Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Umeme wa Richmond sasa baada ya wiki 3
Umeme wa Richmond sasa baada ya wiki 3
By Habari Tanzania | Published  10/31/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
.Mitambo zaidi yawasili
Na Furaha Omary, Gazeti la Uhuru
 
KATIKA juhudi za serikali kukabiliana na makali ya mgawo wa umeme, mitambo mingine miwili ya kuzalisha megawati 20 iliwasili juzi usiku na ilianza kufungwa jana katika kituo cha Tanesco, Ubungo, Dar es Salaam.
 
Umeme kutoka mitambo hiyo, iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ya Marekani, unatarajiwa kuanza kuzalishwa katika kipindi cha wiki tatu zijazo.
 
Mratibu wa mradi huo, Simon Jirima, alitoa maelezo hayo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere wakati mitambo ikipakuliwa kutoka ndege ya mizigo ya Antonov 225, inayosemekana ni kubwa kuliko zote duniani, ikiwa na uwezo wa kubeba tani 600, ikitokea nchini Marekani.
 
Alisema mitambo mingine ya kuzalisha jumla ya megawati 80 itawasili kwa meli kwa kuwa ni mikubwa na haiwezi kusafirishwa kwa ndege.
 
Richmond waliingia mkataba na serikali wa kuleta mitambo ya kutoa megawati 100. Makubaliano yalikuwa mitambo ya kuzalisha megawati 20 iletwe haraka kwa ndege ili kupunguza makali ya mgawo wa umeme.
 
Wiki moja ilyopita wakati sehemu ya kwanza ya mashine za mitambo hiyo zilipoletwa, meneja wa kampuni hiyo, Naeem Gire, alisema mashine hizo zilizowasili ni miongoni mwa nne ambazo zitakamilisha mtambo wa kuzalisha umeme utakaotoa megawati 22.8 za umeme.
 
“Mashine hizi ni utangulizi wa mashine nne ambazo zikiungana zitakamilisha mtambo utakaotoa umeme wa megawati 22.8, lakini kulingana na hali ya joto hapa nchini, Tanesco itaamua kama izalishe megawati kati ya 20 na 21,” alisema
 
Alisema haitawezekana kuzalisha megawati zote 22.8 kutokana na joto la Dar es Salaam kuwa kali.
 
Mitambo ya Richmond, ambayo ni ya kukodi kwa mkataba wa miaka miwili, itagharimu sh. bilioni 172, na ni moja ya miradi ya dharura ya umeme wa megawati 240, ilinayolengwa kuwekwa Ubungo, Dar es Salaam. Miradi mingine inatekelezwa na kampuni ya Aggreko.
 
Naeem Gire alisema tayari kuna watalamu wao wa kuendesha mitambo hiyo na endapo kutatokea matatizo yatakayowapa shida kuyamudu watawaagizwa kutoka nje.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by limboa shabani)
    Rating
    it seems she is doing very well in writting the articles.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.