Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mamlaka ya DPP kuhojiwa kortini
Mamlaka ya DPP kuhojiwa kortini
By Habari Tanzania | Published  11/7/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi Wetu

KITUO Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinatarajia kufungua kesi ya kikatiba kutaka kumwondolea mamlaka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ya kufuta kesi bila sababu za msingi.

Tayari maandalizi ya ufunguaji kesi hiyo yamekwisha kufanyika na kwamba sasa yako katika hatua za mwisho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen Kijo-Bisimba, alisema lengo la kufungua kesi hiyo ni kujaribu kuziba mianya ya DPP kutumia madaraka yake vibaya kwa kufuta kesi za vigogo au watoto wao.

Mkurugenzi huyo wa LHRC, ambaye kituo chake kilishiriki kikamilifu katika kuhakikisha sheria ya takrima katika uchaguzi inafutwa, alisema kituo hicho kwa kushirikiana na wanaharakati wengine ambao hakupenda kuwataja, wanajipanga ili kuhakikisha kesi hiyo haipingwi kabla ya kufikishwa mahakamani.

Mkurugenzi huyo alisema lengo ni kuhakikisha kuwa kama DDP anafuta kesi, basi kunakuwa na sababu za msingi ambazo zinatolewa kwamba kwa nini alifuta kesi sio kufuta bila kutoa sababu.

Aliongeza kwamba DPP akifuta kesi, kisha akatoa sababu za msingi, itakuwa ni vema zaidi kwani itaondoa maswali kwa wananchi kwamba kesi fulani imefutwa kwa sababu zipi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.