Kibondo
Jeshi la magereza wilayani Kibndo limetoa wito kwa wananchi kubadili mwelekeo wa kuona fahali watu kufungwa jela badala yake wajenge tabia ya kuelimishana kabla ya kosa.
Wito huo umetolewa na mkuu wa gereza wilayani Kibondo Bw. Muhamed Hamis wakati akitoa mada juu ya suala la ulinzi na usalama pamoja na uhamiaji haramu wilayani Kibondo.
Bw. Hamis ameeleza kuwa haina maana kwa wananchi kuona fahali watuhumiwa wengi wanapotiwa mbaroni na kufungwa jela bali ni fahali kupambana na uharifu na kupunguza kiwango cha wanafungwa.
Amesisitiza kuwa magereza wilayani Kibondo hayana nafasi ya kutosha kulingana na kasi za watu kufanya uharifu hivyo jamii haipaswi kujivunia hilo, badala yake washirikiane na jeshi la polisi kutokomeza wimbi la uharifu ili kusiwepo wanaofungwa.
Ameongeza kuwa upo mpango wa kuwaachia wafungwa waliorekebika tabia na wenye vifungo vidogo maarufu kama parole ambao pindi utakapoanza rasimi baadhi ya wafungwa watakuwa nje ya magereza kwa uchunguzi.
Aidha Bw. Hamis amewaonya viongozi wa vijiji, kata na tarafa kuwa wanapaswa kutoa elimu kwa wananchi wao na amewataka wao wenyewe wasijihusishe na uvunjifu wa sheria za nchi.
Alibainisha kuwa idadi kubwa ya wafungwa wanaofungwa miaka mingi ni wa makosa ya ubakaji, utumiaji wa silaha, ujambazi na mauaji ambapo wengi wao hufungwa mika kati ya 30 na 90.
Akionyesha kusikitishwa na hali hiyo Bw. Hamisi alisema wengi wa wafungwa waliohukumiwa miaka mingi familia zao ziekata tama na baadhi ya wanawake wamekuwa wakienda magereza kuwaomba taraka waume zao ili waolewe kwa wanaume wengine