Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kampuni ya utalii yadaiwa kuajiri Wakenya kienyeji
Kampuni ya utalii yadaiwa kuajiri Wakenya kienyeji
By Habari Tanzania | Published  10/29/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Claud Gwandu, Arusha

KAMPUNI moja ya utalii ya mjini hapa inadaiwa kuwaingiza nchini waongoza utalii zaidi ya 10 kutoka Kenya wanaofanya kazi za kuongoza utalii huku Watanzania watano wenye sifa wakiachwa bila kazi.

Rais hao wa Kenya hao, tayari wamepewa hati ya kuishi nchini ya daraja B na inasemekana wameruhusiwa kufanya kazi za kuongoza utalii katika mikoa ya Arusha,Manyara na Mara.Hati hizo zimetolewa na Idara ya uhamiaji Makao Makuu.

Kwa mujibu wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TTGA), Wakenya hao ambao wapo katika mbuga mbalimbali za wanyama nchini wamekuwa nchini kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu wakifanya kazi hizo.

TTGA imewataja Wakenya hao (majina tunayo) ambao nyaraka za mikataba ya ajira zao kampuni wanayofanya kazi (jina tunalo) kuwa wameruhusiwa kihalali.

Alipoulizwa kwa simu kuhusu kuwapo kwa Wakenya hao, mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo alikana kuwa si kweli na kwamba taarifa hizo zinasambazwa na wabaya wake wanaotaka kulipaka matope jina la kampuni yake.

“Hayo si maneno ya kweli, hakuna Wakenya na kama una majina kama unavyodai basi nitumie kwa njia ya fax, lakini mimi sina taarifa za kuwapo kwa watu kama hao,”Alisema mkurugenzi huyo katika mazungumzo hayo kwa njia ya simu.

Alipoulizwa kuhusu Watanzania watano ambao wanadaiwa kuwa na shahada za masuala ya utalii, lakini hawapewi kazi hiyo na badala yake wanapewa Wakenya, mkurugenzi huyo alisema kuwa hakuwa na taarifa yoyote juu ya suala hilo.

Hata hivyo, alipobanwa juu ya kutaka majina ya Wakenya hao wakati anasema hawapo, mkurugenzi huyo hakuwa na la kusema .

Tatizo la kuingia nchini kwa waongoza utalii kutoka nje na kufanya kazi za kuongoza utalii nchini,limekuwa likilalamikiwa na waongoza utalii wazalendo ambao wamekuwa wakidai kuwa wanakosa kazi za kufanya kutokana na nafasi zao kushikwa na wageni.

Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha, Julai mwaka huu kupitia kwa mkuu wa idara hiyo mkoani humo,Justine Kabigumila ilitoa mwongozo kwa wageni kupata vibali vya kuongoza utalii, lakini miezi mitatu baadaye ikafuta mwongozo huo.

Kabigumila amekuwa akidai kuwa amechukua hatua hiyo kutokana na maagizo kutoka kwa wakubwa wake wa kazi na kila anapofuatwa anadai kuwa anasubiri maelekezo mengine kutoka kwa wakubwa wake walioko makao makuu.

Ingawa kuna makampuni zaidi ya 300 ya utalii mjini hapa,lakini yake yanayomilikiwa na Watanzania wenye asili ya Asia yamekuwa yakituhumiwa kuwatumia waongoza utalii kutoka Kenya na kuwaacha wazawa bila kazi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Peter)
    Rating
    This is a Xenophobic article not doing much to the regional (EAC) spirit. Will Tz survive alone in the region in future?
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.