Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Viongozi Afrika wanastahili lawama
http://www.habaritanzania.com/articles/1686/1/Viongozi-Afrika-wanastahili-lawama
By Ramadhan Semtawa
Published on 11/5/2006
 
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya chama cha NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amewashutumu viongozi wa mataifa ya Afrika kwa uchu wao wa madaraka ambao umekuwa chanzo cha vita na machafuko yanayosababisha wakimbizi.

Na Ramadhan Semtawa

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya chama cha NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amewashutumu viongozi wa mataifa ya Afrika kwa uchu wao wa madaraka ambao umekuwa chanzo cha vita na machafuko yanayosababisha wakimbizi.

Alisema kutokana na uchu huo, viongozi wengi wa Afrika wamekuwa wakijaribu kuingia madarakani kwa kutumia njia za kuwagawa wananchi kidini, kikabila na hata kimajimbo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi wakati wa mkutano wa asasi zinazotoa msaada wa kisheria katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dk Mvungi, alisema ni uongo kusingizia Wazungu kwamba wanaichafua Afrika.

Dk Mvungi aambaye alikuwa akizungumza katika mkutano huo uliaofanyika katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), jijini Dar es Salaam alieleza kwamba, hakuna ukoloni unaojipenyeza Afrika ambao unaweza kuwa chanzo cha machafuko isipokuwa viongozi wenyewe ndiyo chanzo.

"Uchu na uroho wa madaraka wa baadhi ya viongozi wetu wa Afrika ndiyo chanzo cha machafuko yanayozalisha wakimbizi barani Afrika," alisema Dk Mvungi na kuongeza,:

" Wanaingia madarakani kwa kutumia njia za kugawa wananchi kama udini, ukabila na hata ujimbo, matokeo yake wakiingia madarakani hutokea machafuko." alisi
sitiza.

Mwanataaluma huyo ambaye pia ni mwanasiasa, alisema hali hiyo pia iliikumba Tanzania, kule visiwani mwaka 2001 baada ya kuzalisha wakimbizi kwa mara ya kwanza ambao walikimbilia Shimoni, Mombasa.

Kwa upande mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), tawi la Tanzania, Veronica Moday Ebi, alisema wakimbizi kama walivyo watu wengine wanapaswa haki zao za msingi za kibinadamu kama zilivyoanishwa katika Tamko la Dunia la Haki za Binadamu la mwaka 1948.