Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mama Salma ahimiza uelewano wa walimu na wanafunzi
Mama Salma ahimiza uelewano wa walimu na wanafunzi
By Habari Tanzania | Published  11/2/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Noor Shija, Tokyo, Japan
 
MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete amesisitiza kuwa mahusiano mazuri baina ya wanafunzi na walimu yanamjengea mwanafunzi msingi mzuri wa elimu.
 
Alisema hayo wakati akizungumza na walimu na wanafunzi mara baada ya kutembelea shule ya msingi ya Bancho, mjini Tokyo, iliyofunguliwa miaka 135 iliyopita.
 
Mama Salma alisema ushirikiano shuleni utawasaidia wanafunzi kushika na kuendeleza mambo mbalimbali wanayofundishwa wakiwa darasani.
 
“Shule ya msingi ndiyo mahali ambapo watoto wanatayarishwa kuwa viongozi wazuri wa baadaye na raia wema kwa taifa lolote, hivyo ni bora kukawa na mahusiano mazuri baina yao na waalimu,” alisema.
 
Wakati wa ziara hiyo, Mama Salma alitembelea darasa la sayansi ambapo alishuhudia watoto wanavyotayarishwa kuipenda elimu ya sayansi kwa kufundishwa kwa vitendo mambo yanavyoweza kubadilika kutoka uasilia wake na kuwa katika mfumo mwingine.
 
Alitumia wakati huo kuishukuru serikali ya Japan kwa misaada inayotoa kwa Tanzania, hasa katika sekta ya elimu, ambayo alisema hivi sasa imeboreshwa zaidi.
 
Shule ya msingi ya Bancho imewahi kutembelewa na Mama Maria Nyerere, mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Mbongo)
    Rating
    tatizo ni kwamba anapita huko huko akinadi hiyo NGO yake na wake wa ndugu zake wanaokula kwenye serikali ya awamu ya nne. akijifanya anawawakilisha wanawake wa kitanzania, hii ni material advantage ya nafasi aliyonayo. anatakiwa kunadi mali asili za kitanzania na utalii na nchi kwa ujumla na siyo kutafata mahapa pa yeye kuponea na ukoo wake huko baadaye. hatuna chuki na yeye salma lakini tumeshangatwa wakati wa serikali ya ben na mke wake anna hivyo hatuwezi kukaa kimya kuona wanatumia vyeo vya mabwana zao kuhamisha mali za mlipa kodi na misaada wanayopewa walalahoi.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.