Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbunge aomba Magereza itoe ardhi
Mbunge aomba Magereza itoe ardhi
By Habari Tanzania | Published  11/5/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Hussein Issa, Mtwara

UONGOZI wa Gereza la Namajani, Wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara umeshauriwa kuliachia eneo kubwa la ardhi wanalomiliki na kuwapa wananchi ambao watalitumia kwa kilimo.

Mbunge wa Masasi, Raynald Mrope (CCM) aliiambia Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalum kuwa gereza hilo linamiliki eneo kubwa ambalo halitumiki na kuliacha likiwa pori huku wananchi wakihangaika kutafuta sehemu ya kulima.

“Nashangaa sana kuona Magereza wanamiliki eneo kubwa mno ambalo nina hakika halitumiki sasa kwanini wasiachie wananchi walitumie katika harakati za kujiepusha na adha hii ya njaa," alisema Mrope.

Hata hivyo, alishukuru juhudi za serikali kuingilia kati suala hili kati kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wa Masasi kupata ardhi na kuepuka na njaa inayotokana na ukosefu wa mashamba huku kukiwa na ardhi isiyoendelezwa.

Mbunge huyo aliongeza kuwa wananchi hao hawataki kutumia eneo lote, isipokuwa sehemu kwa ajili ya kulima mazao au hata mboga mboga za muda mfupi nasio kulimiki eneo la gereza kama wanavyodai viongozi wa gereza hilo.

Aliwataka viongozi hao waachie sehemu ndogo ambayo hawaitumii kwa wananchi kuwapa nafasi ya kilimo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.