Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  MAGUFULI ATEMA CHECHE NA KUSEMA:Viwanja visivyoendelezwa Mbezi Beach vyachukuliwa
MAGUFULI ATEMA CHECHE NA KUSEMA:Viwanja visivyoendelezwa Mbezi Beach vyachukuliwa
By Habari Tanzania | Published  05/31/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Viwanja visivyoendelezwa Mbezi Beach vyachukuliwa
 
Zaidi ya viwanja 10,000 vyarudishwa serikalini
Wamo pia walioshindwa kulipa mradi wa viwanja Dar
Lengo ni kuondokana na ‘migogoro ya ardhi’ isiyo lazima
 
SERIKALI imewanyang’anya kuanzia leo watu na taasisi zilizopewa viwanja na kushindwa kuviendeleza katika maeneo ya Tegeta na Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
 
Zaidi ya viwanja 10,000 vinahusika katika hatua hii, iliyotajwa kuwa ni ya ‘kusafisha migogoro ya ardhi’.
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, aliwatangazia waandishi wa habari jana kuwa, pia serikali imewaagiza wananchi wasiokamilisha malipo ya viwanja walivyopewa kupitia mradi wa viwanja 20,000, wavilipie mara moja ndani ya wiki moja, kuanzia jana.
 
Magufuli, alitamka hayo alipokuwa anatoa ufafanuzi wa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali kutatua matatizo ya ardhi nchini na upangaji katika majengo yanayomilikiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
 
Alisema katika viwanja vya Tegeta na Mbezi Beach, picha za angani zilizochukuliwa zimeonyesha kuwa viwanja vingi vilivyo wazi na baada ya kufanyiwa uhakiki, kuanzia tamko la jana vyote vimenyang’anywa na kuchukuliwa na serikali.
 
Kwa mujibu wa Magufuli, viwanja hivyo vya Mbezi Beach na Tegeta, viligawiwa kwa wananchi kwenye miaka ya 1980 na 1990 na wengi ama hawakuviendeleza kabisa au wameendeleza kwa kiasi kidogo, kama kuiwekea ukuta au kujengewa vibanda.
 
Akifafanua juu ya tamko hilo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Salome Sijaona, alisema kuwa kuanzia tamko hilo kutolewa, hakuna mtu yoyote anayeruhusiwa kuviendeleza.
 
Katibu Mkuu alitoa mfano wa viwanja hivyo, ambapo alisema katika kila kitalu kuna wastani wa viwanja kati ya 700 na 900, ambapo visivyoendelezwa vinafika idadi ya nusu yake.
 
Alitoa mfano wa kitalu kimoja alichokitaja kwa jina la ‘G’ huko Mbezi Beach, ambapo alisema kulikuwa na viwanja zaidi ya 700 na kati yake 450 vilikuwa havijaendelezwa mpaka sasa.
 
Salome alisema kuwa, Mbezi Beach kuna vitalu sita (kitalu A-F) vyenye jumla ya viwanja visivyopungua 4,200, wakati Tegeta kuna vilatu 12 (A-L). Lakini katika idadi hiyo, vitatu havitahusika katika unyang’anywaji kwa sababu maalum.
 
Waziri Magufuli alisema katika hatua hizo zinazolenga kufuta migogro ya viwanja, pia imewataka wote waliopewa viwanja kupitia mradi maalum na kuvilipia, lakini hawajakamilisha malipo, wafanye hivyo ifikapo Juni 6, mwaka huu.
 
Alisema hiyo itaondoa migogoro ya watu kuhodhi viwanja na kujihusisha na rushwa na utapeli, njama alizosema hata maofisa ardhi wamo na badala yake sasa anajenga mazingira mazuri ya kupatikana viwanja kwa wingi kwa kila anayetaka na uwezo wa kujenga.
 
Hata hivyo, alisema katika mradi wa viwanja maalum jijini Dar es Salaam , bado kuna viwanja 7,552 ambavyo havijagawiwa kwa watu, kati yake 6,183 viko wilayani Ilala, Kinondoni (685) na Temeke (684).
 
Alisema katika eneo la Kibada wilayani Temeke, upimaji unaendelea wa viwanja vipya 5,000 kwa madhumuni kama hayo.
 
Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 27 kwa ajii ya kuendeleza mradi huo nchini, ambapo Waziri Magufuli alisema utaendelezwa katika baadhi ya miji kwa viwango kama Mwanza (9,500), Morogoro (4,000).
 
Kuhusiana na kamati alizoziunda hivi karibuni katika wilaya tatu za mkoa wa Dar es Salaam chini ya wakuu wa wilaya kuchunguza migogoro ya ardhi, Waziri alisema zimeanza kutoa ripoti zake na taarifa zinaeleza wilaya ya Kinondoni ndiyo inayoongoza kwa matatizo.
 
Pia, Waziri Magufuli alisema kuwa, serikali imeamua kufanya mapitio ya kina ya wapangaji wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC), ili shirika hilo liwe na wapangaji halali.
 
Alisema asilimia 90 ya kazi imekamilika na uchambuzi unaendelea kufanyika chini ya usimamizi wa ofisi yake ambapo mafaili yote ya wapangaji wa NHC yameitishwa katika makao makuu ya wizara.
 
Kwa mujibu wa Magufuli, hivi sasa wapangaji halisi watajaza fomu na kuweka picha zao, na kuongeza: “Wakati wa kufanya hizi nyumba za ‘National Housing kuwa za kiukoo umepita.”
 
Kutoka gazeti la Uhuru
ISSN 0876-3896 NA.19323
Na Peter Orwa

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.