Na Mwandishi Wetu
JIJI la Dar es Salaam, ambalo lilianza kung’ara na kupendeza kutokana na kuchipuka kwa majumba ya vioo, huenda likabakia kuwa magofu ya kale baada ya serikali kutoa amri ya kuhifadhi na kuzuia kubomolewa kwa majengo zaidi ya 100, mengi yakiwa katika mitaa maarufu ya katikati ya jiji.
Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo, alitoa notisi katika gazeti la serikali la kuhifadhi majengo na maeneo katika jiji la Dar es Salaam na mikoa kadhaa kuanzia Julai mosi, mwaka huu.
Diallo, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, ametaja sababu za kuhifadhi majengo na maeneo hayo kuwa ni umuhimu wake kwa urithi, historia, michoro, uchumi, kijamii na utamaduni kwa taifa, kwa mujibu wa sheria ya mambo ya kale.
Majengo 30 yanayohifadhiwa katika mtaa wa Indira Gandhi, mjini Dar es Salaam, na majina yake ni Rajani, Khanga, Cosmos, Kanti Dadabhai, Metro, Sulemanjee, majengo ya Manzili na Jivan Hirji lililopo kwenye makutano na Mosque.
Mengine ni Kassum’s 1948, Sheikh Miji, Pentagon, Bajarang, Surat Cycle, Al-Saif Stationary, Hamza Alli Noor Mohamed, Riyaz Mansion na R.V 1936/Remtulla lililopo kwenye makutano na mtaa wa Asia, duka la Magereza, Kilimo Bora, K-A, GF, Ary Bhavani, Jani, Essajee, Textile na Babla Spare yaliyopo kwenye makutano na barabara ya Morogoro.
Mengine ni Shella Beach lililopo makutano na mtaa wa Nkrumah, Shashi House makutano na Jamhuri,Alli Remtula Kassam (Bata) makutano na mtaa wa Aggrey na Shri Hari Vilas makutano na mtaa wa Kitumbini.
Mtaa wa Jamhuri ni The Diamond Jubilee, R.K Auto Electic, Husseinali Bhimji, Chama Cha Mapinduzi (1932), Kurasini Shop, Gadhiri Nivas, Jaraj, Adhiya, Dar es Salaam Printer, BMTL, Suchak House na Masasi Sign-Writer and Standard Electronic katika makutano na mtaa wa Mrima.
Gujarat(1931) Topaz, Kanti(1936), Masumini Printways, Laxmin Nivas,Mussaji, Mums and baba(1936) na Manjis-Moraf na Tata madina yaliyopo kwenye makutano na mtaa wa Zanaki.
Yaliyotajwa kuhifadhiwa katika mtaa maarufu wa Samora ni Matasalamat Mansion, Acacia and New Acacia-1937, Alcove Restaurant, Prince Tanzania, Step, Kelvin House, Tanzania Publishing House, Melita, MC George House na Kassum’s, yaliyopo Makutano na mtaa wa Mkwepu na Quality Shivacom lililopo kwenye makutano na mtaa wa Mkwepu.
Katika mtaa wa Nkurumah majengo yenye kuhifadhiwa ni pamoja na Chox, Sham Niwas, National Tyre. co. ltd, Habib Punja Star na Deca lililopo makutano na mtaa wa Bibi Titi Mohamed.
Mtaa wa Mkwepu ni majengo ya Kassum’s Radio House-1938, No Man, New Palace Hotel iliyopo kwenye makutano na mtaa wa Makunganya.
Tanganyika Bakeries na Gemin Clothing yaliyopo mtaa wa Lindi; Trade Union Tanzania lililopo makutano ya mitaa ya Lindi na Bibi Titi Mohamed, Golden Computer Training Center na Mohsin yaliyopo Mtaa wa Bibi Titi Mohamed,Ibrahim Fancy lililopo mtaa wa Mkwepu, Sulemanji lililopo kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na mtaa wa Kaluta, MGM Bureau De Change lililopo barabara ya Morogoro na M/S Megji lililopo mtaa wa Makunganya.
Mengine ni Noor Manji mtaa wa Azikiwe; GTY mtaa wa Jamaat, Maemaid Bureau De Change mtaa wa Kaluta, Slamur mtaa wa Sewa; Posta ya Zamani barabara ya Sokoine Drive; Mahakama Kuu barabara ya Kivukoni Front.
Tanzania Legion kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Mazengo na Jengo la Ushirika lililopo Lumumba.
Soko la Kariakoo ni miongoni mwa majengo yanayohifadhiwa, ikiwemoshule ya sekondari ya Pugu, Bwalo la Polisi la Oysterbay, klabu ya Selander Bridge, Klabu ya Reli Gerezani, Klabu ya Gymkhana na hoteli za Palm Beach na Etiennes.
Mengine ni uwanja wa Ndege wa Mwalimu J K Nyerere, terminal zote mbili, Stesheni ya reli Dar es Salaam, klabu ya Parthenon na makaburi ya Jumuia ya Madola.
Mkoa wa Pwani majengo ya hifadhi ni maboma ya Utete Rufiji na Saadani, Bagamoyo ambapo Morogoro ni Mnara wa Sokoine uliopo Dakawa , Stesheni ya Reli, Uwanja wa Jamhuri, makazi ya chifu Kingalu Mahenge na Boma la Morogoro.
Dodoma ni Jengo la Bunge, makazi ya Chifu Mazengo, Makazi ya Sultani Salum Kimolo, Ntemi Joseph Siloti, Boma la Kondoa, Stesheni ya Dodoma, Hoteli ya Dodoma na uwanja wa Jamhuri.
Tabora ni uwanja wa ndege eneo la Kariakoo, Stesheni , Boma laTabora,Ntemi Fundikira, Kipalapala Seminary,chuo cha Ualimu Ndala,Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, uwanja wa Vita na Tabora Hotel.
Majengo yanayohifadhiwa Shinyanga ni Ntemi Muhelezi Lwasa na Chuo cha Uuguzi Kolandoto. Mkoani Mwanza ni uwanja wa Nyamagana, Hospitali ya Mkoa na kliniki ya Makongoro, makazi ya Mkuu wa Mkoa, Chuo cha Pasiansi, Utemini House na gereza la Butimba.
Kagera ni makazi ya Omukama Rumanyika, Omukama Rutinwa, Omukama Lukamba, uwanja wa ndege wa Duka Kubwa, Boma la Biharamulo na uwanja wa Kaitaba. Mkoa wa Kigoma ni ofisi ya Mkuu wa wilaya,nyumba ya mkuu wa mkoa wa Kigoma na Mwami Ruhaga.
Mkoa wa Mtwara maeneo yaliyotamkwa kuhifadhiwa ni Boma la Mikindani, uwanja wa Umoja, makazi ya mwenye Che Namilike, Mwenye Che Somanga, Mwenye Che Nkanga, Mwenye Che Nanumba na Boma ya Masasi iliyopo Mkomaindo, na majengo ya zamani ya shule ya kati ya wasichana katika kanisa la Anglikana Mtandi .
Kwa upande wa mkoa wa Ruvuma ni uwanja wa Majimaji, makazi ya Nkosi Nduna, Nkosi Tawete, Nkosi Mbawala na hoteli ya Ngoni Arms ambapo mkoani Iringa majengo yanayohifadhiwa ni makazi ya Chifu Mkwawa huko Kalenga, shule ya sekondari ya Tosamaganga na uwanja wa Samora Machel.
Mkoani Kilimanjaro maeneo ya hifadhi ni Moshi Bolt Hole (mahandaki yanayofahamika kwa Kichaga kama Mreshe) yaliyopo Mweka chini, German Kindergarten School ambayo sasa yanatumiwa kuwa majengo ya utawala katika chuo cha Mweka, Boma la Moshi, majengo yote yaliyokuwa makao makuu ya Wajerumani ambayo sasa ni shuke ya sekondari ya Koila, makazi ya Mangi Marealle, makzi ya Mfumwa Mbwambo yaliyo Bwambo wilayani Same, Mangi Sina Kibosho, Mfumwa Mmbaga, Same, Mangi Mashingia Kirua Vunjo Mfumwa Heriel Makange, Same na Mangi Mandara, Kiboroloni.
Shule ya Sekondari Lutengano kwa upande wa Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa majengo ya hifadhi, ikifuatiwa na Rungwe Sekondari, Boma la Tukuyu, makazi ya Malafyale Mwakalukwa, Malafyale Mwakatumbula, Malafyale Mwandosya na Mwalafyale Mwakang’ata.
Tanga ni shule ya zamani ya Sekondari ya Tanga, Boma la Handeni, Hoteli ya Mkonge na Mkonge House; ambapo mkoani Arusha ni Boma la Arusha, uwanja wa Sheikh Abeid Amani Karume na Kambi ya Dakta Mary Leakey.