Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  JK asisitiza wawekezaji kutoa ajira kwa Watanzania
JK asisitiza wawekezaji kutoa ajira kwa Watanzania
By Habari Tanzania | Published  11/3/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Noor Shija, Tokyo , Japan
 
RAIS Jakaya Kikwete amefafanua kuwa Tanzania inahitaji wawekezaji kutoka duniani kote, lakini amesisitiza kwamba wawape kipaumbele katika ajira Watanzania wenye uwezo ambao ni wengi, badala ya kufikiria kuwapa ajira watu wanaotoka katika nchi zao.
 
Rais Kikwete alitoa ufafanuzi huo kufuatia taarifa iliyonukuliwa kimakosa na gazeti hili kwamba amewakataa wawekezaji kutoka India na Pakistan.
 
“Siyo kwamba hatuwataki wawekezaji kutoka India na Pakistan, nilichosema ni kwamba Tanzania kumejaa wawekezaji kutoka India na Pakstan, lakini bado hawatoshi. Tunahitaji wawekezaji zaidi kutoka duniani kote, lakini nasisitiza kuwa watoe kipaumbele cha ajira kwa Watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi hizo,” alisema Rais.
 
“Tanzania inahitaji wawekezaji wengi kutoka Japan ili kuongeza ajira na kuwajengea uwezo Watanzania zaidi,” alisema katika ufafanuzi wa mazungumzo yake na mtaalamu wa uchumi wa Japan, Dk. Shoichi Kobayashi.Kobayashi ndiye aliyeandika mpango ‘Min Tiger 2020’ ambao unalenga kukuza pato la Mtanzania kutoka dola 375 za Marekani kwa mwaka za sasa hadi dola 1,500 kufikia mwaka 2020 na kukuza pato la taifa toka dola bilioni 10 kwa sasa hadi dola bilioni 40 mwaka 2020.
 
Rais Kikwete alisema Tanzania ina wawekezaji wengi kutoka bara Asia, zikiwemo India na Pakistan, “lakini tungependa na Wajapan nao waje kwa wingi ili kuweza kufikia malengo ya kuondoa umasikini”.
 
Rais alibainisha kuwa kuna bidhaa kutoka Japan, lakini sasa Tanzania inahitaji wawekezaji wa kuwekeza katika sekta mbalimbali, hasa viwanda, ili kutoa ujuzi na ajira nyingi kwa Watanzania kwa lengo la kuinua uchumi wa Mtanzania.
 
Rais Kikwete jana alimaliza kutembelea Japan na leo anakwenda China kuendelea na ziara ya kikazi ya kujitambulisha na kutafuta wawekezaji.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Hamis s nsombo)
    Unrated
    Habari hiyo ni nzuri wawekezaji wengi kutoka asia hasa india na pakistan wamekuwa wakiaji wafanyakazi wengi kutoka inchi zao hata kwa kazi zisizo na ujuzi.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.