Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  MHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YATOA HUKUMU KWA WAUAJI
MHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YATOA HUKUMU KWA WAUAJI
By Prosper Kwigize | Published  11/1/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Kibondo
 
Mahakama kuu kanda ya tabora inayoendelea na kikao chake katika mahakama ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imetoa hukumu nane kwa watuhumiwa wa kesi za mauaji ambapo wawili wameachiwa huru.
 
Katika kikao hicho kilichofanyika mwishoni mwa wiki hkimu mwenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji kutoka Kigoma mheshimiwa Stephen Awasi amemhukumu kifungo cha cha nje cha miezi 12 askari wa jeshi la wananchi mwenye namba MT 70335 PTE Robert Wangwe aliyebainika kumuua Bw. Stephen Nzowa mkazi wa kijiji cha Kanyomvi, Kakonko.
 
Wengine waliohukumiwa vifungo ni pamoja na James Kasindye mkazi wa wilaya ya Kibondo ambaye atatumikia kifungo cha miaka kumi jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Bw. Juma Magogwa mkazi wa kijiji cha Kanyonza, kakonko wilayani Kibondo.
 
Mheshimiwa Awasi amemuhukumu kifungo cha miaka minane jela Bw. Jonas Ruyungu (33) mkazi wa Kigoma baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Ntacho Nkoreye mkazi wa kijiji cha Kagezi wilayani Kibondo.
 
Aidha mahakama hiyo imemtia hatiani Bw. Kataga Buchabucha wa Kibondo kwa kosa la kumuua Bw. Kajolo Bujanja wa kijiji cha Kumshindwi na amehukumiwa kwenda jela kwa jumla ya miaka tisa.
 
Mwingine simamishwa kizimbani kwa tuhuma ya mauaji ni Bw. Kanyundo Matabe (52) ambaye ameuepuka mdomo wa jela baada ya kufutiwa shitaka na mkurugenzi wa mashitaka wa serikali, ingawa alidaiwa kumuua Bw. Bernard Bichuro.
 
Kwa upande mwingine Bw. Zenobius Vincent (28) ambaye alishtakiwa kwa kosa la kumuua Bw. Narobo Kalimanzira makzi wa kijiji cha Bitare, amehukumiwa kifungo katika magereza ya vichaa Milembe Dodoma baada ya kubainika kuwa kitendo chake kilishinikizwa na kutokuwa na akili timamu yaani Kichaa.
 
Walioachiwa na mahakama baada ya kubainika kutokuwa na kosa ni Bi. Zubeda Helena na Chubwa Emanuel ambao kwa pamoja walidaiwa kumuua Bw. Juma Karol mkazi wa kijiji cha Kasanda wilayani Kibondo mwaka 2002.
 
Mahakama kuu kanda ya Tabora inatarajia kukaa tena katika mahakama ya wilaya ya Kibondo alhamisi wiki hii baada ya mapumziko ya sikukuu ya Idd el Fitri

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Favourites' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.