Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mfanyabiashara Dar ajiua kwa kujipiga risasi
Mfanyabiashara Dar ajiua kwa kujipiga risasi
By Habari Tanzania | Published  05/30/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi Wetu
 
MFANYABIASHARA amejiua kwa kujipiga risasi akiwa chumbani nyumbani kwake mjini Dar es Salaam.
 
Sambamba na tukio hilo, polisi inawashikilia wafanyakazi watano wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security Limited, kwa tuhuma za wizi wa vitu mbalimbali ikiwemo simu ya mkononi wakati walipokuwa wakizima moto.
 
Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana aliwaambia waandishi wa habari jana na kumtaja mfanyabiashara aliyejiua kuwa ni Simon Alphan (47), mkazi wa Sinza, Dar es Salaam.
 
Kuhusu tukio la mfanyabiashara aliyejiua, Tibaigana alisema lilitokea juzi saa saba mchana, baada ya mkewe Hawa Fadhili kusikia mlio wa bunduki.
 
Akimnukuu Hawa, Tibaigana alisema mama huyo alisikia mlio wa bunduki hiyo wakati akiwa sebuleni akila chakula cha mchana.
 
Tibaigana alisena baada ya mlio huo, Hawa aliingia chumbani alikokuwa mumewe na kumkuta akiwa tayari amejipiga risasi kichwani na huku akiwa ameshikilia bastola mkononi.
 
Kamishna Tibaigana alisema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana, ingawa marehemu alikutwa akiwa na ujumbe uliosomeka: “Nimeamua kujiua kutokana na matatizo ya kifamilia, hivyo familia yangu isisumbuliwe na mtu yeyote.”
 
Kuhusu tukio la uporaji, Tibaigana aliwataja wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ulinzi Kitengo cha Zima Moto wanaowashikilia kuwa ni Nicholaus Mwenye (25), Batrea Mwitula (31), Munila Donald (23), Adam Stambuli (31) na Hassan Marwa (30).
 
Kwa mujibu wa Tibaigana, wafanyakazi hao walikamatwa baada ya wakazi wa jengo lililoungua moto lililoko Garden Avenue, kulalamika wakidai kwamba wamehusika na uporaji wa vitu mbalimbali kutoka katika nyumba iliyokuwa ikiungua.
 
Tibaigana alisema kufuatia malalamiko hayo ya majirani, upekuzi ulifanywa na simu aina ya Nokia 6610, kupatikana ikiwa imefichwa katika moja ya buti ya lori la zimamoto lenye namba za usajili T 414 ACQ aina ya DENNIS. Simu hiyo ni mali ya Prosovia Temu ambaye ni mmoja wa wakazi wa jengo hilo linalomilikiwa na Wizara ya Miundombinu zamani Ujenzi.
 
Nyumba hiyo namba tano inayomilikiwa na Godbless Urono (48), iliungua juzi saa 2:45 asubuhi kutokana na hitilafu ya umeme iliyoanzia katika jokofu. Mali mbalimbali zikiwemo samani ziliteketea kwa moto.
 
Hata hivyo, alisema hakuna madhara yoyote kwa binadamu ukiacha mke wa Urono, Jane (40) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu kutokana na kupatwa na shinikizo la damu.
 
Pia, watoto watatu wa Urono walitibiwa katika hospitali hiyo na kuruhusiwa kurejea nyumbani.
 
Akizungumzia tukio hilo jana mchana, Meneja Mkuu wa Ultimate Limited, Martin Perks, alikiri kushikiliwa kwa wafanyakazi wake na kusema kwamba mbali ya simu hakuna vitu vya thamani vilivyoporwa.
 
Hata hivyo, alisema wafanyakazi wake walijitahidi kuokoa maisha ya wakazi hao na kwamba suala la wizi anaiachia polisi.
 
Wakati huo huo, mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Habiba mwenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 25, alikufa ghafla juzi muda mfupi baada ya kufika kwa ‘mama ntilie mmoja’ na kukaa kwenye ‘benchi’ kwa lengo la kujipumzisha kabla ya kuendelea na safari yake.
 
Akimunukuu ‘mama ntilie’, Halima Fadhili (19), ambaye huendesha shughuli zake katika maeneo ya Kigamboni, Tibaigana alisema alisema Habiba ambaye ni mkazi wa Manzese Midizini, alikutwa na umauti huo baada ya kudondoka ghafla na kupoteza fahamu akiwa amekaa kwenye ‘benchi’ hilo.
 
Kwa mujibu wa Halima, marehemu alikuwa akielekea eneo la Kigamboni kwa ajili ya kuwatembelea ndugu zake.
 
Kutoka gazeti la Uhuru

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.