Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Lowassa aomba wabunge wasiibue hoja ya umeme
Lowassa aomba wabunge wasiibue hoja ya umeme
By Habari Tanzania | Published  10/31/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Mwandishi Wetu, Gazeti la Mwananchi

WAKATI Bunge linaanza mkutano wake wa tano leo, serikali imewaangukia wabunge wa CCM katika harakati za kujaribu kuwafumba midomo ili kufifisha makali ya mjadala wa hali ya umeme unaobashiriwa kwamba utaibuliwa bungeni.
 
Harakati hizo za serikali zilijibainisha juzi (Jumapili) wakati wa kikao cha Kamati ya wabunge wa CCM kilichofanyika mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
 
Serikali ililazimika kuwaweka sawa wabunge wa CCM kufuatia hisia kuwa suala la hali ya umeme na uhalali wa kampuni ya Richmond Development Corporation (RDC) kupewa zabuni na serikali, linaweza kuibuka ndani ya mkutano unaoanza leo.
 
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zimesema, wabunge wa CCM mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa kuchuja majina 36 ya wana-CCM wanaogombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, waliihoji serikali juu ya wingu zito linalotanda dhidi ya hali ya umeme nchini hususan uhalali wa kampuni ya RDC kupewa zabuni ya kuleta majenereta ya dharura.
 
Wabunge hao waliitaka serikali iwaeleze kinagaubaga juu ya mazingira ya Richmond kupewa mkataba huo na kufafanua juu ya tuhuma kuwa kampuni hiyo inayodai kuwa imesajiliwa Marekani, haitambuliki huko.

Akijibu hoja za wabunge, chanzo cha habari kimesema, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alikwepa kuzungumzia hoja ya Richmond moja kwa moja akidai kuwa yeye ndiyo kwanza ameingia wizarani hapo na hakuwapo wakati mikataba ya kampuni hiyo ikisainiwa.
 
Waziri Karamagi anadaiwa kusema kuwa mara baada ya kuingia wizarani alianza kushughulika hali ya umeme ili kuhakikisha inatengemaa walau ifikapo Desemba upatikanaji wa nishati hiyo urejee katika hali ya kawaida. Hata hivyo, Waziri Karamagi aliwaambia wabunge hao kuwa pamoja na malalamiko yanayoihusu Richmond, kama serikali itavunja mkataba nao, italazimika kubeba hasara kubwa kwa kuwa italazimika kulipa fidia kubwa kwa Richmond.
 
Alisema kwa sasa Richmond bado haijavunja mkataba na wanaendelea na utekelezaji kwa mujibu wa makubaliano. Hata hivyo, majibu hayo ya Karamagi yanaelezwa kuwa hayakuwaridhisha wabunge hao wa CCM ambao walitaka kuelezwa bayana juu ya uhalali wa kampuni ya Richmond kupewa zabuni hiyo na serikali.
 
Kufuatia maswali hayo, Waziri Mkuu Lowassa ilibidi aingilie kati na kumsadia Karamagi na kuwaeleza wabunge kuwa Serikali ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete mwenyewe, inalifuatilia kwa karibu suala la umeme nchini. "Lowasa alisema suala la umeme linamsononesha sana Rais na analifuatilia kwa karibu na kwamba kuna siku Rais aliwahi kumpigia simu saa saba za usiku kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo na waliongea kwa saa nzima," alisema mbunge mmoja wa CCM aliyehudhuria kikao hicho cha juzi.

Inadaiwa kuwa katika ufafanuzi wake, Lowassa aliwaomba wabunge wa CCM kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kutafuta suluhisho la kudumu la hali ya umeme, kauli ambayo inatafsiriwa kuwa ni kuwanyamazisha wabunge hao kuzungumzia hoja hiyo kwa kishindo ndani ya Bunge.
 
"Serikali ilisema inajua kuwa wapinzani wataibua hoja hiyo ndani ya kikao cha Bunge, na hivyo ni muhimu kwa wana CCM kuielewa serikali katika jambo hilo na kuiunga mkono," kilisema chanzo kingine cha habari. Tangu serikali iingie mkataba na kampuni IPTL mwaka 1995 kwa ajili ya kuzalisha umeme na kuiuzia Tanesco, kumekuwako na malalamiko mengi juu ya mikataba ya nishati.
 
Tangu wakati huo, serikali imekuwa ikiahidi kuwa itakuwa makini, lakini tangu kuanza kwa mgawo mkali wa umeme nchini ambao umesababishwa na ukame na hivyo mitambo ya kufua umeme wa maji kushindwa kufanya kazi kutokana na kupungua kwa maji, juhudi kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuingia mkataba wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia.
 
 Miongoni mwa kampuni zilizioingia mkataba na serikali katika siku za hivi karibuni kabisa ni ya Aggreko ambayo tayari imekwisha kuanza kuzalisha megawati 20 za umeme takribani wiki mbili zilizopita huku kampuni nyingine iliyoingia mkataba huo ni Richmond na ilitakiwa iwe imekwisha kuanza kuazalisha umeme huo sasa.

Kutokana na sababu mbalimbali Richmond ndiyo kwanza awamu ya pili ya mitambo yake ya kuzalisha umeme huo iliwasili juzi jijini, baada ya kwanza kuwasili wiki moja iliyopita.
 
Kabla ya kuwasili kwa mitambo ya Richmond, kumekuwapo na taarifa za kutatanisha kuhusu uwezo wa kampuni hiyo, uhalali wake wa kupewa kazi hiyo na kama ni kweli kwamba kampuni hiyo ina makazi yake nchini Marekani.
 
Kuna habari pia kwamba kuhamishwa kwa mawaziri wote wa Nishati na Madini katika mabadiliko yaliyofanywa na Rais hivi karibuni, kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na jinsi suala la umeme lilivyoendeshwa katika mchakato mzima wa kupatikana kwa kampuni za kuzalisha umeme wa dharura kwa kutumia gesi.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by an unknown user)
    Rating
    swala la richmond LINA UTATA MKUBWA tuache kuzunguka mbuyu tuambiane ukweli jamaniii
     
  • Comment #2 (Posted by Born Again Pagan)
    Rating
    Hiyo kampuni ya Richmond Development Corporation ipo. Physical address ni 5825 Schumacher, Houston, Texas 77057. Phone: (713) 952-3472. Fax: (713) 952-0932. Website yao hii: www.rdevco.com. Owners ni Mohamed Gire (mfanya biashara Mhindi wa Kitanzania na Dr. Mohamed Haque (Economist wa Pakistan). Wao ni wakala tu. Hawana wala hawatengenezi hizo turbines! Kutokana na habari za kuaminika, Mohamed Gire ana dada yake huko London na ndugu yake hapo Dar. Nadhani huyo ndugu yake anajua zaidi makubaliano hayo ya kibiashara!

    According to international business transaction, wakala wa namna hii hutafuta mnunuzi anataka nini. Halafu wanatafuta muuza. Mara nyingi hufanya this kind of business transaction kupitia tenders au direct felt-needs za mnunuzi. Mnunuzi (sijui alikuwa Tanesco) anatafuta muuza kupitia wakala (Richmond Development Corporation) wa namna hii. Hukubaliana kupitia benki (kupata a letter of credit) inayohakikisha kuwa mnunuzi ana pesa taslimu kulipia bidhaa. Natumaini enabling bank Tanzania ilikuwa ile ya CRDB Bank Ltd. ambayo pengine haikutaka kudhamini transaction hii. Pengine walitaka Wizara ya Fedha ndiyo idhamini kwani sijui kama Tanesco walikuwa wana haja ya huo umeme ziada. Wakala humtaarifu muuzaji kuwa kuna pesa hizo katika benki, na bidhaa kupelekwa kwa mnunuzi.

    Wakati mwingine wakala hukubaliana na mnunuzi wa umma to inflate bei, hata kama bei ya mwuzaji ni chini, au hununua vyombo (majenereta) vikuu kuu na kujidai kuwa ni vipya ), kama yalivyokuwa madege ya abiria tuliyonunua miak ya 1979/80! Mwuzaji kazi yake ni kwenda benki kupewa pesa zake. The difference inakuwa ni mali ya wakala, licha ya commission yake. Mara nyingi fedha za umma zimeibiwa kwa njia hii kati ya mawakala na wawakilishi wanaotia saini kwa niaba ya serikali au shirika la umma!

    Ukifungua and search engine juu ya Mohamed Gire na rafiki yake huyo wa Kipakistani, utaweza kupata mengi zaidi, ikiwa ni pamoja na kuhamia Houston kutoka Chicago kwa Gire na michango yake ya kutunisha kampeni za Democratic Party (political campaigns contributions).

    Ubalozi wetu hapa Washington, DC, unajua zaidi kuhusu huyo Mohamed Gire. Soma taarifa ya habari zilizopokelwa na kuandikwa na ippmedia.com:

    Tanzania Ambassador to US takes-on new foreign policy

    2003-08-19 10:21:22
    By Guardian Reporter
    Tanzania Ambassador to the United States Andrew Daraja took the country?s new foreign policy that focuses on economic considerations to heart when he recently visited the US city of Houston, Texas.
    While there, he met with US investors wishing to do business in Tanzania and also lobbied Houston?s Mayor, Lee P. Brown, for continued involvement in the country.
    The new foreign policy announced recently by Minister of Foreign Affairs and International Co-operation Jakaya Kikwete in the just ended Bunge session stresses economic interests instead of political considerations. The minister has urged all Tanzania missions abroad to focus on advancing the country?s commercial relationships.
    In a gala hosted to welcome him to Houston, Daraja thanked the Mayor and the Richmond Development Corporation CEO, Mohammed Gire, for their efforts in creating strong Tanzanian- Houston partnership, emphasising the need for continued collaboration in technology, agriculture, education, health care and cultural exchanges.
    According to the American Embassy spokesperson, Mayor Brown awarded Daraja honorary Citizenship of Houston, while urging him to open a Tanzanian consulate there.
    At the same time, Daraja met with the president of Absolute Adventure Travel, Graham Farebrother, a Houston-based tour operator. The tour operator is recipient of the 2003 Tanzania Tourism Board Award for sending more tourists to Tanzania?s Southern Circuit than any other operator.
    Gire, the Richmond Development Corporation CEO, is a Tanzanian-American. He arranged the Ambassador?s visit to Houston and will be accompanying the mayor on a forthcoming tour of Africa.
    Richmond Development Corporation is an international infrastructure development company working in Tanzania on several large infrastructure projects including the oil and gas sector.
    Accompanying Daraja on his trip to Houston was Chief of Chancellery, Alex Massinda.
    In an appearance before the Bunge?s committee on foreign Affairs on July 29, US Ambassador Robert V. Royall commended Tanzania for its new ?economic diplomacy.?
    The diplomat added: ?The liberation diplomacy of the past, when alliances with socialist nations were paramount and so-called Third World Solidarity dominated foreign policy, must give way to a more realistic approach to dealing with your true friends - those who are working to lift you into the 21st century where poverty is not acceptable and disease must be conquered.? (ENDS).

     
  • Comment #3 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Tunahitaji watu mabao wako well-informed kama Born Again Pagan kujenga hoja zenye maana. Keep it up! Unajua kuna wengine wanaibuka tu na kuanza kupiga kelele zisizokuwa na maana almradi tu wamedika na kuonekana wameponda mtu/watu fulani.
    Lets be more constructive on our discussions. Do some reseacrh and then you have a right to speak. Thanks Born Again Pagan.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.