Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Lowassa Kaimu Rais
Lowassa Kaimu Rais
By Habari Tanzania | Published  10/30/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Shabani Matutu

WAZIRI Mkuu, Edward Lowassa anakaimu nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kazi hiyo ameianza jana baada ya Rais Jakaya Kikwete kuanza ziara ndefu kwenye nchi za China, Japan, Korea Kusini na Falme za Kiarabu (UAE).

Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, nae ameondoka nchini jana kuelekea mjini Roma, Italia, kwa ziara ya siku tisa kuhudhuria kikao cha 32 cha Kamati ya Hifadhi ya Chakula, anakomwakilisha Rais Kikwete.

Rais Kikwete atakuwa na mazungumzo na wakuu wa nchi hizo na anatarajia kuanza ziara yake nchini Japan kwa ajili ya kuishirikisha nchi hiyo katika mambo ya miundombinu.

Katika ziara yake, Rais Kikwete ameambatana na mkewe, mama Salma Kikwete; Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar anayehusika na fedha na uchumi Dk. Mwinihaji Makame; Naibu Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo na Mbunge wa Muhambwe, Felix Kijiko (CCM).


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.