho yataonyesha hakuna maambukuzi ya virusi vya ukimwi, majibu yatatolewa kwa muhusika na kama kipimo kitaonyesha kuwepo kwa maambukizi, damu itapimwa tena kwa kutumia kipimo cha pili aina ya Determine kuthibitisha kuwepo kwa maambukizi.

"Iwapo vipimo vyote viwili yaani SD Bioline na Determine vitaonyesha kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi, mhusika atapewa majibu kuwa anayo maambukizi lakini endapo majibu ya SD Bioline na Determine yatakuwa tofauti, kipimo cha tatu aina ya Unigold kitatumika kuamua kama kuna maambukizi ya virusi vya ukimwi au la," inasema taarifa hiyo.

Gondwe alisema mfumo wa sasa wa upimaji kwa kutumia Capillus ikifuatiwa na Determine, utaendelea kwa muda wakati wizara inaendelea na maandalizi ya mipango ya kuingiza nchini vitendanishi vya SD Bioline na Unigold na pia kuwapa watoa huduma mafunzo kuhusu matumizi ya vipimo hivyo.

Awali, upimaji wa virusi vya ukimwi umekuwa ukifanyika kwa kutumia mifumo mbalimbali ya kimaabara na mifumo hiyo ni pamoja na ile inayotumia vitendanishi vya Elisa (Enzyme linked immunosorbant Assay) na mingine inatumia vitendanishi vinavyotoa majibu kwa muda mfupi(Rapid HIV Test).

Mfumo wa vitendanishi vya muda mfupi, ulioanza kutumika nchini mwaka 1996 umeonekana kuwa kikwazo katika juhudi za taifa za kupanua wigo wa upimaji wa maambukizi ya virusi vya ukimwi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.