Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ajali ya treni yajeruhi 30
Ajali ya treni yajeruhi 30
By Habari Tanzania | Published  11/5/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi Wetu

ABIRIA 30 wamejeruhiwa baada ya mabehewa mawili ya treni ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuacha njia na kupinduka katika stesheni ya Kaliua, Mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Muhudi Mushihiri aliliambia Mwananchi Jumapili kwa simu kutoka Tabora kuwa katika ajali hiyo, watu 20 walitibiwa na kuruhusiwa kuendelea na safari yao kuelekea Mpanda, Mkoa wa Rukwa wakati wengine 10 walilazwa.

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo iliyotokea katikastesheni ya Kaliua hakijajulikana, lakini uchunguzi ulikuwa ukiendelea kwa kuhusisha maofisa wa polisi wa TRC.

Kamanda huyo alisema kuwa ajali hiyo ilitokea saa 3.40 asubuhi na kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha katika tukio hilo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.