Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wakazi Mbezi Luis waingiwa hofu
Wakazi Mbezi Luis waingiwa hofu
By Habari Tanzania | Published  10/30/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Charles Mullinda

WAKAZI wa Mbezi Luis Mshikamano, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wamekumbwa na hofu kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu.

Baadhi ya wakazi hao waliozungumza na Tanzania Daima, hivi karibuni, walisema mfululizo wa vitendo vya uhalifu, kujeruhiwa na kuporwa mali kunawafanya waishi kwa hofu.

Wiki iliyopita, walifanya mkutano wa kuweka mikakati ya kujilinda na baadaye walifanya maandamano hadi kituo cha polisi cha Mbezi ili kufikisha kilio kwa askari wa kituo hicho.

Mwenyekiti wa kikao hicho, Rymos Maruchu, alisema kutokana na hali mbaya ya kiusalama, wananchi wanapaswa kujipanga kujilinda wenyewe.

Alisema iwapo watajitolea kuendesha ulinzi na jeshi la polisi kushirikiana na wananchi hali hiyo inaweza kubadilika.

“Wote mnakumbuka tukio la kutisha la hivi karibuni la kuuawa kwa Gines Silayo (32) kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa majambazi akiwa na jirani zake wanne.

“Walivamiwa na majambazi wakiwa kwenye baa ya Nova iliyopo eneo hili na kujeruhiwa kwa kupigwa nondo, wakaporwa pesa ndogo za matumizi walizokuwa nazo na simu za mkononi.

“Ili tuepukane na matukio kama haya, ni lazima tuanze kujilinda wenyewe,” alisema Maruchu.

Alisema katika kipindi cha miezi mitano, baa tatu zimevamiwa na wateja kuporwa mali na kujeruhiwa kwa vipigo, na kwamba matukio hayo yanatokea kati ya saa mbili na saa tatu na nusu usiku.

Reginald Msengi, ambaye alikuwa katibu wa kikao hicho alisema kuwa, maeneo hayo yamepanuka kutokana na ujenzi, hivyo ili kuimarisha ulinzi kwenye eneo hilo wananchi wenyewe wanatakiwa kujitolea.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.