Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wamachinga wanaouza viwanja kukiona
Wamachinga wanaouza viwanja kukiona
By Habari Tanzania | Published  10/30/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Prisca Nsemwa

HATUA kali za kisheria zitachukuliwa na serikali kwa wamachinga watakaouza viwanja kwa wenzao, ambavyo serikali imevitoa bure ili waweze kufanyia biashara.

Taarifa hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Lucy Semindu.

Alisema kumezuka tabia kwa baadhi ya wamachinga, hasa kwenye maeneo ya Kibasila na Kigogo Sambusa, ambako walioshika viwanja huwauzia wenzao kwa bei ya juu kinyume cha utaratibu.

“Viwanja wamepewa bure na serikali, machinga atakayebainika anamuuzia mwenzake kiwanja ambacho yeye amepewa bure na serikali, hatua kali zitachukuliwa,” alisema Semindu.

Hivi karibuni, serikali mkoani Dar es Salaam iliwahamisha wamachinga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kisheria na kuwapeleka kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.