Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Tume ya Mawasiliano kujenga kitega uchumi
http://www.habaritanzania.com/articles/1744/1/Tume-ya-Mawasiliano-kujenga-kitega-uchumi
By Ramadhan Semtawa
Published on 11/9/2006
 
MAMALAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeanza kujijengea uwezo wa kiuchumi baada ya kuanzisha mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba ya ghorofa 14 ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh25 bilioni.

Na Ramadhan Semtawa

MAMALAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeanza kujijengea uwezo wa kiuchumi baada ya kuanzisha mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba ya ghorofa 14 ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh25 bilioni.

Katika mradi huo ambao ujenzi wake unafanyika pembezoni mwa barabara ya Sam Nujoma, TCRA itatumia asilimia 50 ya jengo hilo.Habari kutoka TCRA zilizothibitishwa na uongozi wa mamlaka hiyo, zinasema katika mradi huo, mamlaka hiyo itakuwa katika ubia na kampuni nyingine.

Hata hivyo, chanzo hicho kimefafanua kwamba hadi sasa TCRA inaendelea kutafuta wabia watakaoshirikiana nao katika mradi huo."Ni mradi mkubwa, utakuwa wa ghorofa 14, mamlaka inatarajiwa kuchukua asilimia 50 ya jengo sehemu nyingine huenda zikapangishwa," kilifafanua chanzo hicho.Kwa mujibu wa chanzo hicho, Mhandisi Mshauri wa mradi huo ni kampuni ya Arch Plan.Jengo hilo ambalo ramani yake iko hata katika kalenda ya mwaka huu ya TCRA, litakuwa la kisasa.Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Uhusiano wa TCRA, Victor Nkya, alithibitisha kuanzishwa kwa mradi huo wa kwanza wa aina yake wa mamlaka hiyo.

Wakati huo huo, Kampuni ya Simu ya Zambia (Zambia Telecom), imekubali kulipa deni la mamilioni ya shilingi, inayodaiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kipindi cha mwaka 2002 hadi Machi 2006.Makubaliano hayo yamo katika ripoti ya mpango wa biashara ambayo Zambia Telecom imeuwakilisha kwa TTCL wiki iliyopita.Habari za kuaminika kutoka ndani ya TTCL, zinasema katika mpango huo, Zambia Telecom ambayo inadaiwa zaidi ya dola 400,000 ( zaidi ya Sh 500,000 milioni) imekubali kulipa dola 63,000 kila mwezi kuanzia mwisho wa mwezi huu.

Uamuzi wa Zambia Telecom kukubali kulipa fedha hizo umetokana na mazungumzo yaliyofanyika kati ya ujumbe wa TTCL na wa kampuni hiyo yaliyofanyika mjini Lusaka, Zambia mwezi uliopita.Katika mazungumzo hayo, Zambia Telecom iliomba muda kutoka TTCL ambao ingeweza kutoa mpango wake wa kibiashara ambao ungeonyesha kama ingelipa fedha au ifidie gharama hizo katika simu za kimataifa zinazopigwa nchini humo na wateja wa TTCL.Chanzo hicho kimebainisha kwamba, ni Zambia Telecom pekee ndiyo inayodaiwa baada ya Kampuni ya Kenya Telecom kumaliza deni lake.

Kenya Telecom ilimaliza deni hilo baada ya kukatwa fedha hizo katika simu za kimataifa zilizopigwa na wateja kutoka TTCL."Zambia Telecom imekubali kulipa dola 63,000 kila mwezi, imekwishaleta mpango wake wa biashara na itaanza kulipa mwisho wa mwezi Novemba," kilifafanua chanzo hicho.TTCL inadai jumla ya Sh113 bilioni ambazo ni deni la ndani na nje ya nchi na hivi karibuni ilianzisha operesheni ya kuhakikisha fedha zote zinapatikana.Hivi karibuni Meneja Mawasiliano wa TTCL, Issa Semtawa, alilithibitishia gazeti hili kufanyika kwa mazungumzo kati ya ujumbe wa kampuni hiyo na wa Zambia