Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Jeff Msangi  »  UNAIPENDA NCHI YAKO?
UNAIPENDA NCHI YAKO?
By Jeff Msangi | Published  11/1/2006 | Jeff Msangi | Rating:
Na Mwandishi wa HabariTanzania.com

Mtanzania mwenzangu,

Kwa mtazamo wa kawaida na wa kijuujuu,watanzania tunajulikana kwa kuwa wazalendo sana. Tunasemekana kuwa watu tunaoipenda nchi yetu na tunaojipenda pia. Tumejipa majina kemkem katika kujivunia utanzania wetu. Nchi yetu inajulikana miongoni mwa wengi kama “bongo” yaani akili.

Zamani zile “bongo” ilikuwa ni jiji la Dar-es-salaam tu,siku hizi bongo ni Tanzania nzima au niseme Tanganyika nzima ingawa najua kuna watu wanajidai kwamba jina Tanganyika halimo katika msamiati wao. Huko ni kujidanganya na kupotosha historia.

Kwa wengi, ingawa sera za kiuchumi za Mwalimu Nyerere zilifeli,sera za kijamii zilifanikiwa sana. Mojawapo ya mafanikio ya kijamii ni pamoja na hili la “uzalendo”.Mapenzi yasiyo kifani kwa nchi yetu,popote tulipo tunaiota Tanzania nk.

Leo nataka niangalie kidogo kama kuna ukweli wowote kwamba tunaipenda sana nchi yetu. Lakini kabla sijaenda mbele sana naomba niweke wazi kwamba mimi siamini kama tunaipenda kweli nchi yetu kama tunavyodai. Naona tunashabikia nchi yetu lakini hatuipendi nchi yetu.

Kwani nchi ni nini basi? Nchi ni mbuga za wanyama? Nchi ni maeneo ya kijografia aliyotuwekea mkoloni? Nchi ni mashamba yasiyozalisha? Tafsiri ya nchi inaweza kuwa ngumu sana, kila mtu anaweza akawa na tafsiri yake na kila mmoja akawa sawa.Kwangu mimi nchi ni yote hayo hapo juu na mengineyo pamoja na watu wake. Sipati picha na “nchi” bila watu.

Nchi yetu ipo ilipo kwa sababu ya ukosefu wa “uzalendo”.Tofauti na madai ya wengi wetu,mapenzi (uzalendo) kwa nchi yetu ni kama hakuna. Kama unaipenda nchi yako,utaiibia? Kama unaipenda nchi yako utakula rushwa? Kama unaipenda nchi yako hutoonyesha wazi bali mpaka utolewe kashfa ndio uzinduke? Kama unaipenda nchi yako utakwepa kodi? Kama unaipenda nchi yako utakuwa mzembe kazini? Kama unaipenda nchi yako utaloga wenzako?

Kama unaipenda nchi yako utaacha kuichagulia viongozi bora na sio kwa kusubiri upewe rushwa? Kama unaipenda nchi yako utaikana? Kama unaipenda nchi yako utaachia wageni waje na kuchuma uchumi wote wa nchi ilhali wewe umekaa tu kibarazani?

Kama unaipenda nchi yako utakuwa huijui hata historia yake achilia mbali jiografia yake? Kama unaipenda nchi yako utajifanya huijui hata lugha rasmi ya nchi yako ili mradi uonekane bora miongoni wa kundi fulani la watu? Kama unaipenda nchi yako mbona huungi mkono chochote cha kitanzania kiwe ni sanaa au bidhaa za nyumbani?

Maswali yanayohoji “uzalendo” wetu ni mengi kupita kiasi. Ninaposema hatuipendi nchi yetu huwa najaribu kuangalia jinsi gani wengi wetu tunaishi katika “uzalendo” kwa kufanya hasi ya mambo niliyoyataja hapo juu ambayo ni machache tu. Je “uzalendo” wetu ni ushabiki tu usio na maana yoyote? Tunaposema tunaipenda nchi yetu huwa tunamaanisha nini?

Nyerere aliturithisha rushwa? Nyerere aliturithisha uzembe na uvivu, kutowajibika? Hiyo ndio misingi ya taifa letu? Ni wazi kabisa kwamba Hayati Mwalimu Nyerere alijitahidi sana kuhakikisha kwamba uzalendo kwa nchi yetu unakwenda na vitendo. Kama alifanikiwa au alifeli pia jibu lipo miongoni mwetu sisi wenyewe,kila mmoja wetu. Tafakari.

Nimefikia kuandika juu ya “uzalendo” tena kwa sababu naamini huo ndio msingi wa kujenga nchi. Hizi nchi za wenzetu zimejengwa kwa kutumia msingi wa uzalendo. Ukiwa hapa Canada au Marekani unaona kabisa jinsi gani wenzetu wanazipenda nchi zao.Utathibitisha hilo kwa kuangalia jinsi ambavyo wanajitolea pindi wanapohitajika.

Wanaamini kwamba nchi ni yao na wao ndio wa kuijenga au kuibomoa,chaguo ni lao. Kwa bahati mbaya kwetu sisi tunadhani kuwa “mzalendo” ni pale tu unapotamka kwamba unaipenda nchi yako huku vitendo vyako vikithibitisha chuki mbaya uliyonayo.

Najua wengi mtasema “ah Jeff,sisi tunaipenda nchi yetu sana tu,tatizo ni viongozi wetu ndio wanatuangusha” Nitakuuliza,unadhani hizi nchi zilizoendelea huwa zinaongozwa na malaika? Jibu ni hapana,zinaongozwa na watu,tena wengi wao ni wala rushwa kama wetu tu, tofauti ni kwamba wananchi wanatambua kwamba uzalendo ni pamoja na kuhakikisha tunachagua viongozi na sio watawala.

Na isitoshe wanaamini kwamba kiongozi akikosea basi hana budi kuondolewa.Hakuna kulindana kwa sababu kama unamlinda kiongozi mbovu,basi hata wewe huna mapenzi kwa nchi yako. Nchi ni watu na sio viongozi peke yao.

Kwa kumalizia naomba ndugu msomaji,baada ya kumaliza kusoma hii makala,jiulize nini unaifanyia nchi yako ili kuthibitisha “uzalendo” wako? Tuipende nchi yetu kwa vitendo na sio maneno.

jeffmsangi@sympatico.ca 

www.harakati.blogspot.com


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Maneno mazito sana haya Jeff! Hayan=, mwenye masikio na asikie na mwenye macho na aone! Tubadilike, wakati ni huu!! Asante sana.
     
  • Comment #2 (Posted by Kichuguu)
    Rating
    Very good observation. let us do somethiong about it
     
  • Comment #3 (Posted by Mukurya wa Mwita)
    Rating
    Makala hii mbona ni ulalamishi usiotowa suluhisho wajameni!
    Jeff huwa nakusoma kwenye gazeti la tanzania daima,jaribu kupunguza lugha ya kuzunguka na kung'ang'ania point moja.
    Pia unaonekana kama wewe unaipenda Tanzania kuliko wengine mbona umekimbilia huku utumwani na kuiacha Tanzania yako? Rudi nyumbani tuijenge wote na siyo ukimbie mambo yakisha kuwa mazuri kama mafisi yanayotaka tuungane nayo unakimbia nyumbani nyumbani. mie naona huu ni sawa na uanasiasa wa kiccm.

     
  • Comment #4 (Posted by salema emilius)
    Rating
    Nakupongeza sana! naamini hatuna watanzania wengi wenye ufahamu wa maana ya uzalendo.Tumepumbazwa. Hasa wale ambao hawajawahi kutoka Tanzania wakaona wenzetu wanafanya nini basi hubaki kuamini tumeendelea au tumeendelea. Inasikitisha sisi ndiyo tuna wachagua watawala.Tunahitaji viongozi.
     
  • Comment #5 (Posted by maimina binti selumani)
    Rating
    it's such a shame kwa sisi wa bongo kuwa na viongozi waliotoka nje ya ndoa zao ,nawaita wahuni wa jiji kupeleka vimada Bagamoyo halafu mzee mzima kuishia kujishow off kwa kumpika kijana wa wato risasi,kwanza nyie mnaojiita wahuni wa jiji mjifunze jinsi ya kutumia bastola zenu kwenye shughuli zinazohitajika.Kama unavyosema Msangi ndio tutaishia kuwa kama nchi za majirani alimasi nadhahabu kibao lakini mboga za watu ndio nyani mpaka kuishia kupata ebola,watanzania msikubali kuwachagua hawa wahuni wa mjini hawatusaidia kitu chochote bali kutuletea ushamba na kufanya nci za jirani kututawala kwasababu ya mizubayo yetu ,halafu nyie viongozi ni ushamba gani mkiona hao mainvestors mnapagawa lakini sisi vijana twenye akil hamtuangalii hata!
     
  • Comment #6 (Posted by Faru Parutu KamunyuI)
    Rating
    Jeff,
    Makala yako ni nzuri, inasisimua na inajenga misingi imara. Hata hivyo haizungumzii sababu zinazoyeyusha barafu hilo la uzalendo zaidi ya kusema kuwa hata ughaibuni kuna viongozi walarushwa na katika sehemu nyingine unasema wananchi wa nchi hizo huchagua viongozi wazuri kama kipimo cha uzalendo wao. Vipi kuhusu tofauti za kimiundombinu (regional infrastructural disparities) ambayo wamesababisha wakoloni na bado haijatibiwa miaka 45 tangu kupatikana kwa uhuru?Ukipata muda, elimisha kwa kuangalia jamii kwa mrengo Huo.
     
  • Comment #7 (Posted by stephen nyagonde)
    Rating
    Ni wazi muheshimiwa jeff umeuonyesha umati wa watanzania ni jinsi gani tunatakiwa tuwe na uchungu na nchi yetu hali kadharika uwajibikaji na thamani yetu katika nchi hii kwa vizazi vya leo na hata vijavo. mimi naona kauri mbiu iwe "umifanyia nini Tanzania na siyo Tanzania imekufanyia nini" kwa mwenendo huu nafikiri tutapata maendeleo yakinifu kwani wahujumu nchi hama kwa hakika si wazalendo, naamini siku ya mwisho hata kwa mwenyezi mungu wataulizwa!Thats are few from me kaka but kaza buti kumakesure elimu hii inatufikia wausika big up sana!!!1
     
  • Comment #8 (Posted by Freddy Macha)
    Rating
    Miezi miwili mitatu iliyopita. Niko pale BBC London tunasikiliza mahojiano kati ya Mwalimu Nyerere na mwandishi wa habari kutoka Kenya. Mwaka 1963. Nyerere anafafanua maana ya neno mwananchi. Anasema mtu asiyekuwa na taifa lake si mwenye nchi. Mwaka huo Nyerere na wenzake, Kwame Nkrumah na Mfalme Haile Sellasie wameunda Umoja wa Nchi za Kiafrika, OAU. Makala imenikumbusha mahojiano ya Mwalimu. Lugha fasaha, maelezo ya msingi, Kiswahili chepesi, akili. Oyee mtani
     
Submit Comment


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.