Na Elizabeth Mjatta
MAAFISA watano wa polisi, akiwemo Inspekta Jenerali Saidi Mwema, jana wameapishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa wajumbe wa tume ya utumishi ya polisi na magereza.
Wengine walioapishwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DPP) Robert Manumba, Mkurugenzi wa Utawala, Levinus Mbuya, Kamishina wa Utawala na Fedha, Clodwig Mtweve na Shaban Mlubi.
Wajumbe hao waliapa mbele ya Jaji Thomas Mihayo, ambaye aliwataka kufanya kazi kwa bidii kwani kazi hiyo ni nyeti na muhimu katika kujenga jeshi imara na lenye heshima kwa jamii.
Alisema yeye binafsi ameridhishwa na uamuzi wa jeshi hilo kutoa namba za simu za maafisa wa ngazi za juu kwa umma ikiwa njia mojawapo ya kupambana na uhalifu hapa nchini.
“Sio mimi tu, hata wananchi wengi wamekuwa na imani kwa jeshi lao kutokana na viongozi kuwa wawazi kwa umma hivyo hali hii inailirudishia jeshi hilo heshima,” alisema Jaji Mihayo.
Wajumbe hao walioapishwa watakuwa na kazi mbalimbali katika tume hiyo, ikiwamo kushughulikia masuala ya nidhamu katika jeshi, kuwapandisha vyeo askari wanaofanya vizuri katika jeshi hilo na kushughulikia masuala ya adhabu na makosa mabalimbali