Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Sh. bilioni moja kwa kila mkoa ziko tayari
Sh. bilioni moja kwa kila mkoa ziko tayari
By Habari Tanzania | Published  10/27/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
.Sasa kuanza kutolewa na benki
.Ruksa kwa watu binafsi, vikundi
 
Na Ramadhan Mkoma
 
AHADI ya Rais Jakaya Kikwete ya kutoa mikopo sh. bilioni moja kwa kila mkoa kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wananchi, sasa imeiva baada ya Benki Kuu ya Tanzania kutiliana saini na benki za CRDB na NMB kwa ajili ya kuanza kuitoa.
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali aliyasema hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa Ballali, makubaliano kati ya benki hizo na BoT, yalifikiwa Jumatatu, wiki hii, na kwamba mikopo sasa itaanza kutolewa wakati wowote.
 
Alisema katika kufanikisha utoaji wa mikopo hiyo, BoT itatoa mafunzo maalum ya masuala ya mikopo kwa maofisa 2,000 kutoka benki hizo.
 
Ballali alisema CRDB na NMB zitatoa nusu ya fedha zilizotengwa na zingine zitatolewa na benki za ukubwa wa kati baada ya kuingia mkataba na BoT.
 
Alizitaja benki zingine kuwa ni Posta, Dar es Salaam Community, First Adili na Akiba Bankcorp.
 
Katika kufanikisha utoaji wa mikopo hiyo, alisema tayari Benki Kuu imeainisha kanda tano ambazo maofisa hao wataanza kutoa huduma hizo.
 
Alizitaka kanda hizo kuwa ni Kanda ya Ziwa inayohusisha mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Kagera; Kanda ya Kusini itakayojumuisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Sumbawanga na Ruvuma.
 
Kanda ya Kaskazini itakayokuwa na mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Singida, Tanga na Manyara; Kanda ya Pwani itakuwa na mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Lindi na Mtwara.
 
Alisema mikopo hiyo, itayokuwa na riba ya asilimia 10, itatolewa kwa watu binafsi, vikundi na kwa Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS).
 
Kuhusu kiwango cha fedha, alisema kila benki itajiwekea utaratibu wa kiasi cha kutoa na vile vile kuhakikisha mikopo inarejeshwa ili kuwawezesha wananchi wengine kukopa.
 
Wakati huo huo, Gavana Ballali amesema uchumi wa Tanzania uko katika mwelekeo mzuri licha ya matatizo yaliyojitokeza, ikiwa ni pamoja na shilingi kuyumba ikilinganishwa na dola ya Marekani.
 
Alisema hayo yanathibitishwa na kiwango cha ukuaji wa uchumi ambacho kilifikia asilimia 6.8 kwa mwaka jana ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika yaliyofikia asilimia 4.
 
Pia alisema katika kipindi hicho, mfumuko wa bei za bidhaa nao ulishuka na hadi asilimia 4 kutokana mafanikio yaliyotokana na mageuzi ya kiuchumi kwa kipindi cha miaka 10 sasa.
 
Kwa mwaka huu, alisema, licha ya matatizo yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na ukame na umeme, bado uchumi umekua kwa asilimia 5.9 ikilinganishwa na lengo la asilimia 7.2.
 
Kuhusu kuyumba kwa shilingi ikilingnishwa na dola ya Marekani, Ballali alisema ni hali ya kawaida pindi fedha ya nchi inapoachwa huru ili ‘ijitafutie’ nafasi yake dhidi ya dola za Marekani.
 
Alisema utaratibu huo ni mzuri na umekuwa ukitumika katika nchi mbalimbali, badala ya nchi kufikia maamuzi ya kuidhibiti fedha yake kwa kubadili thamani.
 
Ballali alitoa mfano wa mataifa ambayo yaliwahi kupitia hatua kama hizo kuwa ni ya Amerika ya Kusini na Poland ambazo kwa sasa sarafu zake zimeimarika.
 
Akifafanua, alisema hali ya kudorora inayoonekana sasa inatokana na madhara ya kiuchumi ambayo taifa limepitia katika kipindi kirefu na kwamba pindi yatakapokaa sawa hali hiyo haitajitokeza.
 
Ballali alitoa mfano katika miaka ya 1960 kwamba dola haikuthaminiwa na watu kwa vile shilingi ilikuwa na nguvu ikilinganishwa na sasa.
 
Alivitaja vigezo vungine vilivyochangia kuyumba kwa uchumi, mbali ya ukame, kuwa ni kupanda kwa bei ya mafuta na kupungua kwa mauzo ya nje.
 
Ballali alitoa mfano wa bei ya pipa la mafuta ambalo limepanda kutoka dola za Marekani 20 hadi dola 70, hali aliyosema imeziathiri nchi nyingi.
 
Alisema hali hiyo ilisababisha serikali kutumia dola bilioni 1.1 kwa mwaka jana pekee kununua mafuta ikilinganishwa na dola milioni 400 zilizotumika kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
 
Hata hivyo, alisema hali hiyo haikuathiri akiba ya fedha za kigeni ambazo hadi sasa ziko dola za Marekani bilioni 2.
 
Pia alisema serikali imechukua hatua mbalimbali za kuimarisha uchumi wake, ikiwa ni pamoja na kuongeza bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje.
 
Ballali alizitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na maua, mboga ambazo zitauzwa pamoja na samaki na dhahabu ili kuziba pengo la mazao ya awali ambayo yalikuwa yakichangia kuongeza mauzo ya nje.
 
Aliitaja mikakati mingine kuwa ni kuwepo kwa maeneo huru ya biashara na vile vile kuanzishwa kwa maeneo maalum ya kiuchumi chini ya utaratibu wa kampuni tatu kutoka Japan.
 
Alisema kampuni hizo zitahusika katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani zitakazouzwa nje ya nchi.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by washawasha)
    Rating
    Hiyo Bilioni moja haitosaidia kwa sababu Mafia ambayo ni kisiwa na wilaya ya mkoa wa pwani tunahitaji zaidi ya Billioni 2 ili kujenga bandari katika kisiwa che2 hiko sasa bilioni kwa mkoa ni vichekesho na ni ndogo vile vile.Serikali ongezeni hela hiyo
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.