Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Waziri akataa wananchi kushawishiwa kuhusu Shirikisho
http://www.habaritanzania.com/articles/1601/1/Waziri-akataa-wananchi-kushawishiwa-kuhusu-Shirikisho
By Ramadhan Semtawa
Published on 10/30/2006
 
NAIBU Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodarus Kamala amekemea baadhi ya watu kutoka nje ya nchi ambao wanafanya ushawishi wa kutaka kuwaamulia watanzania kuingia katika shirikisho la Afrika Mashariki.


Na Ramadhan Semtawa

NAIBU Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodarus Kamala amekemea baadhi ya watu kutoka nje ya nchi ambao wanafanya ushawishi wa kutaka kuwaamulia watanzania kuingia katika shirikisho la Afrika Mashariki.

Hatua hiyo ya Naibu waziri huyo imekuja jana baada ya kubainika kuwa baadhi ya wanasiasa wa nchi za Kenya na Uganda na vyombo vya habari kuwashawishi watanzania wakubali kujiunga na shirikisho bila ya kufuata taratibu.Alisema hakuna nchi ambayo inapaswa kuifundisha nyingine kuhusu nini cha kufanya katika kuelekea shirikisho.

"Kila nchi haitakiwi kuingiliwa, hatutarajii hilo, ndiyo maana kila nchi ina kamati yake ya kukusanya maoni," alisema.

Dk. Kamala alisema Watanzania wanajua kipi kizuri, wana akili timamu na kwamba hawataki kufundishwa ndiyo maana kila nchi imekuwa na kamati yake ya kusimamia uchukuaji maoni.

Hadi sasa nchi za Kenya na Uganda kwa sehemu kubwa zimekuwa zikitaka utekelezaji wa mpango kasi (Fast Trucking) kuelekea shirikisho huku Tanzania ikionekana haijawa na msimamo.Mwananchi imebaini kwamba, hatua ya Tanzania kutokuwa na msimamo inatokana na kuwepo makundi mawili yenye mitazamo na maslahi tofuati katika dhana nzima ya kuelekea shirikisho.Mgawanyiko huu umefika hadi katika baraza la mawaziri ambapo baadhi ya mawaziri wameonyesha wazi wazi nia yao ya kulitaka shirikisho huku wengine wakipinga.

Kundi la mawaziri linalounga mkono mpango wa kuwapo kasi ya kufikia shirikisho linaeleza kuwa Tanzania itanufaika zaidi kuliko Kenya na Uganda kutokana na utajiri ilionao wa madini na rasmali nyingine."Tanzania haipaswi kuwa na hofu kuhusu kuiunga na shirikisho kutokana na kuwa na nafasi kubwa ya kunufaika, kuliko Kenya na Uganda, ni heri Uganda ndio ambao wangehofu kwa sababu hawana bandari," alisema mmoja wa mawaziri.

Hata hivyo, Mwananchi imebaini kwamba, baadhi ya mawaziri majina (tunayo) wameliambia gazeti hili kwamba wasingependa kuona Tanzania inaingia katika shirikisho na Kenya.Mawaziri hao walisema hata ndani ya vikao vya baraza la mawaziri kumekuwa na mitizamo tofauti kuhusu mpango huo."Nani aungane na Kenya wewe, kitu hicho sijui kama kitakuwepo, watu wenyewe wanapigana hata bungeni,"alisema waziri huyo.Waziri mwingine ambaye sasa amebadilishwa kutoka katika wizara ya awali kwenda nyingine, alisema kumekuwa na upotoshaji kwamba shirikisho lazima liwepo.

"Hakuna shirikisho ambalo ni la lazima au lililowekwa na wanasiasa, sisi ndiyo tuko katika baraza na tunashiriki vikao, hilo limekuwa likipotoshwa na baadhi ya wenzetu", alisisitiza waziri huyo.Jumuiya na Taasisi za kiislamu nchini imetoa msimamo wake kuhusu shirikisho kwa kusema kwamba itafanya utafiti kabla ya kuruhusu Waislamu kutoa maoni kwani hawana ufahamu na suala zima la jumuiya.Baadhi ya wanasiasa wa Kenya na Uganda wakiwemo wabunge wameamua kujitokeza hadharani kuwashawishi watanzania wasiogope kujiunga na shirikisho.

Juhudi za kumpata Waziri wa Afrika Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Ibrahim