Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Polisi wasaka walioeneza SMS Mchungaji Rwakatare kakamatwa
Polisi wasaka walioeneza SMS Mchungaji Rwakatare kakamatwa
By Habari Tanzania | Published  11/12/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Beatrice Moses

JESHI la Polisi linakisaka kikundi cha watu kinachodaiwa kuzusha na kueneza ujumbe (sms) wa simu za mkononi unaodai Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Mikocheni B, Jijini Dar es Salaam, Dkt. Getrude Rwakatare amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuingiza na kuuza madawa ya kulevya.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi Kanda maalum Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana alisema Jijini jana wanakisaka kikundi hicho na watawafikisha kortini watakaobainika kuhusika na usambazaji ujumbe huo unaolenga kupotosha jamii.

" Faili limefunguliwa hapa. Tunachofanya ni kukisaka kikundi hicho kwa kuanzisha na kueneza ujumbe huo kikitumia watu mbalimbali kwamba Polisi wamemkata Mchungaji Rwakatare kwa kuhusika na madawa ya kulevya. Nafikiri lengo lao likiwa ni kumchafulia jina. Tunawasaka ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria," alisema.

Hadi sasa kuna taarifa za kuaminika kuwa tayari mmoja kati ya wanaotuhumiwa amekamatwa akidaiwa kutuma sms 400 za aina hiyo ambayo gazeti hili lilitumiwa Novemba 4 mwaka huu. Hata hivyo Kamanda Tibaigana hakueleza zaidi wanavyolifuatilia.

Akizungumza jana na gazeti hili nyumbani kwake Mikocheni, Mchungaji Dkt. Rwakatare alieleza kuhuzunishwa kwake na suala hilo ambalo alisema limelenga kumchafulia jina lake kwa waumini na jamii kwa ujumla na kumkatisha tamaa kufanya kazi ya Mungu.


Alisema alishangaa kupokea ujumbe kwenye simu yake uliodai amekamatwa na Polisi Jumamosi wiki iliyopita kwa kukutwa na madawa ya kulevya na dhamana imefungwa, jambo lililomshtua kwani siku hiyo alikuwa nyumbani kwake amepumzika baada ya kutoka kwenye mahafali ya shule ya sekondari ya St. Marys.

Alisema baada ya kusoma simu hizo, alikuta akipigiwa simu na watu wanaomfahamu wakiwemo waumini wake wengi wakionekana kustaajabu kwa kumpata kwenye simu yake na kuzungumza naye kwani walipata ujumbe kuwa amekamatwa hivyo kumhoji ilikuwaje.

"Sijui hata nieleze nini maana nimeumia sana. Uzushi huu ni mbaya mno. Nafikiri wanafanya ili kuniporomosha kiroho lakini mimi namtumainia Mungu. Naamini hawezi kuniacha niaibike kamwe.

Ukweli ni kwamba siwezi kujihusisha na biashara chafu kama hiyo ambayo inamaliza maisha ya vijana na kurudisha nyuma maendeleo ya kanisa na taifa kwa ujumla," alisema kwa uchungu.

Alisema anadhani waliofanya hivyo wanachuki kutokana na mafanikio ambayo Mungu amemjalia katika kuhubiri injili na kuendelea sekta ya elimu nchini kwa miaka mingi sasa.

Hata hivyo, alisema pamoja na fitna zote hizo, hawezi kuacha kuitumikia jamii na Mungu kutokana na uzushi huo bali ataendelea kuhubiri na kushiriki katika maendeleo ya taifa kwa ujumla.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.