Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Idd Simba aliweka pamba masikio-Mzindakaya
Idd Simba aliweka pamba masikio-Mzindakaya
By Juma Pinto | Published  10/30/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Asema viongozi wengi hawapendi kusoma, Asema wanaozomea wabunge ni wahuni

MBUNGE wa Kwela (CCM), Chrisant Mzindakaya amesema aliamua kutoa bomu la kashfa ya sukari mwaka 2001 kufuatia aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Idd Simba kuweka pamba masikioni.

Mh: Mzindakaya ambaye aliongoza ujumbe wa wabunge wenzake nane waliofanya ziara ya kutembelea bunge la Uingereza ‘House of Commons na lile la Scotiland ‘House of Lords, aliyesema hayo katika mahojiano maalum na kipindi cha TV cha Tanzania Vision kinachorusha hapa Uingereza katika chaneli ya Sky 183 na kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi.

Mbali na Mzindakaya ambaye ni mkuu wa msafara, wabunge wengine waliomo kwenye msafara huo ni Khalifa .S.Khalifa, Shally Raymond, John Shibuda, William Ngeleja, Amina Chifupa Mkapakanjia, Aziza Ally, Chacha Wangwe na Katibu wa msafara, Justina Shauri.

Mbunge huyo mkongwe wa bonge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanja anafikisha miaka 40 la kuliongoza bunge hilo mwishoni mwa mwezi ujao, alisema aliamua kuweka mambo hadharani ya kashfa ya sukari kufuatia Waziri aliyehusika kutokubali makosa.

Mbali na kuwa mbunge kwa miaka 40, Mzindakaya amewahi kuwa mkuu wa mkoa kwa miaka 13 na naibu waziri wa miaka 9, alisema mara nyingi makosa makubwa yanafanywa kwa wale waliopewa nafasi ya kukosoa na siyo kwa wale wanaosolewa.

Alisema mtu yoyote mwenye heshma na anayejua anachofanya, hatasika kusema ukweli wa jambo ambalo ana uhakika nalo na analolifahamu na wale wanaohusika japo watanuna kwa kusema ukweli basi itakuwa kwa muda tu.

“Mara nyingi mimi nilivyojifunza kwa Tanzania demokrasi ni kubwa na nimeona kwa Marais wote watatu hadi wa sasa Jakaya Kikwete, anatafuta watu wa kumsaida kwa kukosoa mambo, lakini kwa njia ya kusaidia kujenga na siyo kubomoa kwa maan ya majungu” alisema Mh: Mzindakaya.

Mbunge huyo wa Kwela aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa kuibua kashfa hiyo ya sukari mwaka 2001 alisema kuna kuibua makosa makubwa ya kiutendaji katika serikali na mimi naamini kabisa, mbunge yoyote au mwananchi akiwa na ushahidi wa jambo na kuliibua basi nchi na Rais atamshukuru.

Alisema anapotaka kuibua jambo, kwanza lazima ailifanyie utafiti, lakini pia kabla ya kufanya lolote na muhisika aanapaswa kuambiwa kwamba hili jambo linavyofanyika sivyo, lakini itatokea anayehusika kushindwa kuelewa na kuleta ubishi ndipo suala litakapotoka hadharani.

Mh: Mzindakayaka alisema katika suala hilo, kama Waziri wa Vianda na Biashara aliyehusika kipindi kile angeelewa, lile jambo lisingetoka hadharani, kwani kabla ya kutolewa kashfa ile hadharani Waziri aliandikiwa barua, ameambiwa, lakini aliendelea na msimamo wake wa kushikilia kosa lake.

Aliendelea kusema jambo kubwa ni kukosoana na kurekebishana ndani kabla ya kutoa jambo hadharani tena ikitilia maanani wote wa chama kimoja , lakini kufikiwa kwa hatua hiyo ilitokana na muhusika (Waziri) kutokuwa na masikio.

“Unamwambia muhusika, hivi sivyo lakini ingekuwa hivyi ndivyo, lakini yeye anashikilia na msimamo wake, basi ndipo unapoamua kuweka mambo hadharani ili umma uweze kuelewa,” alisema Mh: Mzindakaya.

Sakata hilo la sukari likaingia bungeni, Mzindakaya akaja na hoja binafsi dhidi ya Simba. Akatoa taarifa kuhusu kile alichokiona kuwa ni kashfa kwa waziri huyo, serikali na hata Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akaweka shinikizo la kutaka Simba, kwanza ajiuzulu nafasi yake ya uwaziri na pili aliombe radhi bunge kwa kulidanganya wakati alipokuwa akiwasilisha makadirio na matumizi ya wizara yake pale alipolitafuna tafuna suala zima kuhusu sakata hiyo ya sukari.

Awali Simba alilieleza bunge bayana kwamba hata jiuzulu kwani haoni kutenda kosa lolote. Kauli yake hiyo haikuweza kumuokoa na wala haikuweza kukiokoa chama chake. Upinzani mkali ukaendelea toka ndani ya CCM na nje wakimtaka ajiuzulu.

Miezi mitatu baada ya kuendelea kwa mashinikizo, hatimaye Simba akaamua kujiuzulu uwaziri, akisema bayana kwamba amelazimika kuchukua uamuzi huo kwa ajili ya kuinusuru serikali yake kusambaratika na chama chake kustawi.

Kiongozi huyo wa msafara wa wabunge waliokaa hapa Uingereza kwa wiki moja na wamerejea Tanzania jana (Jumatatu), aliyasema hayo kufuatia swali aliloulizwa kwa nini suala hilo halikuzungumzwa ndani ya vikao vya bunge kabla ya kulitoa nje kwa kuwa iliyokoselewa ni wizara ya Serikali ambayo inaongozwa na CCM na yeye (Mzindakaya) ni mwanachama wake.

Katika ziara ya wabunge hao ni ziara ambazo spika wa bunge la Tanzania, Mh Samuel Sitta ameamua kizifanya kwa lengo la wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea mabunge mbalimbali dunia kujifunza jinsi wenzao wanavyoweza kuendesha mabunge yao.

Akizungumzia tofauti iliyopo sasa na ile ya miaka 40 iliyopita ndani ya bunge la bunge la Tanzania, Mh.Mzindakaya alisema kipindi cha sasa wasomi ni wengi na kiwango cha uelewa kimeongozeka kwa kiasi kikubwa, hali inayofanya wao wazee kuzidi kujifunza na kujiendeleza ili kwenda na wakati.

“Watanzania hatupenda kujiendeleza kwa kusoma na hili mtu akishapa digrii yake na cheo, basi hawapendi kujiendeleza tena wanaona ndio wamemaliza na hii ndio kasoro kubwa sana,” alisema

Alisema hata baadhi ya viongozi ya viongozi Serikali, wamekuwa na kasumba hiyo, lakini pamoja na uzee aliokuwa nao bado anapenda kusoma na kujifunza na hata akisafiri amekuwa akinunua vitabu vya kusoma na kujifunza, lakini wengine watarudi na masanduku matatu ya nguo.

Mkongwe huyo alisema mtu mwenye kuhitaji maendeleo na kujua mambo yanavyokwenda kwa wakati katika dunia ya sasa ni lazima asome, kwani dunia ya sasa inahitaji wasomi ili kuweza kujua mambo mengi, bila kusoma hakuna jipya utakaloweza kujua.

Kuhusu suala la wafanyabishara mbalimbali na watu wenye uwezo kifedha Tanzania kuingia katika ulingo wa siasa na hasa katika nafasi za ubunge, Mzindakaya alisema wao ndani ya CCM wameliona hili na wanalifanyia kazi.

“Mh Rais ameliona hili, hivyo katika vikao vyetu vya ndani ya chama tunajitahidi kuangalia utaratibu mzuri wa kupata wabunge ili kuondokana na hali hiyo ya watu kutumia fedha kupata cheo,” alisema Mzindakaya.

Akizungumzia tabia ya baadhi ya wananchi kuzomea wabunge wao, pindi wanapotambulishwa kwa Rais au Waziri Mkuu katika mikutano ya hadhara kwenye majimbo yao,Mh.Mzindakaya alisema kuzomea kiongozi siyo tabia ya Watanzania ni mambo ya kihuni.

Alisema hatua hiyo ilikuwa ikitokea mwaka jana, kufuatia makundi mbalimbali ya kampeni kupandikiza baadhi ya watu na hiyo inawezekana wanaofanya mambo hayo ni wanachama wenzao kutoka ndani ya CCM.

Mbunge huyo mkongwe alisema tatizo lingine linalosababisha hatua hiyo ni kura za maoni inayofanywa ndani ya chama, ambapo mgombea aliyeshindwa kwenye kura hizo anakuwa na kundi lake lililokuwa liko nae pamaoja, hivyo kutoa madukuduku yao moyoni kwa kuzomea katika mikutano ya hadhara.

“Ni kazi ya chama kuhakikisha kwamba tunarudisha umoja na kuvunja makundi mara baada ya kura za maoni, kwa kufanya hivyo ndiko kutakaweza kuleta umoja na ushirikiano mzuri na siyo kubakisha makundi na kuanza kuzomea, hali ambayo si utamaduni wetu Watanzania,” alisema.

Kuhusu mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni kwa Mawaziri kuhamishwa wizara zao, Mh: Mzindakaya alisema Rais Kikwete ametumia busara kubwa sana kwa mawaziri wahusika kuhamishwa kutoka wizara moja kwenda nyingine .

“Ni jukumu la waziri aliyehamishwa kutoka wizara moja kwenda nyingine kujiuliza kwa nini amehamishwa katika wizara yake na kujiuliza kama amepelekwa pale kwa mazuri au kwa kupewa onyo la kazi,”

Alisema yawezekana Mh: Rais ametoa uhamishwa huo kwa kuona furani nikimpeleka wizara furani anaweza kuwa muhimu zaidi kuliko pale alipokuwa mwanzo na mwingine anaweza kupelekwa wizara nyingine kwa onyo tu, nyote vinawezekana.

“ Rais hafanyi kosa kumpa mtu madaraka, anayekosa ni yule aliyepewa jukumu na kushindwa kutekeza majukumu yake, hivyo kwa Mh Rais kufanya mabadiliko ni vitu vya kawadia katika kutafuta ufanisi wa shughuli za Serikali.

Kuhusu mafanikio ya ziara yao katika mabunge hayo, Mzindakaya alisema wamejifunza mengi sana na kubwa zaidi waliloliona kwamba mabunge ya wenzetu demokrasia yao imeshika hatamu kubwazaidi, tofauti na bunge letu ambapo kuna heshma kidogo.

“Hapa tumeona Waziri Mkuu anajibu swali na watu wanaingilia hutuba yake, sasa kwetu hatujafikia hatua hiyo kwani bado tuha heshma kubwa, lakini yote kuna mambo mengine sana tumejifunza na tutayapeleka kwa wenzetu,” alisema Mzindakaya.

Alisema mtu kusoma si kukaa darasani tu, lakini hata hizi safari ambazo wabunge sasa wameanza kwenda kutembelea sehemu mbalimbali duniani ni somo tosha, hivyo tumejifunza mengi na tunatarajia kuwapelekea wenzetu kile ambacho tumenufaika nacho na kukifanyia kazi.

Kuhusu matarajio yake baada ya miaka mitano itajayo, iwapo atagombea tena ubenge katika jimbo lake, Mh: Mzindakaya alisema atatoa msimamo wake muda ukifika kwani ana mawazo yake ambayo anayafikilia.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by mohd case)
    Rating
    cheki sasa mtu kama huyu amekaa kwenye ubunge na ungozi serikalin zaid ya miaka 40 hadi watu wanamzomea akiongea lakini bado tu anaropokwa ujinga na kumtetea huyu mcheza msondo aliyebadilika kuwa rais na kipenzi cha waandish wa habari na vijana illiterate na wazee wa maskan wa kahawa sijui kikwete au kiwete,sisi wabongo hatuwezi kuendelea hadi hii type ya viongozi kama hawa mabogus na machangudoa kina amina chifupa basi hatutaendelea kamwe tutabaki wadanganyika tu na mali zetu na ardhi yetu kuporwa na hawa majirani zetu wanaotraka tuungane nao,na viongozi wanabaki kushindana tu kwenda kushangaaa ulaya na america jinsi wanavyoendelea zaidi na wakirudi wanadanganya hao wadanganyika wenzao walioksa kusoma na wazee wa maskan.
     
Submit Comment


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.