Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Rais Karume:Zanzibar shwari
Rais Karume:Zanzibar shwari
By Habari Tanzania | Published  11/4/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, amesema hakuna mpasuko wa kisiasa visiwani humo na wala hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea juu yake wala uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari wa kuelezea mafanikio ya serikali yake katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani, alisema tatizo lililopo ni kwamba wananchi na hasa Chama cha Wananchi ( CUF), hawakumuelewa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema chimbuko la neno mpasuko wa Zanzibar lilitokana na hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa bungeni Dodoma Desemba 30 mwaka jana kuhusiana na mikakati yake ya kumaliza mpasuko wa Zanzibar.Alisema CUF ilichukua sehemu ndogo ya hotuba ya Kikwete kwa lengo la kupotosha wananchi.Kwa mujibu wa Karume, alichosema Rais Kikwete ni suluhu ya watu wa Zanzibar hasa Pemba ambapo wananchi wameamua tu kupigia kura chama cha upinzani.

Rais Karume alisema hakuna mazungumzo yanayoelezwa na vyombo vya habari kuhusiana na suala la mpasuko wa Zanzibar na akatupilia mbali mapendekezo ya wasomi ya kutaka serikali ya umoja wa kitaifa.Alisema hakuna taarifa anayoijua yeye ndani ya Chama Cha Mapinduzi wala nje ya chama kuhusiana na mazungumzo juu ya mpasuko wa Zanzibar, bali anachofahamu yeye ni tatizo ndani ya CUF, na kwamba kama wanashindwa kuyatatua CCM iko tayari kuwasaidia.

"Hao wasomi waliopendekeza serikali ya umoja wa kitaifa ni wasomi ambao wamepotea, wamepotoka na wanapoteza muda wao," alisema Karume.Alisema kamwe haiwezi kuwepo serikali ya mseto wala ya umoja wa kitaifa kwa sababu CCM ilipewa ridhaa ya kuongoza kwa kura za wananchi.Kwa kauli hiyo Karume amejitokeza kwa mara ya kwanza kuunga mkono kile kilichozungumzwa na Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna kuwa hakukuwa na mpango wowote wa kuunda serikali ya mseto visiwani humo.

Akizunguzia njaa visiwani Pemba, Rais Karume alisema serikali imefuatilia na kubaini kuwa hakuna aliyekufa njaa wala aliyelala njaa bali kilichokuwepo ni upungufu wa pesa za kununulia chakula kilichojaa madukani.Kauli hiyo ya Karume imekuja wakati kumekuwepo na taarifa za kukanganya kuhusiana na suala hilo. Awali, uongozi wa serikali katika eneo hilo ulikanusha kuwepo kwake na baadaye ukakiri na kuomba msaada.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.