Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mengi ni rafiki wa Waislamu Sheikh Khalifa
Mengi ni rafiki wa Waislamu Sheikh Khalifa
By Habari Tanzania | Published  05/29/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Kamati ya Maimamu ya Kuokoa Mali za Waislamu Nchini, imesema Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Bw. Reginald Mengi si adui wa Waislamu bali rafiki anayetoa mchango mkubwa katika kueneza dini hiyo.

Msimamo huo ulitolewa jana na Katibu wa Kamati ya Kuokoa Mali za Waislamu nchini, Sheikh Khalifa Khamis wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Khamis alitoa msimamo huo jana kufuatia matamshi ya Sheikh Ali Basaleh aliyoyatoa Mei 19, mwaka huu katika msikiti wa Idrissa Jijini Dar es Salaam kwamba Bw. Mengi amekuwa akitumia vyombo vya habari kuupiga vita Uislamu.

’Kamati yetu inatamka kuwa Mengi ni rafiki wa Waislamu na anatoa mchango mkubwa katika kueneza Uislamu na si kuupiga vita’ alisema.

Hata hivyo, Kamati hiyo imemtaka mwislamu yeyote anayefahamu mbinu zinazotumiwa na Bw. Mengi kuupiga vita Uislamu awapelekee ushahidi huo ili waufanyie kazi.

Alisema” lakini tunalaani majungu, chuki na fitina.

Alisema Kamati haina maelezo yanayothibitisha jinsi Bw. Mengi anavyoupiga vita Uislamu bali wanao ushahidi unaothibitisha anavyosadia maendeleo ya Waislamu.

Kuhusu kumsomea Bw. Mengi dua ya ahla badri, Sheikh Khamis alisema Kamati yake imewataka Waislamu wote nchini kuwapuuza watu hao kwani hawajui wasemalo.

Alisema kitendo cha kutishia kumsomea Bw. Mengi ahla badri ni cha unafiki na hakuna sababu ya kuwafanya waache kufanya hivyo.

’Kamati yetu inaamini kuwa mtu aliyetamka kusoma dua alifanya hivyo kujaribu kutishia,kwani tuna hakika kuwa hajui kusoma dua hiyo, hakupata ijaza yake na kama kweli itasomwa itawadhuru wao wenyewe’ alisisitiza.

Aliongeza kuwa ahla badri haitomdhuru mtu yoyote asiyekuwa na hatia.

Hata hivyo, alisema dua hiyo haiwezi kumwacha mtu mzushi na mwongo anayetumia dini kama kigezo cha kusababisha chuki, uhasama baina ya wanadamu na wanajamii kwa ujumla.

Kadhalika, Kamati hiyo imetoa wito kwa Waislamu wote kutolifanya sakata La Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuwa
ni mapambano dhidi ya Uislamu.

’Watu wanaotaka tuamini kuwa mgogoro wa fedha za NSSF ni Uislamu ni jambo ambalo halina maana na ni upotoshaji mkubwa wa misingi ya dini ya Kiislamu’ alisisitiza.

Alisema suala hilo liko Mahakamani na kwamba wanayo imani kuwa uamuzi wa hakika juu ya usahihi wa matumizi ya fedha hizo utatolewa na chombo hicho cha juu na si kwa vitisho vya kipuuzi vya kusoma ahla badri, wala kuchochea chuki za kidini kupitia msikiti.

Aidha, Kiongozi huyo alisema baada ya kuangalia madhumuni ya kuundwa kwa mfuko wa NSSF na lengo la serikali kuweka uongozi wa kusimamia hakuna mahali palipoandikwa kuwa ikiwa kiongozi wa mfuko akiwa ni Mkristo au Mwislamu mfuko huo utakuwa kwa manufaa ya dini ya kiongozi huyo.

’Kwa msingi huo tuhuma kwamba wanaohoji uhalali wa matumizi ya fedha hizo za wananchi wanaupiga vita Uislamu, hazina msingi kwa kuwa mfuko huo si wa Kiislamu na hauendeshwi kwa misingi ya Kiislamu’ alisema.

Alisema daima Uislamu unamtaka kila mmoja kutumia busara na kuchunguza kama taarifa aliyopokea inayo ukweli au la.

Kadhalika, Kiongozi huyo alisema wakati umefika kwa Waislamu nchini kote kukataa kutumiwa na baadhi ya wahubiri wa dini hiyo kuwatumbukiza katika kujenga chuki na hasara zenye misingi ya kidini pasipokuwa na sababu za msingi jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Uislamu.

Kuhusu sakata la kiwanja cha Chang’ombe, -alisema Kamati yake imemtaka Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba kutoa taarifa ya tume yake hadharani ili waumini wote nchini wafahamu kilichogunduliwa wakati Tume yake ikifanya uchunguzi wake na hivyo kusababisha watumishi saba wa BAKWATA kutimuliwa kazini.

Kadhalika,Kamati hiyo imemtaka Mufti Mkuu kuwaeleza waumini hatua gani za kisheria atakazochukua dhidi ya watuhumiwa walioghushi miuhtasari na nyaraka mbali mbali na kubadili miliki ya kiwanja cha Waislamu.

Hata hivyo, Sheikh Khamis alikana kupewa chochote ili kuzungumzia masuala hayo bali amefanya hivyo kwa mujibu wa Uislamu unaomtaka kila watu kuwa wakweli.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.