Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali yabanwa iuze magari ya kifahari
Serikali yabanwa iuze magari ya kifahari
By Habari Tanzania | Published  11/4/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Abdallah Bawazir, Dodoma

MBUNGE wa Ubungo, Charles Keenja, ameishauri serikali kuuza magari yake yenye gharama kubwa ili fedha zitakazopatikana zisaidie katika kutoa mikopo kwa wanafunnzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini.

Keenja alitoa ushauri huo jana bungeni, wakati wa kipindi cha maswali majibu. Awali mbunge huyo aliitaka serikali pia kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaofaulu kwa kiwango cha daraja la pili badala ya daraja la kwanza pekee kwa kuwa utaratibu huo unawanyima wanafunzi wengi hasa wanaotoka katika familia masikini fursa ya kuendelea na masomo ya juu.

“Sikubaliani na dhana kuwa nchi hii haina fedha. Serikali ina magari mengi ya thamani, yangeuzwa haya na fedha zikatumika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu,” alisema mbunge huyo.

Akijibu ushauri huo, Naibu Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Gaudencia Kabaka, bila ya kugusia suala la magari, alisema serikali inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha upungufu wa fedha za mikopo kwa wanafunzi unapatiwa ufumbuzi, ikiwa ni pamoja na kuwahimiza watu waliokopa na wameshamaliza masomo yao kurejesha mikopo hiyo ili iweze kugawiwa kwa watu wengine.

“Serikali inawataka watu wote waliokopa katika kipindi cha mwaka 1994/95 kurejesha mikopo hiyo na tayari tumekwisha waandikia waajiri barua ili kuhakikisha mikopo hiyo inalipwa,” alisema Kabaka.

Alisema serikali pia imekuwa ikiidamini Bodi ya Mikopo kukopa fedha ili wanafunzi wengi zaidi wapate kunufaika na mikopo hiyo.

Kuhusu wanafunzi wa kiume waliopata daraja la pili nao kupewa mikopo, Kabaka, alisema kikwazo kikubwa kinachozuia wanafunzi wa madaraja mengine kupewa mikopo hiyo ni uwezo mdogo wa kifedha wa serikali.

Alisema ongezeko la mahitaji ya fedha kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, limetokana na ongezeko la posho ya chakula na malazi, ongezeko la muda wa mafunzo kwa vitendo kwa baadhi ya mitaala kutoka wiki sita hadi tisa na idadi kubwa ya waombaji wenye sifa.

Alisema katika kipindi cha masomo cha 2005/6, Bunge liliidhinisha Sh32.2 bilioni kwa Bodi ya Mikopo lakini kiasi hicho hakikukidhi mahitaji ya wanafunzi wote waliotimiza masharti ya kupewa mikopo, hali iliyoilazimu serikali kuidhamini bodi ya mikopo na kukopa Sh31 bilioni kutoka PSPF hivyo kufanya fedha za mikopo kufikia jumla ya Sh63.5 bilioni iliyoweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi 42,729, sawa na asilimia 82.72 ya wanafunzi wote 51,657 waliokuwa katika vyuo vyote vya elimu ya juu.

Kwa mwaka huu wa masomo wa 2006/7, Naibu huyo waziri alisema Bunge limepitisha Sh63.5 bilioni na kwamba kiasi hicho kimeshindwa kukidhi mahitaji yote ya wanafunzi.

Alisema kutokakana na upungufu huo, serikali kwa mara nyingine, imelazimika kuidhamini Bodi ya Mikopo kukopa Sh47.8 bilioni. Alisema mkopo huo umewezesha fedha za mikopo kwa wanafunzi kwa mwaka huu wa masomo kufikia Sh111.3 bilioni, kiasi ambacho kitakidhi mahitaji ya wanafunzi 51,064 sawa na asilimia 75.07 ya wanafunzi wote 68,029 wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu nchini


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.