Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kesi ya kumpinga Askofu kuanza leo
Kesi ya kumpinga Askofu kuanza leo
By Habari Tanzania | Published  11/13/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Gasper Andrew, Singida

KESI kupiga kusimikwa mchungaji John Lupaa kuwa askofu wa Kanisa Angelikana, Doyasisi ya Bonde la Ufa, leo inatarajiwa kuanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Singida.

Oktoba 20, mwaka huu, muumini wa kania hilo, William Sunja kwa niaba ya wenzake, alifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini hapa kuiomba isimamishe kwa muda usimikwaji wa Askofu mpya Lupaa hadi hapo kesi ya msingi ya kupinga uteuzi wake, itakapotolewa uamuzi na mahakama.

Kesi hiyo ya msingi imefunguliwa na Sunja na wenzake, dhidi ya wadhamini wa Kanisa Angelikani Tanzania, Dayosisi ya Bonde la ufa, Askofu Mstaafu Alpha Mohamed, Askofu Mkuu wa Kanisa la Angilikan Tanzania, Donald Mtetemela na Askofu Mteule wa Dayosisi hiyo Mchungaji Lupaa.

Sunja na wenzake wanapinga uteuzi wa Mchungaji John Lupaa kuwa askofu mpya wa kanisa hilo kwa madai kwamba uteuzi wake, ulikiuka Katiba ya kanisa hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mwishomi mwa wiki iliyopita, Hakimu wa Mkazi wa Mahakama hiyo, Joseph Chaba, alisema oktoba 20 mwaka huu, ilisimamisha kwa muda kusimikwa kuwa Askofu Mteule Lupaa hadi hapo kesi iliyofunguliwa kupinga uteuzi wake,itakapotolewa uamuzi na mahakama.

Alisema hata hivyo, karani wa mahakama hiyo aliyetumwa Manyoni kuwasainisha zuio hilo viongozi wa kanisa hilo, inadaiwa viongozi hao hawakuafikiana na zuio hilo, badala yake waliendelea kumsimika Lupaa kuwa Askofu mpya wa Dayosisi hiyo.

Ilidaiwa kwamba tamko lililotolewa na Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo juni 10 mwaka huu, lilisema majina ya Askofu Msaidizi David Mattonya na mchungaji John Lupaa yaondolewe kwenye orodha na taratibu za kutafuta waombaji wapya urudiwe.

Tamko hilo lililotolewa na maaskofu wapatao 16 wa kanisa hilo waliokuwa chini ya Askofu Mkuu Donard Mtetemela lakini halikufanyiwa kazi.

Pamoja na pingamizi hilo, mchungaji Lupaa alisimikwa rasmi oktoba 22 mwaka huu, ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida, Florence Horombe, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, Parseko Kone.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.