Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Madaktari Watanzania wafa ajalini Nigeria
Madaktari Watanzania wafa ajalini Nigeria
By Habari Tanzania | Published  11/1/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Agnes Yamo

MADAKTARI wawili raia wa Tanzania wamefariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea Abuja nchini Nigeria Oktoba 29.

Madaktari waliofariki dunia katika ajali hiyo wametajwa kuwa ni Dk. Nakijwa Kanyika wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na Dk. Moshi Ruhiso wa Hospitali ya Makandana ya Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaeleza kuwa, Watanzania hao waliwasili nchini Nigeria Oktoba 27 kwa shughuli za kikazi zilizokuwa zikiratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

“Maiti za Watanzania hao zilitambuliwa na Watanzania wenzao, Dk. Esther Mwakitalu pamoja na Dk. Harriet Hamis, ambao waliongozana nao huko Nigeria. Hao walibaki Lagos kwa ajili ya kwenda jimbo jingine,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Mipango ya kuisafirisha miili ya Watanzania hao inafanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria kwa kushirikiana na WHO. Miili hiyo inatarajiwa kuondoka Abuja leo kuja Dar es Salaam.

“Serikali imesikitishwa na vifo hivyo na imetuma rambirambi kwa familia za marehemu, ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo,” ilieleza sehemu ya taarifa.

Ndege ya abiria aina ya Boeing 737 ilianguka Oktoba 29 ikiwa ni muda mfupi baada ya kupaa kuelekea katika Jiji la laskazini la Sokoto nchini Nigeria.

Katika ajali hiyo, watu 100 walifariki ambapo watu sita wanadaiwa kunusurika na taarifa zaidi zinasema kuwa Rais wa Nigeria, Olusegun Obasanjo ameagiza kuanza kwa uchunguzi wa ajali hiyo


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.