Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Waziri Mwapachu na dawa ya msongamano wa magari Dar
Waziri Mwapachu na dawa ya msongamano wa magari Dar
By Habari Tanzania | Published  10/26/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
.Asema askari wataongezwa kuyaongoza
 
.Afanya ziara ya ghafla kwa helikopta
 
Na Mohamed Mhina wa Polisi
 
WIZARA ya Usalama wa Raia, imesema kuwa itaongeza idadi ya askari wa Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam na miji mingine yenye msongamano wa magari kusaidia kazi ya kuyaongoza kwa njia ya kubadilishana, ili kupuguza msongamano.
 
Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, aliyasema hayo jana baada ya kumaliza ziara ya ghafla ya kuzunguka maeneo yenye msongamano wa magari barabarani, aliyoifanya kwa kutumia helikopta.
 
Ziara ya Waziri Mwapachu ilianza saa 1.00 asubuhi na kumalizika saa 3.00 asubuhi na alifuatana na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Said Mwema, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Alfred Tibaigana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Polisi, Elice Mapunda.
 
Mwapachu alisema katika mkutano uliofanyika ofisini kwake baada ya ziara ya jana, kuwa ukaguzi wa jana utamuwezesha kuishauri serikali juu ya namna ya kupunguza tatizo la msongamano na hata kutunga sheria mpya au kurekebisha zilizopo kuhusiana na usalama barabarani.
 
Alisema, ziara imemuwezesha kubaini tatizo kubwa la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, unaosababishwa na matumizi mabaya ya barabara yanayofanywa na madereva wakiwemo wa mabasi ya daladala kupenya visivyo barabarani na mengine kuegeshwa hovyo.
 
Sambamba na hilo, jingine lililobainika kwa mujibu wa tathmini hiyo ni mabasi kusimama hovyo kushusha na kupandisha abiria kinyume na taratibu.
 
Waziri Mwapachu alisema baada ya vita dhidi ya ujambazi kufanikiwa, sasa hatua inayofuatia ni kupambana na adha ya msongamano wa magari barabarani.
 
Naye IGP Mwema, aliwaomba wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha polisi kupambana na wahalifu na wanaovunja sheria za barabarani na kusababisha ajali na maisha ya watu kupotea au wengine kubaki na vilema vya kudumu.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.