Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mkuu wa Mkoa Ditopile akamatwa kwa mauaji
Mkuu wa Mkoa Ditopile akamatwa kwa mauaji
By Habari Tanzania | Published  11/6/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Muhibu Said

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ramadhan Ditopile Mzuzuri, ametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za mauaji ya raia kwa kutumia bastola yake jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka eneo la tukio zilizothibitishwa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, zinaeleza kuwa Ditopile anatuhumiwa kumuua dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), mkazi wa Kawe Mzimuni, jijini Dar es Salaam kwa kumpiga risasi kichwani.Ditopile, anatuhumiwa kumuua dereva huyo juzi saa 2.30 usiku, katika njia panda ya barabara ya Kawe na Bagamoyo, Wilaya ya Kinondoni, baada ya kuchukizwa na hatua ya gari lake kugongwa kwa nyuma na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu.Marehemu ambaye alifariki dunia papo hapo, alikuwa akiendesha gari aina Isuzu Journey, linalofanya biashara ya daladala kati ya Ubungo na Tegeta na lilikuwa likitokea Ubungo kwenda Tegeta.Gari hilo lililigonga gari aina ya Prado lililokuwa likiendeshwa na dereva wa Ditopile, Nassoro Mohamed (42), mkazi wa Kijitonyama, Dar es Salaam, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo, mkoani Pwani.

Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa baada ya gari hilo kugongwa, dereva wa Ditopile, alishuka na kwenda kukagua uharibifu uliotokana na tukio hilo. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, gari hilo lilivunjwa taa moja ya nyuma.

Walisema wakati dereva huyo akiendelea kulikagua gari hilo, Ditopile naye alishuka na kuungana na dereva wake katika ukaguzi huo.Walisema baada ya kuona uharibifu huo, Ditopile, alimfuata marehemu na kumtaka ashuke katika gari alilokuwa akiliendesha ili aende kushuhudia uharibifu uliotokea na kisha waende polisi.Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu, alimweleza Ditopile kuwa ajali hiyo ilitokea kwa bahati mbaya na kumwomba msamaha kwa tukio lililotokea.Walisema mkuu huyo wa mkoa, hakukubaliana na utetezi huo na badala yake aliendelea kumwamuru marehemu ashuke kwenye gari na kumtaka akaeleze maneno hayo polisi.

Mashuhuda hao, walisema marehemu alipoona Ditopile anazidi kutoa maneno ya ukali, aliamua kufunga kioo cha gari kuepuka kuchochea hasira za kiongozi huyo.Walisema kitendo hicho kilimuudhi Ditopile ambaye alichomoa bastola aliyokuwa nayo na kuanza kuitumia kugonga kwenye kioo cha gari la marehemu huku akimsisitiza kushuka katika gari.Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu aligoma kutii amri hiyo ya Ditopile na ndipo alipomfyatulia risasi iliyopenya kwenye kioo cha gari na kufumua kichwa cha marehemu.

Mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika eneo hilo muda mfupi baada ya tukio hilo, alishuhudia mwili wa marehemu ukiwa umeegemea kwenye kiti cha dereva huku damu na ubongo vikiwa vimetapakaa ndani ya gari alilokuwa akiliendesha.Tukio hilo lililozua hofu, lilisababisha mtafaruku mkubwa miongoni mwa watu, wakiwamo madereva na abiria waliokuwa wakisafiri katika njia hiyo, kutokana na mlio wa risasi.

Watu waliokuwa kwenye magari, walishuka na kuanza kukimbia ovyo katika sehemu mbalimbali wakidhani kuwa eneo hilo limevamiwa na majambazi.Watu pekee waliobaki katika eneo hilo, ni dereva anayedaiwa kuwa wa Ditopile na mwanamke ambaye hakuweza kufahamika mara moja ambaye anadaiwa kuwa alikuwa katika gari lililokuwa limembeba Ditopile.

Hata hivyo, wakati hayo yanajiri, hakuna mtu yeyote alimyetambua mtu aliyemfyatulia marehemu risasi isipokuwa dereva wa gari lililokuwa limembeba.Baada ya tukio hilo, mwandishi wa habari hizi, alishuhudia kondakta wa gari hilo ambaye hakuweza kufahamika mara moja, akipambana na mtu huyo wakinyang'anyana bastola inayodaiwa kutumiwa na Ditopile.Katika 'mpambano' huo, bastola hiyo ilidondoka na kondakta na mtu huyo wakaanza kugombea kuiokota.Hata hivyo, kondakta alizidiwa nguvu na mtu huyo aliiokota bastola hiyo na kutokomea nayo kusikojulikana.

Dakika chache baadaye, polisi waliobeba silaha wakiwa ndani ya magari matatu aina ya Lond Rover Defender, walifika katika eneo hilo.Akielezea tukio hilo, Kamishna Tibaigana, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku katika eneo hilo na gari lililombeba Ditopile, lilikuwa na abiria wawili; akiwamo Ditopile mwenyewe na mtu mwingine ambaye hajafahamika. Alisema wote walikuwa wakitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo."Mara baada ya ajali hiyo kutokea, magari hayo yalisimama. Dereva Nassoro Mohamed alishuka na kwenda kuangalia gari lake ili kubaini lilivyoharibika/kugongwa, aliliona limepata madhara kidogo upande wa nyuma," alisema Kamishna Tibaigana na kuongeza:

"Wakati Nassoro Mohamed akiendelea kuangalia, alishuka mheshimiwa Kapteni Ukiwaona Ramadhani Ditopile Mzuzuri ili naye aende kuona uharibifu uliotokea. Baada ya kuona uharibifu uliotokea alimtaka dereva wa Isuzu Journey, Hassan Mbonde, ashuke ili naye aone uharibifu uliotokea kisha waende polisi kutoa taarifa."Dereva wa Isuzu Journey alikataa kushuka kwenye gari lake na badala yake alifunga kioo cha dirisha la mlango wake kisha alifunga mlango na ku-lock kwa ndani.

Mheshimiwa Ditopile Mzuzuri baada ya kuona dereva amefunga mlango, alisogelea dirishani na kutoa bastola yake na kuanza kugonga dirisha kwa kutumia bastola yake, huku akimwamuru ashuke ndipo ghafla alifyatua risasi moja ambayo ilivunja kioo cha dirisha na kumjeruhi Hassan Mbonde kichwani na alifariki dunia papo hapo," alisema Tibaigana katika maelezo yake kwa waandishi wa habari.

Tibaigana, alisema baada ya tukio hilo, dereva Mohamed, aliendesha gari lake na kuondoka sehemu ya tukio akiwa na abiria wake wawili."Mtuhumiwa Ukiwaona Ramadhani Mwinshehe Ditopile Mzuzuri amekamatwa na anaendelea kuhojiwa. Pia mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili," alisema Kamanda Tibaigana.Asubuhi jana, watu walimiminika katika Kituo cha Polisi Kawe kwa ajili ya kuandikisha maelezo yao juu ya jinsi walivyoshuhudia tukio hilo.Baadhi walisimulia kuwa katika tukio hilo, Mkuu huyo wa Mkoa alipiga risasi mbili ambapo moja ilimkosa marehemu na nyingine ndiyo ilimuua papo hapo.Daladala aliyokuwa akiendesha marehemu Mbonde ilikuwa imeegeshwa katika kituo hicho cha polisi na baada ya baadhi ya watu kutoa maelezo, walitakiwa kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi.

Nyumbani kwa marehemu kulikuwa na watu wachache huku mvua ikiendelea kunyesha na wengi wao walikuwa wakijadili tukio hilo. Marehemu Mbonde ameacha watoto wadogo watatu."Hii inatakiwa Rais aunde Tume kama ilivyokuwa kwa Zombe, hivi hivi hakutakuwa na haki," alisema muombolezaji mmoja.Watu hao walishikwa na hasira na kutaka kuwavamia waandishi waliokuwa msibani hapo baada ya redio moja kutangaza kuwa marehemu alikufa katika ajali.

Habari zilizopatikana msibani hapo zilieleza kuwa marehemu Mbonde atazikwa leo saa saba mchana katika makaburi ya Kawe.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by McFallan)
    Rating
    Hii haikubaliki na sheria inapaswa ifuate mkondo wake. Inasikitisha kuona viongozi wanajichukulia hatua za kisheria mikononi na hawawajibishwi. Wapo viongozi waliowapiga watu makofi:-Na hakuna hatua yoyote ya kuwawajibisha iliyochukuliwa. Hatimae limefikia hili la kuua mtu kwa sababu ya kugonga gari. Tunamuomba Rais JK: sio kuunda tume bali kuhakikisha sheria zinafuata mkondo wake. Maana tume huundwa pale mazingira yanapokuwa yana utata. Huyu Ditopile amefanya uhalifu sawa na uhalifu wa kawaida. Taratibu ziko wazi. Anafaa 1. Kuvuliwa ukuu wa mkoa mara moja 2. Kukaa rumande pasipo kupewa dhamana (maana hii ni kesi ya mauaji) mpaka pale hatima ya kesi yake itakapo bainika
    Pia ni vema Raisi akawawajibisha viongozi wengine wenye tabia ya kupiga watu makofi kama ile iliyotokea huko Iringa. Viongozi tulionao wanapaswa kufahamu kuwa wao ni viongozi tu na wafanye majukumu yao. Wao sio miungu watu.
    Pia kwa vile aliyetenda uhalifua huu ni kiongozi wa serikali. Serikali inapaswa kuchukua jukumu la kuhakikisha hatima ya watoto wa marehemu na ya mjane aliyeachwa.

     
  • Comment #2 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Ni makosa makubwa sana kwa Tibaigana kujifanya kuwa anajua kabisa ni nini kilichotokea. Kwa nini anadai kuwa Bastola ya Ditopile ilifyatuka bahati mbaya kwa kuigonga kwenye dirisha? Inabidi Ditopile mwenyewe athibitishe kuwa hii ilikuwa ni bahati mbaya; na sheria lazima imbanne kwa kutumia silaha, ama kuuwa makusudi, au kwa kitendo cha kijinga na kibabe cha kutumia bastola kugongea dirisha. Tibaigana acha ubabaishaji, usianze kujenga mazingira ya kumuachia mhalifu kabla hata hajafikishwa mahakamani.
     
  • Comment #3 (Posted by Yona Kimori)
    Rating
    Ditopile, as a long-serving government offcial, had no reason to react foolishly. In stead of pulling out his pistol and try to threaten the daladala driver, he could have called the traffic police to arrive at the scene. This is a very serious offence and the law should take its course. However, RC has shown a very bad example to the public in humiliating the a fellow Tanzanian. Being a leader of that callibre does not give an excuse to to abide to the traffic law and country laws in general. I think he deserves a severe punishment!
     
  • Comment #4 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Nadhani tunapojadili tuwe na busara ili hata watakaokuwa wanasoma maoni yetu wapate kujifunza na kuelewa. Sijaona mantiki iliyotumika kumshambulia Tibaigana hapo juu. Ukisoma habari nzima hautaona mahali popote ambapo Tibaigana amesema kwamba ni bahati mbaya. Tusiwe na mtazamo wa chuki binafsi ndipo tutaweza kuwasilisha hoja nzuri zenye kujenga.
    Kitendo alichofanya Ditopile hakiwezi kuvumiliwa; ni vizuri vyombo vya sheria vikafuata mkondo wake na haki ikatendeka.
     
  • Comment #5 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Hata dhamana asipewe ili aonje joto ya jiwe kama walalahoi wengine, maana atatumia fedha yake na za wananchi kuchukua dhamana na kuhonga ili ashinde kesi.Watanzania msikubali, fuatilieni kwa makini.Mahakimu na majaji fuateni haki na sheria zilizopo bila upendeleo wowote.
     
  • Comment #6 (Posted by Jojo)
    Rating
    wewe unknown user wa comment number tatu(3) hapo juu naona huijui Tanzania vizuri, hivi sasa Tanzania kumegeuka kuwa kama nchi za magharibi, watu wana upeo hivi sasa zaidi wa kuelewa na ku-predict yatakayotokea, kingine ni kwamba nchi hizi unahitaji watu wafanye-protest ili serikali iweze kuchukua sheria (enforce law), tumeona mangapi yenye ukweli na serikali haichukui hatua mpaka waunde tume na bado yaliyojiri kwenye tume wala hayafanyiwi kazi. Tibaigana anaweza akawa amechemsha kwa kauli akiogopa kuwaudhi wakubwa, yeye ni mtu wa kuipa media ukweli kwa sababu issue imetokea ndani ya mkoa wake hivyo akikosea tu na watu wanatoa habari si za uhakika ikiwa vilevile kuishutumu serikali inafisha au kupendelea makundi ya wakubwa, Zombe kwani aliwekwa ndani baada ya siku ngapi kupita kiwa anatanua nyumbani kwake? Labda haupo tanzania mwenzangu lakini ukweli ni kwamba Tanzania imejaa uozo fulani katika utendaji wa vyombo vya dola. mfano nchi za wenzetu, by now ungesikia Rais keshamfukuza kazi huyu Dito na yupo under tight security. Tusubiri tuone mambo na jk!!
     
  • Comment #7 (Posted by mnagwa)
    Rating
    aisee; ama kweli hasira ni hasara,gali la mzuzuli linaweza likatengemaa kama linapelekwa garageje itawezekana kurudisha uhai wa hasani mbonde?je tanzania ndio imefikia ivyo,kuua binadamu mwenzio ni kosa kubwa sana hata kama alikukosea, vinginevyo aliyeuawa kama aliweza kuua.Kulikoni kosa kwa accident ndogo,sisi wananchi tunaiyomba kavument ichukue sheria zinazohusika na mauaji bila kujali kama yeye ni nani,kwani hata mbele ya mungu uyu mzee, ameshamkosea.
     
  • Comment #8 (Posted by Edward)
    Rating
    Nimeshangazwa sana na Mkuu wa Mkoa ndugu Ditopile. Lakini hii sio kama ni kitu cha ajabu sana. Watu wengi Watanzania wamekuwa na hisia na maisha ya viongozi wetu. Ndio maana kuna vyama vingi vya siasa, tatizo ni kwamba hatujui jinsi gani ya kuishinda CCM. Hiki chama kina majambazi wengi na sio wote ila wengiwao hawajali maisha ya binadamu. Hali ya kufikia kwamba watu wanakufa muhimbili na wao wanapeleka ndugu zao ulaya na nchi zingine kwa matibabu. Wanajenga majumba makubwa oysterbay na mbezi. Hii ndiyo hali ye kweli na hili tukio sio la kushangaza. Wananchi tunaangalia Raisi Kikwete atajibu nii au atasema nini, huyu ni mwenzake. Pia tutaona jinsi gani Ditopile atajitetea? Mimi ninauhakika Ditopile atatoroka au ataachiwa kwa namna moja au nyingine.
     
  • Comment #9 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Jojo, hapa hakuna anayetaka kutteea uovu ndiyo maana nadhani vema hata mijadala yetu ionyeshe hivyo. Kwamba tunasimamia ukweli. Comment #2: "....bastola ya Ditopile ilifyatuka bahati mbaya ...." Siyo maneno ya Tibaigana. Kama unafuatilia vizuri kwenye vyombo vya habari (magazeti na redio), hakuna maneno kama hayo kwenye kauli ya Tibaigana. Unapotaka kuremba hoja yako kwa kutia chumvi, huo si ustaarabu; tutashindwa kukutofautisha na hao unaowalenga. Tabia chafu ni pamoja na kutunga na kusema uongo.
    Hapa siyo suala la kuijua ama kutoijua Tanzania; ni ukweli tu.
     
  • Comment #10 (Posted by arnie)
    Rating
    Mfumo mzima wa kuteua viongozi tuujadili na tuubadilishe.Wakuu wa mikoa na wa wilaya wengi huwa wameshindwa kugombea ubunge kwani hawata pata kura kutokana na viburi vyao,sasa Rais huwa wengi anawapa appointment si kwa uwezo wao,bali kwa kujuana na kurejesheana fadhila.Lets introduce direct democracy,hawa watu wapigiwe kura na wananchi wa maeneo yao,watajiheshimu na kuheshimu raia,kwani waki tupiga makofi watakosa hizo kura.Tuna wanajeshi wengi wakuu wa wilaya na mikoa, kwa nini?Multy party democracy hairuhusi hicho,kwa mfano kumfanya BRIG. GEN.DR Balele kuwa mkuu wa mkoa wakati bado alikuwa active solder?Swala la DITOPILE,tukumbuke wakati Mwamwindi alipo muua Dr Kleruu kule IRINGA.Raia kamuua mkuu wa mkoa,kesi ilifuatiliwa hadi mtuhumiwa kuhukumiwa kifo.Sasa mkuu wa mkoa kaua raia,sheria ifuatwe,haija badilishwa,ni ile ile.
     
  • Comment #11 (Posted by Jojo is back again)
    Rating
    Bwana uliyetoa comment # 2 na 9 - kama upo tanzania ona hii makala from 'Daily news' ya tarehe 08. (ya leo hii)
    Na nukuu...."Welcome Fredo Tibaigana! He tells the press that 'unfortunately' when Dito was waving the pistol, it went off and the bullet struck the poor driver in the head.

    Braza Tiba, you know that is not it. 'Unfortunately?' is not the word. This is an unfortunate murder charge. Leave it to the lawyers and the lawmen. What is this 'unfortunate' thing? ...."
    Basi niliyoyasema ujue nilimaanisha nini, kuwa mtu kama yeye inabidi awe makini na vyombo vya habari hasa kunapokuwa na matukio. tanzania ndiyo hiyo na system ndiyo inayotuaribu kutokuwa wa wazi hata kwenye issues zinazogusa taifa lote. Can you tell me jinsi Zombe alivyokwenda idara ya maelezo for press conference na kusema kaua majambazi na wakubwa wake walikaa kimya mpaka tume ikaundwa na Rais?? bosi wa zombe alikuwa wapi? please give me a minute jamani.

     
  • Comment #12 (Posted by an unknown user)
    Rating
    hii ni mbaya sana kwa kiongozi mkubwa kama yeye(ccm)na inonesha jinsi gani mzee huyo alivyozoea kuonea na kuzaririsha raia wa chini,hivyo naomba vyombo husika vimpe adhabu kali na ikiwezekana afungwe maisha
     
  • Comment #13 (Posted by ralph nyangi Awino)
    Rating
    does anybody know what happened to RC (mr Mzuzuri), well i know that he was arrested and locked up at one point, but then what happened to him after that, is he serving time? or bailed out on a bond, and how much was it if anybody knows ?
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.