Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »   Mkuu wa Mkoa Ditopile akamatwa kwa mauaji
Mkuu wa Mkoa Ditopile akamatwa kwa mauaji
By Habari Tanzania | Published  11/5/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ramadhan Ditopile Mzuzuri, ametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za mauaji ya raia kwa kutumia bastola yake jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka eneo la tukio zilizothibitishwa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, zinaeleza kuwa Ditopile anatuhumiwa kumuua dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), mkazi wa Kawe Mzimuni, jijini Dar es Salaam kwa kumpiga risasi kichwani.Ditopile, anatuhumiwa kumuua dereva huyo juzi saa 2.30 usiku, katika njia panda ya barabara ya Kawe na Bagamoyo, Wilaya ya Kinondoni, baada ya kuchukizwa na hatua ya gari lake kugongwa kwa nyuma na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu.

Marehemu ambaye alifariki dunia papo hapo, alikuwa akiendesha gari aina Isuzu Journey, linalofanya biashara ya daladala kati ya Ubungo na Tegeta na lilikuwa likitokea Ubungo kwenda Tegeta.Gari hilo lililigonga gari aina ya Prado lililokuwa likiendeshwa na dereva wa Ditopile, Nassoro Mohamed (42), mkazi wa Kijitonyama, Dar es Salaam, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo, mkoani Pwani.

Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa baada ya gari hilo kugongwa, dereva wa Ditopile, alishuka na kwenda kukagua uharibifu uliotokana na tukio hilo. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, gari hilo lilivunjwa taa moja ya nyuma.

Walisema wakati dereva huyo akiendelea kulikagua gari hilo, Ditopile naye alishuka na kuungana na dereva wake katika ukaguzi huo.Walisema baada ya kuona uharibifu huo, Ditopile, alimfuata marehemu na kumtaka ashuke katika gari alilokuwa akiliendesha ili aende kushuhudia uharibifu uliotokea na kisha waende polisi.

Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu, alimweleza Ditopile kuwa ajali hiyo ilitokea kwa bahati mbaya na kumwomba msamaha kwa tukio lililotokea.Walisema mkuu huyo wa mkoa, hakukubaliana na utetezi huo na badala yake aliendelea kumwamuru marehemu ashuke kwenye gari na kumtaka akaeleze maneno hayo polisi.

Mashuhuda hao, walisema marehemu alipoona Ditopile anazidi kutoa maneno ya ukali, aliamua kufunga kioo cha gari kuepuka kuchochea hasira za kiongozi huyo.Walisema kitendo hicho kilimuudhi Ditopile ambaye alichomoa bastola aliyokuwa nayo na kuanza kuitumia kugonga kwenye kioo cha gari la marehemu huku akimsisitiza kushuka katika gari.Hata hivyo, mashuhuda hao, walisema marehemu aligoma kutii amri hiyo ya Ditopile na ndipo alipomfyatulia risasi iliyopenya kwenye kioo cha gari na kufumua kichwa cha marehemu.

Mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika eneo hilo muda mfupi baada ya tukio hilo, alishuhudia mwili wa marehemu ukiwa umeegemea kwenye kiti cha dereva huku damu na ubongo vikiwa vimetapakaa ndani ya gari alilokuwa akiliendesha.Tukio hilo lililozua hofu, lilisababisha mtafaruku mkubwa miongoni mwa watu, wakiwamo madereva na abiria waliokuwa wakisafiri katika njia hiyo, kutokana na mlio wa risasi.


Watu waliokuwa kwenye magari, walishuka na kuanza kukimbia ovyo katika sehemu mbalimbali wakidhani kuwa eneo hilo limevamiwa na majambazi.Watu pekee waliobaki katika eneo hilo, ni dereva anayedaiwa kuwa wa Ditopile na mwanamke ambaye hakuweza kufahamika mara moja ambaye anadaiwa kuwa alikuwa katika gari lililokuwa limembeba Ditopile.

Hata hivyo, wakati hayo yanajiri, hakuna mtu yeyote alimyetambua mtu aliyemfyatulia marehemu risasi isipokuwa dereva wa gari lililokuwa limembeba.Baada ya tukio hilo, mwandishi wa habari hizi, alishuhudia kondakta wa gari hilo ambaye hakuweza kufahamika mara moja, akipambana na mtu huyo wakinyang'anyana bastola inayodaiwa kutumiwa na Ditopile.Katika 'mpambano' huo, bastola hiyo ilidondoka na kondakta na mtu huyo wakaanza kugombea kuiokota.Hata hivyo, kondakta alizidiwa nguvu na mtu huyo aliiokota bastola hiyo na kutokomea nayo kusikojulikana.


Dakika chache baadaye, polisi waliobeba silaha wakiwa ndani ya magari matatu aina ya Lond Rover Defender, walifika katika eneo hilo.Akielezea tukio hilo, Kamishna Tibaigana, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku katika eneo hilo na gari lililombeba Ditopile, lilikuwa na abiria wawili; akiwamo Ditopile mwenyewe na mtu mwingine ambaye hajafahamika. Alisema wote walikuwa wakitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo.

"Mara baada ya ajali hiyo kutokea, magari hayo yalisimama. Dereva Nassoro Mohamed alishuka na kwenda kuangalia gari lake ili kubaini lilivyoharibika/kugongwa, aliliona limepata madhara kidogo upande wa nyuma," alisema Kamishna Tibaigana na kuongeza:

"Wakati Nassoro Mohamed akiendelea kuangalia, alishuka mheshimiwa Kapteni Ukiwaona Ramadhani Ditopile Mzuzuri ili naye aende kuona uharibifu uliotokea. Baada ya kuona uharibifu uliotokea alimtaka dereva wa Isuzu Journey, Hassan Mbonde, ashuke ili naye aone uharibifu uliotokea kisha waende polisi kutoa taarifa.

"Dereva wa Isuzu Journey alikataa kushuka kwenye gari lake na badala yake alifunga kioo cha dirisha la mlango wake kisha alifunga mlango na ku-lock kwa ndani. Mheshimiwa Ditopile Mzuzuri baada ya kuona dereva amefunga mlango, alisogelea dirishani na kutoa bastola yake na kuanza kugonga dirisha kwa kutumia bastola yake, huku akimwamuru ashuke ndipo ghafla alifyatua risasi moja ambayo ilivunja kioo cha dirisha na kumjeruhi Hassan Mbonde kichwani na alifariki dunia papo hapo," alisema Tibaigana katika maelezo yake kwa waandishi wa habari.

Tibaigana, alisema baada ya tukio hilo, dereva Mohamed, aliendesha gari lake na kuondoka sehemu ya tukio akiwa na abiria wake wawili."Mtuhumiwa Ukiwaona Ramadhani Mwinshehe Ditopile Mzuzuri amekamatwa na anaendelea kuhojiwa. Pia mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili," alisema Kamanda Tibaigana.

Asubuhi jana, watu walimiminika katika Kituo cha Polisi Kawe kwa ajili ya kuandikisha maelezo yao juu ya jinsi walivyoshuhudia tukio hilo.Baadhi walisimulia kuwa katika tukio hilo, Mkuu huyo wa Mkoa alipiga risasi mbili ambapo moja ilimkosa marehemu na nyingine ndiyo ilimuua papo hapo.Daladala aliyokuwa akiendesha marehemu Mbonde ilikuwa imeegeshwa katika kituo hicho cha polisi na baada ya baadhi ya watu kutoa maelezo, walitakiwa kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi.

Nyumbani kwa marehemu kulikuwa na watu wachache huku mvua ikiendelea kunyesha na wengi wao walikuwa wakijadili tukio hilo. Marehemu Mbonde ameacha watoto wadogo watatu."Hii inatakiwa Rais aunde Tume kama ilivyokuwa kwa Zombe, hivi hivi hakutakuwa na haki," alisema muombolezaji mmoja.Watu hao walishikwa na hasira na kutaka kuwavamia waandishi waliokuwa msibani hapo baada ya redio moja kutangaza kuwa marehemu alikufa katika ajali.

Habari zilizopatikana msibani hapo zilieleza kuwa marehemu Mbonde atazikwa leo saa saba mchana katika makaburi ya Kawe.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Related Articles
Comments
  • Comment #1 (Posted by McFallan)
    Rating
    Hii haikubaliki na sheria inapaswa ifuate mkondo wake. Inasikitisha kuona viongozi wanajichukulia hatua za kisheria mikononi na hawawajibishwi. Wapo viongozi waliowapiga watu makofi:-Na hakuna hatua yoyote ya kuwawajibisha iliyochukuliwa. Hatimae limefikia hili la kuua mtu kwa sababu ya kugonga gari. Tunamuomba Rais JK: sio kuunda tume bali kuhakikisha sheria zinafuata mkondo wake. Maana tume huundwa pale mazingira yanapokuwa yana utata. Huyu Ditopile amefanya uhalifu sawa na uhalifu wa kawaida. Taratibu ziko wazi. Anafaa 1. Kuvuliwa ukuu wa mkoa mara moja 2. Kukaa rumande pasipo kupewa dhamana (maana hii ni kesi ya mauaji) mpaka pale hatima ya kesi yake itakapo bainika
    Pia ni vema Raisi akawawajibisha viongozi wengine wenye tabia ya kupiga watu makofi kama ile iliyotokea huko Iringa. Viongozi tulionao wanapaswa kufahamu kuwa wao ni viongozi tu na wafanye majukumu yao. Wao sio miungu watu.
    Pia kwa vile aliyetenda uhalifua huu ni kiongozi wa serikali. Serikali inapaswa kuchukua jukumu la kuhakikisha hatima ya watoto wa marehemu na ya mjane aliyeachwa.
     
  • Comment #2 (Posted by Kibusi)
    Rating
    Si vizuri kuchukua tathmini ya viongozi wetu kwa kosa la mtu mmoja lakini pindi jambo kama hili linapotokea ni vizuri serikali ikatuthihirishia kuwa inajali watu wake na kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

    Tukio hili linasikitisha na ni kinyume kabisa na moyo wa upendo na udugu ambao taifa letu linajivunia hasa pale mtu aliyebebeshwa dhamana ya kuisimamia sheria anafanya hivi.

    Labda Ditopile anasumbuliwa na matatizo ya akili!!!!!.......huu ni unyama uliovuka mipaka.
    Pole kwa ndugu na marafiki wa marehemu na Mungu aiweke roho yake pema peponi.
     
  • Comment #3 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Inasikitisha sana kuona viongozi wa serikali wakivunja sheria hadharani. Tena mbaya zaidi ni ya kuua raia. Naamini kabisa hiyo daladala ina namba za usajili na mheshimiwa huyo ina inlfuence ya kupiga simu kwa mamlaka zinazohusika na huyo dereva angechukuliwa hatua ambayo isingesababisha mtu yeyote kupoteza maisha ama kiungo. Hii inaonyesha nchi yetu ina viongozi wa aina gani. Huyo ni mmoja aliyenogewa na vitendo vya unyanyasaji na uuaji mpaka kuvionyesha hadharani. Je ni vingapi ambavyo watu hawajui kuwa vinatokea? hapo hakuna kutunga hadithi wala kupinda sheria kwani kuna wengi watakaoathirika na kitendo kama hicho. Je tunajua kulikuwa na watoto wangapi katika mazingira hayo? wamejifunza nini? Viongozi wa Tanzania hawana utamaduni wa kuheshimu na kustahi wananchi wao na huo ndio mfano halisi. Wengi wanatuonyesha tabia za namma hii kwa maneno yao na sasa wamefikia hatua ya vitendo, wanachi tukae sawa kwani hatujui nani atafuatia kwenye wimbi hili la kupigwa risasi. Huenda hiyo ni moja ya maazimio ya vikao vyao kwamba wakileta ubishi piga risasi. Hapo ndio tunaanza kuangalia azimio la kuruhusu uuzaji wa silaha kwa watu binafsi katika jicho pembuzi. Nani alipitisha na alikuwa na agenda gani? Je hii ndio sababu ya mhusika kuona umuhimu wa watu binafsi kuwa na silaha?
    Hii pia inaonyesha ni kwa jinsi gani mfumo wa nchi yetu ulivyooza, kwani kama kungekuwa na utaratibu mzuri kitu ambacho kingefanyika baada ya ajali ni kwa wahusika kubadilishana information zao za bima na huo uharibifu ungelipwa na bima, kama ilivyo katika nchi nyingine ambapo mtu akipata ajali hawezi kuwa na hofu au kupandwa na jazba. Natumaini mheshimiwa mkuu wa mkoa analijua hilo vizuri sana ila kwa kuwa halitekelezwi na serikali ambayo yeye ni mtendaji mhimu ndio maana aliamua kujichukulia sheria mkononi.
    Fine ameua je taa ya gari lake ilirudia hali yake ya kabla ya ajali?
     
  • Comment #4 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Hiki ni kipimo kingine kwa serikali ya jakaya kwa mwaka 2006. tumeona ya Zombe, tumeona wizi wa silaha mataa ya ubungo, tumeona wizi wa fedha benki ya NBC ubungo, na wote hawa hatujapew ufumbuzi maana ni system inafanya kazi. Hapa hakuhitajiki cha tume wala nini jamani ni kuopteza kodi za mtanzania, ukweli upo wazi hapa!, anatakiwa kuwa Segerea akingojea hukumu yake kwa sasa na si kituo cha polisi, na jakaya anatakiwa kumfuta kazi mara moja ndani ya saa 24 mtu huyu, kwanza ni hatari katika jamii yetu. inashangaza sana mtu aliyekiongozi mkubwa na mwanasiasa wa siku nyingi kutokuheshimu sheria na haki kwa wote. kama sheria haitafuata mkondo wake basi itabidi wanaomlinda wamtafutie 'dito' nchi yake ya kuishi.
     
  • Comment #5 (Posted by Kassam)
    Rating
    Ni picha halisi ya viongozi wetu, si ajabu sana kwani alionyesha ukatili wake kwenye eneo moja. Ukatili wa viongozi upo kila mahala, ona hali za watanzania wanaofanya kazi kwenye makampuni yaliyouzwa. Badala yake wanaambiwa uchumi umekuwa!
    Those who should defend the law are breaking the law openly. Imagine such a killer is RC, the president's representative!
     
  • Comment #6 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Sheria ichukue mkondo wake na haki itendeke.
    Sipendi sana watu wanao-generalize. Eti viongozi wote ndivyo walivyo. Sio kweli; ila cha msingi hapoa ni kwamba haki inatakiwa kutendeka kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria.
    Kwani akitokea mwanaume mmoja akawa shoga, anawakilisha wanaume wote basi. Tuzingatie uchambuzi wenye kujenga hoja na wala siyo jazba ya kila mara kukimbilia "wote ndivyo walivyo" Kasumba hiyo imepitwa na wakati, na inalemaza akili.
     
  • Comment #7 (Posted by Jon Maxshaka)
    Rating
    Ili amani izidi kuwepo, na pia wananchi wae na imani na serikali yao, Ditopile ni lazima afutwe uongozi mara moja na pia kupelekwa Segerea wakati kesi yake ikifanyiwa uchunguzi zaidi.

    Hii ni kosa la jinai, hakuna cha Dhamana kwa sasa, na pia ni lazima mtu huyu (ditopile) apoteze posho zote ambazo anapokea toka kwa walipa kodi kwa maana ametenda kosa la Jinai ambalo haliitaji Tume wala nini. Wapenda haki, Huyu mtu lazima aukumiwe kwa mujibu wa sheria.
     
  • Comment #8 (Posted by Amon Muganyizi)
    Rating
    This is absurd. Nategemea kuwa Ditopile atachukuliwa hatua kali ya kisheria. Nafikiri kwa kuwa ni mkuu wa mkoa ana uhuru wa kwenda na kuua watu ovyo.Yeye kama rahia hana haki ya kumuaru mtu kufanya chochote. Nafikir kitu ambacho angekifanya ni kutoa taarifa polisi na police ndio wange wangeamua kumchukulia hatua dereva huyo. Nfikiri dereva alikuwa na haki ya kufunga kioo kwa kuwa alikuwa anatishiwa na mtu aliyekuwa na hasira.
    Ningependa kufuatilia kesi hii kuona jinsi sheria inavyotumia hapo nchini kwangu.
    Amon Muganyizi
    4332 Ohio Street
    Omaha, NE 68111
    United States of America
    Muganyizi@qwest.net

     
  • Comment #9 (Posted by Switbert Msoga)
    Rating
    Ni kitu cha kusikitisha sana kusikia Mkuu wa Mkoa anampiga risasi na kumuua raia wa hali ya chini katika mazingira kama hayo, eti kwa vile taa ya gari lake imegongwa. Mkuu wa Mkoa ni kiongozi wa hali ya juu anayepashwa kuwa muadilifu na kuonyesha nidhamu ya hali ya juu na kuheshimu raia ambao ndio wapiga kura. Sitaki kuzungumzia pengo kubwa la hali ya maisha lililopo baina ya viongozi wetu na wanainchi wa kawaida ila kwa hili lilitokea kila Mtanzania anasikiliza na kungoja kuona kuwa hali inatendeka na sheria inachukua mkondo wake.
     
  • Comment #10 (Posted by joshua mtinangi)
    Rating
    Bila shaka yoyote mhe. Dito anajutia jambo alilolifanya kuliko hata sisi. Sifa yake nzuri ya utumishi wa umma kwa muda mrefu imefutika ghafla. Naamini kilichomfanya mhe. kuchukua hatua ya kuua si gari yake kugongwa mbali majibizano yake na marehemu yaliyomfanya ahisi kuwa amedharauliwa sana ukitilia maanani kuwa yeye ni askari mstaafu na pia ni mkuu wa mkoa. Viongozi wanapaswa kuepuka kupishana jambo lolote na watu wa chini yao hasa wakiwa nje ya maeneo yao ya kazi. Dereva wa mhe.Dito angeweza kuepusha balaa hili kama angejali usalama wa bosi wake kuliko kujali uharibifu wa gari.Dereva ni mlinzi wa mheshimiwa, kwa namna yoyote ile asingemrusu kushuka kwenye gari. Hata baada ya kushuka alitakiwa aandamane naye. Nawiwa kusema kuwa dereva wa Dito amechangia kutokea kwa kifo hicho. Madereva wanaoendesha wakubwa wanatakiwa kufundishwa mambo ya usalama wa mabosi wao. Naamini wengi ni mambumbu kabisa.
     
  • Comment #11 (Posted by omari)
    Rating
    what Dito did is a stupid act especially to this country.Taking into accout he is a leader and he has been a leader for long time.This should be condemed by all people despite their colour,age,sex,religion and more important their political affiliation
     
  • Comment #12 (Posted by Brian Jonathan Kithuku)
    Rating
    Huu ni unyama wa hali ya juu ambao hauvumiliki popote. Katika nchi yetu ambapo viongozi wetu wametuaminisha kwamba wanazingatia utawala wa sheria, hii ni nafasi ya kuthibitisha kwamba tunamaanisha tunachokihubiri: utawala wa sheria. Hatua zichukuliwe ipasavyo na haki itendeke.
     
  • Comment #13 (Posted by vicky)
    Rating
    huyu ditopile adhabu yake iwe kunyongwa tu nawapa pole sana ndugu na jamaa wa marehemu na raisi kikwete asilete kulindana watanzania tuungane kutetea haki za mareemu alie poteza maisha kwa kugonga plado
     
  • Comment #14 (Posted by rosemary)
    Rating
    Kama nilivyojitambulisha hapo juu,kwakweli nimeshtushwa na taarifa hii ,kwakweri siwezi kusema nikiasi gani nilipata na mshtuko.Niko mbali sana na inchi yangu ,Pia siwezikufanya kitu chochote juu ya hili swala.
    Namjua Ditopile ni mpenda watu mcheshi si mgomvi lazima kutakuwa na kitu,labda alipatwa na alipoteza ufahamu ,Au.nikitu cha kushanga sana ,pia cha kusikitisha,Wewe unafikiri ni mara ngapi alishawai kupatwa na mashwaiba makubwa zaidi ya ili?Mimi nafikiri ni mengi na hakuwai kuua au kuadhibu mtu iweje leo?Ameua ndio na ukichunguza sana hakukusudia,ilikuwa si hamli yake.Nimara ngapi madereva,majambazi,pia polisi wanaua tena kwakukusudia na wanaachiwa huru baada ya muda?Tena wanaua mtu zaidi ya mmoja?Hakukusudia hapewe adhabu lakini sio kifo ,Rosemary,Amsterdam holland
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.