Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  DAWASCO kutengeneza bomba la maji machafu Mikocheni B
DAWASCO kutengeneza bomba la maji machafu Mikocheni B
By Habari Tanzania | Published  05/30/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi Wetu
 
KAMPUNI ya Huduma za Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) imesema inatarajia kukamilisha matengenezo ya bomba la maji machafu katika eneo la viwanda, Mikocheni B ambalo limepasuka na hivyo kusababisha kero kwa wananchi.
 
Hatua hiyo inafuatia malalamiko ya wananchi wa Mikocheni kufuatia kuvunjika kwa kipenyo cha bomba hilo na hivyo kusababisha maji machafu yenye kemikali kutiririka barabarani na hatimaye kuchangia uchafuzi wa mazingira.
 
Meneja wa Maji Machafu wa DAWASCO, Gasper Kilango, alisema jana kuwa matengenezo ya bomba hilo yataanza wakati wowote na kwamba kuchelewa kushughulikia mapema kulitokana na sababu za kiufundi.
 
Kilango alisema walikuwa wakifanya upembuzi yakinifu juu ya saizi ya bomba linalohitajika kwa vile lililokuwepo awali lilikuwa halina uwezo wa kuhimili kiwango cha uchafu unaotoka viwandani.
 
Bomba la maji machafu linalosafirisha uchafu kutoka katika viwanda vya Mikocheni liliharibika wiki kadhaa zilizopita baada ya magari kuvunja kipenyo kwenye eneo la kiwanda cha chuma cha MMI Steel Limited, hivyo kusababisha uchafu ulioambatana na kemikali kusambaa barabarani na kutoa harufu kali.
 
Kufuatia hali hiyo, wananchi wa Mikocheni B walilalamikia hali hiyo huku shutuma zikielekezwa kwenye kiwanda kimoja kinachotengeneza karatasi laini cha Tanpack Tissues Limited kuwa ni chanzo cha uchafu huo wenye kemikali.
 
Hata hivyo, uongozi wa kiwanda hicho ulikanusha kuhusika na hali hiyo kwa madai kwamba wanaopaswa kubeba lawama hizo ni DAWASCO ambao walielezwa juu ya hali hiyo lakini hawakuchukua hatua mapema.
 
Meneja Mkuu wa Tanpack Tissues Limited, Rajesh Shah alisema jana kuwa malalamiko juu ya kiwanda kutiririsha maji machafu lipo kwa muda mrefu na kwamba alishawasiliana na mamlaka husika za mazingira zikiwemo serikali za mitaa Mikocheni B.
 
"Tanpack inaonekana kutiririsha maji kwa vile inatengeneza bidhaa za rangi. Lakini watu lazima wajue kwamba viwanda vyote vya Mikocheni vinatumia bomba hili kusafirisha maji machafu, hivyo lawama hizi hazina budi kupelekwa kwa wenye viwanda wote," alisema huku akionyesha ramani ya mfereji huo wa maji machafu.
 
Shah alisema baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi, kampuni yake ililipa DAWASCO sh. 80,000 kwa ajili ya kujenga bomba hilo ili kuwaondolea wananchi kero wanayoipata.
 
Alisema kuvunjika kwa mfuniko wa kipenyo cha bomba hilo kulitokana na magari kupita pembeni mwa barabara wakati kampuni moja ya ujenzi kutoka China ilipokuwa ikifanya kazi ya kuchonga barabara hiyo.
 
Meneja Mkuu huyo pia alikiri kuwa uwezo wa bomba la maji machafu ni mdogo kulinganisha na kiasi cha maji machafu yanayopita, hali ambayo alisema kampuni yake ililazimika kulipa fedha zaidi kwa ajili ya kupata bomba kubwa.
 
Kutoka gazeti la Uhuru

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.